Ukuu Uliobebwa Na Mwanaume Ni Mkubwa Sana Haupaswi Utumike Kubadilishana Na Ngono....
Hivi unafahamu kuwa Mwanaume ni mtu mkuu sana ambaye jamii nyingi hujivunia uwepo wake?
Endapo utazunguka katika jamii nyingi ulimwenguni kote utagundua kuwa, mwanaume amefanywa kuwa kama kichwa.
Hii inamaanisha kuwa mwanaume ni mtawala, mwenye mamlaka na mbeba maono wa dunia ya sasa na hata ile ijayo!
Vilevile tafiti nyingi kuwahi kufanyika zimeonesha kuwa hata ugunduzi mkubwa wa kisayansi wa maeneo kadha wa kadha umefanywa na mwanaume!
Hata hivyo ukija kwenye maandiko matakatifu utagundua kwamba mwanaume ndiye aliyepewa ukuu.
Hii ni kwa sababu yeye ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuumbwa na kupewa mamlaka kutoka kwa Mungu. Na tunaona Mungu akamuahidi kuwa atamfanyia msaidizi.
Kwa kusema hivyo kumbe mwanaume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanaume. 1 Wakorintho 11:8-9
Hivyo basi, kama mwanaume huna budi ujitambue wewe ni nani, uko wapi, unaenda wapi na umebeba kusudi gani maishani mwako. Ikumbukwe wewe ni kichwa na umepewa mamlaka kuliko mwanamke.
Hii ni sawa na kusema kuwa kutumia muda wako wote wa thamani kwa ajili ya ngono na kufukuzia wanawake ni kugeuza mpango wa Mungu kukuumba.
Ikumbukwe hukuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke aliumbwa kwa ajili yako. Kwa hiyo kutumikia sana ngono ni udhaifu kwa sababu utakuwa unaishi kumtumikia mwanamke maisha yako yote ilihali hukuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke aliumbwa kwa ajili yako!
Ukija kusoma historia ya kuumbwa kwa ulimwengu hadi tulipofikia sasa, utakuja kugundua kuwa, hata Mungu mwenyewe hupendelea Zaidi kutumia wanaume katika kutimiliza kazi zake.
Na sababu za kuwatumia wanaume ni kutokana na ule ukuu walioumbiwa nao!
Kwa mfano alianza na Adamu kama mchungaji wake wa kwanza. Mwanzo 2:17. Adamu alikuwa mwanaume. Hakuweza kutunza agano kwa sababu alimsikiliza eva aliyedanganywa na shetani.
Akala lile tunda basi akapoteza mamlaka yote aliyokuwa nayo kwa sababu ya dhambi! Ikumbukwe mwanamke ndiye alikuwa chanzo cha anguko! Akafukuzwa bustanini! Mwanzo 3.
Baada ya hapo Mungu akaja kwa Nuhu, alikuwa wakiume. Mwanzo 6:8. Huyu alichaguliwa kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye haki.
Na alichaguliwa kama mchungaji wa kuokoa watu wakati wa gharika kuu. Na waliokolewa watu nane tu. 1 Petro 2:20 “…ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka maji”
Mbali na hilo baada ya kifo cha Nuhu, Mungu akaja kwa Ibrahim, naye alikuwa mwanaume. Huyu alikuwa ni baba wa Imani. Mwanzo 12:1-5.
Yeye ndiye chimbuko la taifa la Israeli ambalo Mungu alikuja akaliteua, likawa taifa lake teule! Mbali na kuwa mpaka sasa tuna waisraeli wa kiroho lakini chimbuko la Israeli ni Ibrahim.
Baada ya hapo akaja akamchagua Musa, Kutoka 3:1-10. Ili atimilize ile ahadi aliyomuahidi Ibrahim kuwa; "taifa lako litaingia utumwani nalo litatumikishwa na taifa lingine kwa muda wa miaka 400. Halafu nitakuja kulikomboa kwa mkono wangu wenye nguvu".
Musa aliliongoza taifa la Israeli kutoka misri lakini hakulifikisha nchi ya ahadi. Akafa, akazikwa na Mungu. Kumb 34.
Hata hivyo baada ya kifo cha Musa Mungu akamteua Yoshua, Yoshua 1:1-9. Naye alikuwa mwanaume vilevile. Huyu aliwaongoza wana wa Israeli kutoka Horebu halafu akawastaheresha katika nchi ya ahadi. Kwa hiyo hapa ahadi ya Mungu kwa Ibrahim ikawa imetimizwa!
Baada ya hayo waisraeli wakaiacha njia ya Bwana. Wakaanza kutumikia miungu mingine. Basi wakapotoka machoni pa Bwana. Na kwa vile Mungu ni mwingi wa rehema, na si mwepesi wa hasira bali huwasamehe watu wake makosa yao.
Akaahidi kuwaletea mkombozi taifa la Israeli. Huyu siye mwingine bali ni Yesu Kristo. Isaya 7:14.
Ukweli Yesu alizaliwa. Alikuwa ni mwanaume. Alikuja kulichunga taifa la Israeli na kurejesha ufalme wa Mungu hapa duniani.
Mathayo 4:17 “Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, tubuni kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”
Lakini unajua kuwa maandiko huwa hayatanguki, kama vile Yesu alivyokuja sawasawa na maandiko, naye aliishi sawasawa na maandiko. Basi bwana wakamtenda waliyotaka kumtenda.
Baada ya hayo walimsulibisha, akafa msalabani, akazikwa hatimaye akafufuka siku ya tatu kama yanenavyo maandiko! Zaburi 16:10
Akaahidi kuwa atakuja tena. Lakini kabla ya kuja kwake akatoa unabii juu ya ujio wake wa pili utakuwaje. Unabii huu upo kwenye vitabu vinne vya injili pamoja na kitabu cha agano jipya yaani ufunuo.
Na ndiyo maana kwenye ufunuo sura ya 12 anaoneshwa mtoto mwanaume anazaliwa, huyu mtoto anakuja kuwachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma, kama alivyoahidiwa katika ufunuo 2:27.
Je, kama mwanaume mkristo unamjua huyu mwanaume atakayezaliwa ni nani? Kama Hapana nina mashaka na imani yako! Kawaulize wachungaji wako na walimu wako huyo mwanaume ni nani na yuko wapi? Wakishindwa kukupa jibu nitafute tulijadili hili. 0744284329.
Hivyo ndivyo mwanaume ulivyobeba ukuu. Nimekuonesha hilo ili utambue kuwa katika ufalme wa Mungu wewe ni mkuu na hapa duniani umebeba ukuu vilevile.
Kwa mantiki hiyo hutakiwi kujichukulia poa tu wewe si wakawaida, wewe ni mtu mkuu sana.
Thamani uliyobeba ndani yako haipaswi kutumika huku ikibadilishana na ngono! Hiyo ni kufuru kubwa sana mbele ya Mungu aliyekuumba.
Ndugu mwanaume usiendekeze sana ngono, unatakiwa kujua kwamba ngono inaweza kukufelisha. Kwa kusema hivyo huna kuhakikisha unatambua kwanini upo hapa duniani.
Kama ulivyoona wenzako walotajwa hapo juu vile walivyotumika kama vyombo vilivyomsaidia Mungu kutimiliza kazi yake, vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwako. Hata wewe umebeba ukuu, mamlaka na uongozi.
Unachopaswa kufanya ni kutafuta mwanamke mmoja tu, kama wakati huu ni muafaka kwako kufanya hivyo, baada ya hapo anza naye kufanya maisha!
Kosa kubwa unalopaswa kuepuka ni kuwa na rundo kubwa la wanawake na kutaka kulala na kila mwanamke anayekatiza mbele zako!
Ndugu mwanaume upate kujua kwamba, ukizingatia
hekima ya Kimungu, hekima ya Mungu itakuambia kuwa; tendo la ndoa ni kwa ajili ya uzazi, na hili likitizamwa Kiungu lina mantiki.
Mwanzo 1:28 “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, zaeni mkaongezeke mkaijaze nchi na kuiitisha”. Na watu hawawezi kuzaana bila kufanya tendo la ndoa!
Hii ni sawa na kusema tendo la ndoa ni maalumu kwa ajili ya uzazi ijapokuwa huwa linastahresha na ni tamu sana!
Na ifahamike kuwa ngono yoyote ile inayofanyika huku ikiwa haijalenga uzazi maana yake inafanyika kwa minajili ya kupata starehe na raha na haya ndiyo mapinduzi yanayoendelea karne hii.
Kwa kusema hivyo wanaume wengi huhitaji ngono kwa minajili ya kustarehe tu na siyo kutii amri ya Mungu yaani kuzaliana!
Kwa maneno mengine tendo hili hivi karibuni linafanyika kiholela sana na wanaume wamekuwa wakidai ngono hadharani na wanawasaliti wake zao kwa kigezo cha kusema; “hakuna mwanaume ambaye hutosheka na mwanamke mmoja kitu ambacho siyo kweli”.
Haya mapinduzi yanayoendelea siyo Kweli na siyo halisi! Ndugu mwanaume usidanganyike wewe ni mkuu sana!
Wewe mwenyewe umeona uhalisia ulivyo, chukua hilo kama lilivyo halafu ishi nalo! Tambua ya kwamba wewe ni mtu mkuu na umebeba ukuu! Ndani yako!
Kwa kusema hivyo usitumie thamani yako kubwa Kubadilishana na kitu kisicho na thamani! Au ngono isiyo halali imebeba thamani?
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentaship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 Au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Comments
Post a Comment