Jinsi Ambavyo Tamaa Huwafanya Wanaume Waendekeze Ngono...
Kuwa mwanaume haina maana kwamba umtamani kila mwanamke unayemuona, ni kweli kutamani kupo sikatai, Lakini kutaka kummiliki kila mwanamke unayemtamani ndipo utata unapoanzia!
Cha kustaajabisha ni kwamba kuna baadhi ya wanaume ambao huwa wanaendekeza tamaa kiasi kwamba hutaka kummiliki kila mwanamke wanayemtamani!
Na ndiyo maana hata wakiwa barabarani, kazini, ofisini, mtaani ama popote pale watakapokuwepo, basi wanaume hao huwa macho juujuu kutazama wanawake wanaopita maeneo hayo.
Hali hii hupelekea hata wengine kupata ajali kutokana na kuweka umakini wao wote kuangalia wanawake na siyo kuweka umakini wote kwenye kile wanachokifanya!
Hili ni jambo la ukweli kabisa wala si uzushi, huenda labda kutokana na hilo ndiyo maana wanawake nao wamekuja na staili mpya ya kuvaa nguo zinazowachora miili yao yote ili kuwatega wanaume, wameamua hata kutumia njia mbalimbali kama vile, vidonge, surgery n.k, ili kujaza nyonga na maumbile yao lengo likiwa ni kuwanasa wanaume na wengine wameamua kufanya biashara ya miili yao!
Hawa wote wanatumia udhaifu wa wanaume yaani tamaa zao! Ukweli ni kwamba hakuna kitu kibaya kama mtu kuujua udhaifu wako.
Na ifahamike kwamba, yule anayemjua mtu mwingine ndiye mjanja! Kwa kusema hivyo, ujanja wa wanawake kujua udhaifu wa wanaume (tamaa zao) umewafanya wao wanufaike huku wanaume wakipoteza!
Unatakiwa kujua kwamba kutokana na tamaa wanaume wengi wamekuwa wakipoteza fedha, kazi nzuri, afya bora na utajiri, kwa sababu ya udhaifu wao wa kushindwa kujizuia.
Hii inamaanisha kwamba tamaa inamfanya mwanaume ayagharimu hata maisha yake ili apate Ngono!
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba wapo baadhi ya wanaume ambao hufanya kazi ngumu, katika mazingira magumu na mateso mengi, lakini fedha zao zote huishia kutimiza tamaa za kingono!
Mnamo mwaka 2012 nikiwa kijana mdogo niliweza kufanya kazi kwenye kampuni Fulani hivi. Tulipokuwa tupo site, nilimsikia mwanaume mmoja akisema; “fanya kazi Malaya akapone”. Binafsi nilishangazwa sana na kauli hiyo.
Si haba hata leo hii kukawa kuna baadhi ya wanaume ambao wanafanya kazi ili Malaya wakapone! Poleni sana!
Ndugu mwanaume usidanganyike, hufanyi kazi kwa ajili ya Malaya bali unafanya kazi kwa ajili ya nafsi yako, kwa hiyo badala ya kumlipa malaya jilipe Kwanza wewe! Hii ni kanuni ya kitajiri!
Unatakiwa kujua kwamba tamaa ndiyo humsukuma mwanaume asafiri hata umbali mrefu kwa kutumia gharama nyingi sana kisa ngono ya saa tu, na sisemi hivi ili niweze kuwafanya muwe mabahiri! Lahasha! Ukiwa na mwanamke wako mhudumie!
Yupo mwanaume mmoja hivi ambaye leo hii yupo radhi hata alale njaa kwa dhumuni la kupata penzi.
Leo hii kuna mwanaume mmoja hivi ambaye kimaisha hajatulia, mipango ya maisha hana, lakini akishika fedha tu inaishia kuhonga wanawake kwa ajili ya kuridhishwa kingono.
Tamaa! Tamaa! Tamaa! Imechangia kuwapoteza wanaume wengi sana!
Ukweli ni kwamba tamaa huwa haziishi, na hata kama utakuwa na tamaa nyingi kiasi gani bado huwezi ukawamaliza wanawake wote hapa duniani Zaidi ya kujichosha na kujimaliza tu.
Wanawake hawataisha na kila leo wanazidi kuzaliwa. Ni suala la kuamua tu, yaani umchague mwanamke mmoja tu kati ya wengi halafu uridhike naye.
1 Petro 4:3-4 “Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi.... mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi uleule usio na kiasi wakiwatukana."
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentaship, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0673184329 au tembelea blog yangu kwa kuandika kingmentorshipprogram.blogspot.com
Comments
Post a Comment