Hizi Ndizo Baraka Zilizobebwa Na Maisha Yako Ukiwa Unaadhimisha Siku Yako Ya Kuzaliwa...

Hbd to me, nawashukuru wazazi Wangu pamoja na Mungu mwenye vyote kwa Neema na rehema kwa maana hadi kufikia hapa nilipo haikuwa kazi rahisi! 

Ninapoadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa Kwangu nachelea kukufahamisha kuwa, maisha ni kuishi na siyo kufanya majaribio!

Kwa hiyo hutakiwi tu kuishi kwa sababu umepewa uhai bure, bali unatakiwa uishi kwa sababu kuna maono na kusudi ulilolibeba linalofanya maisha yako yawe ya thamani!

Mnamo tar 23/08/199... Alizaliwa kijana mmoja hivi aitwaye Emmanuel Samuel!

Kuzaliwa kwake ulikuwa ni ushindi mkubwa sana kwa sababu kila mtu hushinda kwanza ili apate kuzaliwa, na hakuna mtu ambaye huzaliwa huku akiwa hakushinda! 

Kijana huyu hakuishia kushinda mara moja tu, hata sasa ni mshindi kwa sababu ameushinda ulimwengu kwa kuzaliwa upya kutokana na mbegu ya Mungu isiyoharibika!

1 Yohana 5:4 " Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu"

Ukweli ni kwamba tunaishi kwenye ulimwengu ambao unatuhitaji tupigane vita nyingi sana, lakini kwa vile tunaye yule Mungu wa yawezekanayo ndiyo maana daima hubaki kuwa washindi na tutazidi kushinda!

Hata hivyo tafiti zimeonesha kwamba, kila Kitu kinachoishi hapa duniani nyuma yake kuna sababu za uwepo wa maisha yake...

Kutokana na hilo kijana huyu mdogo alianza kufanya udadisi juu ya uwepo wa maisha yake hapa duniani, kupitia kujiuliza maswali mbalimbali kama ifuatavyo; " Kwanini niliumbwa?" na "Kwanini ninaishi?"

Baada ya kujiuliza hayo kwa muda mrefu ndipo akabaini ya kuwa, kuzaliwa kwake hakukuwa kwa bahati mbaya bali kulitokana na mpango wa Mungu, hii inamaanisha kwamba Mungu alishampa jukumu la kuja kufanya ili kuisimamia  nchi kavu kwa kuifanya iwe sehemu salama!

Baada ya kugundua kuwa kila kiumbe kina jukumu lake, akaanza kujiuliza sasa jukumu langu ni lipi ambalo ninatakiwa niisimamie nchi kavu?

Aliwaza sana... baada ya hapo akaamua kuchunguza mtindo wa maisha yake kwa umakini pamoja na vile vitu anavypopenda kuvifanya. Na ifahamike kwamba huwa hatupendi vitu bila sababu!

Hatimaye akabaini kuwa mtindo wa maisha yake umetawaliwa na kuandika mada mbalimbali pamoja na kufundisha watu katika vipengele mbalimbali vihusuvyo maisha kitu ambacho siyo rahisi kufanywa na kila mtu... 

Ndipo sasa akabaini kuwa aliumbwa ili; "kuleta nuru na kufukuza giza kwenye fahamu za watu wengi na kuwafanya watu hao wajitambue kupitia kukiishi kipaji chake cha uandishi"

Yes kumbe Mr Emmanuel ni mwana wa nuruni na kila alipo, basi huweza kuangazwa na ile nuru ya mwanga wake aliyoibeba!

Ikiwa ni kumbukizi ya kuzaliwa kwake hapa duniani, Mr Emmanuel Samuel anajivunia uwepo wa maisha yake kwa sababu tokea ameanza kuliishi jukumu aliloumbiwa maisha yake yamefanyika kuwa baraka kwa watu wengine na ameweza kuponya fahamu za watu wengi sana!

Si hivyo tu, pia, Mr Emmanuel amefanikiwa katika kuanzisha huduma ya usimamizi ikifahamika kwa jina la King Mentorship Program ambayo hutolewa kwa miezi mitatu tu kwa kufanya watu wajitambue na wafanikiwe kwa urahisi zaidi katika kuishi kwao hapa duniani!

Mbali na hilo Mr Emmanuel anajivunia uwepo wa maisha yake kwa sababu ameweza kutoa ushauri kwa watu wengi sana na kupitia ushauri huo watu hao wametoka kwenye hali Mbaya na kwenda kwenye hali bora zaidi kimaisha! 

Vilevile Emmanuel Samuel anajivunia uwepo wa Maisha yake kwa sababu mpaka sasa ameweza kuandika VITABU kadhaa ambavyo vimeweza kubadilisha maisha ya wengi!

Kwa mfano mnamo tar 23/08/2023 Mr Emmanuel Samuel alifanikiwa kuchapisha KITABU kiitwacho; "Sikuja Duniani Kwa Bahati Mbaya; Bali Nilizaliwa Kwa Kusudi Maalumu " ambacho kilitolewa bure Kabisa, ukweli ni kwamba kiliweza kuwasaidia wengi sana na kupitia KITABU hicho wasomaji wengi walifahamu kuwa maisha ni Kusudi!

Si hivyo tu, hata sasa kuna KITABU kakiandaa, kinachohusu nguvu ya maono; kinachambua kwa undani kabisa ya kwamba kila mtu aliye hai na anaishi amebeba maono anayotakiwa ayaishi ili audhihirishe ukuu wake ikiwa ni pamoja na kurahisisha maisha ya watu wengine pamoja na maisha yake! 

KITABU hicho kiliahidiwa Kutoka rasmi siku ya leo Lakini kutokana na kubanwa na ratiba hakijakamilika, naomba radhi kwa kushindwa kutekeleza ahadi,  tafadhali elewa ndani ya mwezi huu kitakuwa tayari! 

Kwa hiyo  huna budi kukaa mkao wa kula kwa sababu ndani ya siku chache zijazo kitakuwa tayari, habari njema ni kwamba, kila mtu atakayesoma atapata kujua, amebeba maono gani kwa ajili ya maisha yake, kwa ajili ya jamii yake na kwa ajili ya nchi yake!

Nimatumaini yangu utakuwa tayari kujipatia KITABU hicho, kama Jibu lako ni ndiyo jibu ujumbe huu kwa kuandika neno KITABU ili kitapotoka nikufahamishe.

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika kingmentorshipprogram.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...