Hii Ni kwa Wanaume Tu, Kama Una Nia Ya Dhati Ya Kuishinda Ngono ili utimize Kwanza Ndoto Zako Soma Hii...
Wanaume wengi wameichoka tabia ya kutumikia ngono na pengine labda wanatamani kuiacha lakini hawajui wafanye kipi.
Kutokana na hilo, wengi hujikuta wakijizuia kwa muda mfupi tu baada ya hapo hujikuta wakiteleza tena na kuyarudia makosa yale yale.
Huenda hata wewe ukawa umechoshwa kabisa na tabia hii, na kila ukijaribu kuacha, unaacha kwa muda tu. Baada ya hapo unajikuta ukitumikia tena ngono.
Unatakiwa kujua kwamba, kosa siyo wewe bali kosa ni kutumia mbinu zisizo sahihi katika kuacha huu utumwa usio na faida!
Ukweli ni kwamba, watu wengi wanajua wanachokitaka lakini ni wachache tu ndiyo wanaojua wafanye nini ili wakipate kile wanachokitaka.
Hii inamaanisha kwamba wanaume wengi wanatamani kuachana na utumwa wa ngono lakini ni wanaume wachache tu wanaojua wafanye nini ili waache utumwa huo.
Na hakuna kitu kizuri kama kufanya jambo kwa kutumia mbinu sahihi, kwa maana mwisho wake huwa ni kupata matokeo sahihi!
Hiki ndicho ambacho makala hii inahusu kwa maana inaenda kukuonesha kipi unatakiwa ufanye ili uishinde ngono kwa minajili ya kutimiza Ndoto Zako kwanza!
Hata hivyo kujua mbinu sahihi pasipo kuchukua hatua stahiki ni kazi bure, kwa kusema hivyo usipochukua hatua kwa kufuata ushauri ulioandikwa katika makala hii hutaiacha tabia ya kupenda ngono bali utabaki ukiendelea kuifanya tu.
Pia, unatakiwa kujua kwamba hakuna mtu atakayechukua hatua kwenye maisha yako pasipo uhusika wako.
Hii ni sawa na kusema kuwa kila kitu kilicho kwenye maisha yako kitabadilishwa na wewe mwenyewe.
Je, umechoka kuwa mtumwa wa ngono kama jibu lako ni ndiyo, fanya yafuatayo:-
1. Amini Kwamba Unaweza Ukaishi Bila Ngono
Kuamini ni kupokea kuwa jambo Fulani ni kweli hata kama jambo hilo siyo kweli. Hivyo basi endapo utaamini kuwa unaweza ukaishi bila ngono, itakuwa hivyo na itawezekana kabisa kwa sababu umeamini hivyo.
Na ifahamike kwamba kuamini ni jambo ambalo huanzia ndani ya nafsi yako, ndipo sasa hujidhihirisha nje ya maisha yako.
Mbinu hii niliitumia na ilifanya kazi, na niliweza kukaa muda mrefu pasi kufanya ngono, kwa sababu niliamini kuwa ngono siyo kila kitu katika maisha yangu, badala yake sasa nilitambua kuwa kusudi la kuumbwa kwangu ndiyo kila kitu.
Kwa kusema hivyo nilipojiaminisha kuwa kitu hiki hakina umuhimu kwangu kwa wakati huo, ubongo wangu ulikipokea baada ya hapo ukawa haunichochei nifanye hivyo.
Hiki ndicho kitatokea kwenye maisha yako, kwa maana ubongo wako huongozwa na kanuni ya kuamini inayosema; “chochote kile utakachokiamini kuhusu wewe na dunia yako kitafanyika kwako na dunia yako kama vile ulivyoamini”.
Ukweli ni kwamba ubongo wako huwa unaongozwa na sehemu mbili za akili, yaani Conscious Mind na Subconscious Mind.
Conscious Mind huchukua wazo Fulani na kuliamini kuwa lipo hivi ama vile, baada ya hapo wazo hilo hupokelewa kama lilivyo kwenya sehemu ya pili ya akili iitwayo Subconscious Mind.
Sehemu hii hulichakata wazo hilo na kuleta matokeo yanayolandana na kile kilichoaminiwa na Conscous Mind wakati wa kuwasilishwa kwake.
Na ifahamike kwamba sehemu hii ya akili iitwayo Subconscious Mind huna mamlaka nayo na huwezi ukafanya jambo lolote lile!
Na kila kitakachoaminiwa na Conscious Mind kuwa ni kweli hata kama siyo kweli, kitapokelewa kwenye Subconcious Mind kuwa ni kweli, matokeo yake kitachakatwa ili kuleta matokeo yanayolandana na kile kilichoaminiwa na Conscious Mind.
Na, ndiyo maana kanuni ya akili inasema; “Subconscious Mind hupokea oda na komandi zitokazo kwenye Conscious Mind na kuzikachakata ili kuleta matokeo yanayolandana na kile kilichowasilishwa”.
Hii ni sawa na kusema kuwa endapo utatumia Conscious Mind kuamini kuwa ngono siyo kila kitu kwako, jambo hilo litapokelewa na Subconscious Mind kuwa ni kweli ambapo litachakatwa, matokeo yake Mawazo ya ngono yatakuwa hayachochewi tena kwenye fahamu zako.
Binafsi niliweza kufanikiwa katika hili kwa kutumia mbinu hii, na kama mimi niliweza maana yake hata wewe unaweza.
Amini kuwa ngono siyo kila kitu kwako na unaweza ukaishi bila ngono kwa muda mrefu tu.
Baada ya hapo kuwa bize kutengeneza maisha yako. Unatakiwa uyape maisha yako kipaumbele kwanza na siyo ngono kwa maana unaweza ukaishia kuharibikiwa.
Ndugu mwanaume usiamini madai haya yasiyo na mashiko: “mwanaume hawezi kuishi bila ngono”, “mwanaume hawezi kumaliza miezi mitatu bila kufanya ngono”, “bila mwanamke unaweza ukafa”, “mwanaume anayeishi bila kufanya ngono ana matatizo”, “maisha ya wanaume bila ngono hayana Ladha”, “hakuna starehe tamu kama ngono”.
Hizo ni Imani za kuziepuka kabisa kwa maana endapo utaziamini Imani hizo ni rahisi sana kuteleza.
Kumbuka awali tumeona kwamba chochote kile utakachokiamini kuhusu wewe na dunia yako kitafanyika kwako na dunia yako kama vile ulivyoamini.
Niliamua kujitamkia kutoka ndani ya nafsi yangu kwamba, ngono siyo kitu muhimu sana kwangu, na Imani hiyo ikanifanya niweze kukaa bila kuchochewa kufanya ngono kwa muda mrefu tu, kwa sababu mfumo wangu wa ubongo haukuwa ukinichoea nipate Mawazo ya kufanya ngono. Matokeo yake nilifanikiwa katika hilo.
Wewe pia unaweza, kutoka ndani ya nafsi yako jitamkie kuwa; “ngono siyo kila kitu kwangu”, baada ya hapo jitamkie huku ukiwa na Imani kwa kusema, “sitaki tena kuwa mtumwa wa ngono, na nitakaa maisha yangu pasi na kushiriki mpaka pale nitakapokuwa tayari nimekamilisha mambo yangu”.
Ukishafanya hivyo dumu na imani hiyo mpaka pale utakapoona umeshakamilisha ndoto zako na upo tayari hata kuoa, baada ya hapo unaweza ukamtafuta mwanamke wako ukaoa, na maisha mengine yakaendelea.
Amini kwamba unaweza kukaa bila ngono, kumbuka kuamini ni kupokea kuwa jambo Fulani ni kweli hata kama jambo hilo siyo kweli. Maadamu umeamini kuwa ni kweli nalo litakuwa kweli!
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika kingmentorshipprogram.blogspot.com
Comments
Post a Comment