Jinsi Ambavyo Mtizamo Wa Kijamii Hupelekea Wanaume Waendekeze Ngono....


Vile jamii inavyomuona na kumchukulia mwanaume ndivyo inavyomfanya awe hivyo.

Unatakiwa kujua kwamba huwa hauoni kitu kama kilivyo, bali huwa unakiona kitu kutokana na wewe ulivyo na jinsi ulivyoaminishwa kuhusu kitu hicho. 

Na ifahamikie kuwa, utaonesha mwitikio fulani kuhusu kitu hicho kutokana na fikra ulizonazo pamoja na Imani uliyonayo kuhusu kitu hicho.

Na hii ndiyo sababu kubwa inawafanya wanawake wengi wa leo wasiwaamini kabisa wanaume kuwa wanaweza kutulia na mwanamke mmoja. 

Kwa sababu hiki ni kitu kilichomo ndani ya fahamu zao, na siyo rahisi kuweza kukitoa kwa sababu hicho ndicho wanachokijua na ndicho wanachokiamini!

Kwa mfano jamii inamuona mwanaume kama mtu anayetakiwa; atunukiwe ngono kila anapohitaji haijalishi anahitaji kwa nani, mtu ambaye hawezi akakaa miezi mitatu bila kukutana na mwanamke, (na endapo itatokea hivyo anaweza kuwa chizi). Mtu ambaye huwa hatosheki kimapenzi, mtu ambaye ni kawaida kuwa na wanawake wengi, na mengine mengi kama hayo.  

Huo ni mtizamo usio na ukweli ndani yake, lakini cha ajabu dunia imeaminishwa kuwa wanaume wapo hivyo. 

Na wanawake wamelipokea hilo na wanaliamini wasijue kwamba, wanaume kama akina Yusufu bado tupo na tunaishi hadi leo. Ukipata muda kasome Mwanzo 39: 7-13.

Kutokana na hilo wanaume wamejikuta wakijihesabia haki kwa kupokea kile ambacho jamii inaamini kuhusu wao na kuanza kukiishi. 

Na wanawake nao wameamini kana kwamba ni kama haki kwa mwanaume kumsaliti, kuwa na wanawake wengi, kuhitaji penzi kila muda, n.k! 

Na endapo itatokea ukawauliza hao wanawake wathibitishe uhalali wa jambo hilo hawana uthibitisho, na hawawezi kukupa hoja zenye mantiki kama ninazozitoa hapa! 

Hali hii imepelekea usaliti kwa mwanaume lisiwe kosa bali kwa mwanamke liwe ni kosa kubwa.

Ndugu wanajamii, mmeamini katika upotevu na ndiyo maana mnapotezwa! Wanaume hawapo hivyo ila kwa sababu mmewatengenezea mtizamo huo kuhusu wao ndivyo mmewafanya wawe hivyo!

Na ifahamike kuwa kila mtu huitikia kufanya matendo kuhusu jambo Fulani kutokana na fikra zake zilivyo kuhusu jambo hilo!

Binafsi huwa sipendezwi kabisa na huu mtizamo kutuhusu! Ukweli ni kwamba wanaume hatukuumbwa kwa ajili ya kuwa watumwa wa ngono kama wengi mnavyodhani. 

Na huwa sipendezwi na wanawake wote wenye mtizamo huu kuhusu wanaume, kwa sababu huu ni udhalilishaji kwa ukuu na heshima iliyobebwa na mwanaume.

Unatakiwa kujua kwamba wapo wanaume ambao starehe yao siyo ngono kama ilivyozoelaka, kwa maana ngono ipo kwa ajili ya kuwastarehesha wanandoa tu na kwa ajili na uzazi! 

Cha ajabu jamii yangu imeamini kuwa tendo hilo ni kwa ajili ya starehe na wanawake tofauti tofauti.

Pengine labda hali hii ndiyo imepelekea hata wanawake waanze kujiuza kwa minajili ya kuwastaheresha wanaume! 

Binafsi huwa nashangazwa na mwanaume anayenunua wanawake wanaojiuza. Yaani unatumia fedha zako ulizozitafuta kwa shida kununua kitu kinachotumiwa na kila mwanaume?

Pole na hongera kwa kutumia fedha zako kununua; kifo, maradhi, mikosi, nuksi laana na mabalaa!

Kwa upande wangu huwa napingana na mtizamo wa jamii kuhusu wanaume! 

Na sijawahi kuikubali falsafa ya; “wengi wape” maishani mwangu. Kwa sababu tatizo siyo kuwa wengi bali tatizo wao ni kina nani hata kama ni Wengi?

Siwezi kuhalalisha wazo lililopo gizani eti kwa vile linaaminiwa na wengi. Maadamu nipo nuruni na niweza kutoa nuru halisi kuhusu jambo hilo, basi napinga vikali mtizamo huu. 

Ukweli ni kwamba, wanaume wanaweza wakatulia na mke mmoja na wanaweza kukaa muda mrefu bila kushiriki tendo!

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!

Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...