Hii Ni Kwa Wanawake Tu, Fahamu Kuhusu Maeneo Muhimu Ambayo Unatakiwa Uyatengenezee Maono...

Ilishawahi kusemwa kwamba wakati mzuri wa kuitabiri kesho yako ni kuiandaa leo yako. 

Hata hivyo hakuna kesho mbaya kwa mtu mwenye maono mazuri kuhusu hiyo kesho, kwa sababu kile atakachokiona ndicho atakachokuja kukipata kama uhalisia wake!

Mbali na kuwa wanawake wote hawafanani, hawana ndoto sawa, hawana matamanio sawa, hawaoni mambo kwa namna moja lakini kuna baadhi ya mambo ambayo ni ya kawaida kwa maisha ya kila mwanamke. 

Mambo hayo ndiyo kila mwanamke anatakiwa ayatengenezee maono. Hata hivyo yapo mambo mengi sana ambayo kila mwanamke anatakiwa kuyawekea maono, lakini kutokana na uhaba wa nafasi nitajadili mambo Matano tu. 

Kwa kusema hivyo huna budi kuhakikisha kuwa unatengeneza maono yako kwenye mambo haya kama kweli una ndoto za kuishi kesho iliyo njema na yenye kuvutia. 

1. Maono Kuhusu Mahusiano, Ndoa Na Familia.

Kila mwanamke mwenye ndoto ya kuja kuolewa huna budi kuhakikisha kuwa unatengeneza maono juu ya familia ya ndoto zako, labda uwe umeamua kukaa bila kuolewa. 

Maadamu una mpango wa kuja kuolewa basi huna budi kuhakikisha kuwa unatengeneza maono juu ya vile maisha yako ya ndoa yatakavyokuwa.

Unatakiwa utengeneze maono juu ya mume wako wa ndoto vile atakavyokuwa mtu wa upendo, mwaminifu na mwenye kujali. 

Vilevile ni wajibu wako kutengeneza maono juu ya Watoto utakaozaa (pengine labda hata idadi yao) pamoja na vile mtakavyowalea vizuri kwa furaha, amani na upendo. 

 Hata hivyo ni jukumu lako kuhakikisha kuwa unatengeneza maono juu ya vile utakavyompenda mumeo kwa dhati ikiwa ni pamoja na kumfanya awe kila kitu kwako, huku na wewe ukiwa kila kitu kwake. 

Pia unatakiwa utengeneze maono vile ambavyo; mafanikio, amani, furaha, na upendo vitakavyodumu kwenye ndoa yenu. 

Unatakiwa upate maono juu ya vile utakavyokuwa unawajibika kama mama, kwa kuhakikisha kila kitu kwenye familia kinaenda vyema, na hakuna jambo hata jambo moja litakalokwenda kinyume!

Ukiachilia hilo unatakiwa utengeneze maono juu ya vile utakavyojitoa kwa ajili ya familia yako na kufanya inakuwa kila kitu kwako! 

Ndugu mwanamke bila shaka ukiagizwa utafute maua ya kupamba nyumbani mwako huwa unatafuta maua mazuri na yanayovutia. 

Vivyo hivyo ndivyo unavyotakiwa ufanye kwenye fahamu kwa kuzipamba kwa maono mazuri na yanayovutia kuhusu familia yako ijayo! 

 Unatakiwa kujua kwamba vile unavyolifanya jambo fulani liwe zuri na lenye kupendeza ndivyo unavyozidi kuongeza umakini wako katika jambo hilo. 

Hii ni sawa na kusema hutamkubali kila mwanaume eti kwa vile yeye ni mwanaume, bali utamkubali yule mwanaume anayelandana na maono uliyonayo kuhusu familia yako! 

 Hata hivyo unatakiwa kujua kwamba kile unachokiona ndicho unakipata, kwa kusema hivyo endapo utatengeneza maono mazuri kuhusu familia yako ijayo ndivyo utakavyofanikiwa kutengeneza familia bora! 

 Ewe mwanamke unatakiwa ujue kwamba mwanamke huwa haolewi kwa ajili ya kufua tu, mwanamke huwa haolewi kwa ajili ya kupika tu, mwanamke huwa haolewi kwa minajili ya kuwa mama ya nyumbani, na mwanamke huwa haolewi kwa ajili ya kuzaa tu. 

Endapo unafikiri utaolewa kwa ajili ya haya, wewe bado huna maono, samahani sana tuliza kitenisi utengeneze maono kwanza mama! 

Ukweli ni kwamba hayo yote ni mambo ya ziada tu, lakini jukumu lako kubwa ni kuhakikisha kuwa unajenga familia kwa kuilea kwa misingi bora na kufanyika kuwa baraka kwa mumeo na kwa familia yako. 

 Ewe mwanamke unatakiwa kujua kwamba kuolewa siyo kuteseka, kutaabika wala kunyanyasika. 

Wengi hutaabika kwa sababu walikosa maono. Badala yake waliishi kwenye ule ulimwengu usemao; “liwalo na liwe” na ndiyo maana mwisho wao umekuwa mbovu. 

Kwa kuwa wewe ni wa kipekee ni wajibu wako kuhakikisha kuwa unatengeneza maono yako ili kile unachokiona kije kitokee kama kitu halisi kwenye maisha yako. 

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!

Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...