Unaweza kuwa Yeyote Yule...
Dunia ni wewe unachotaka kuwa, na asili ya Dunia huwa haimfungi mtu, badala yake sasa mtu huyo anaweza akajifunga mwenyewe kutokana na mawazo yake kwa kujiwekea ukomo juu ya pale anapoweza kufika kimaisha!
Na ifahamike kwamba, duniani hakuna vikwazo halisi zaidi ya vile vikwazo unavyojiwekea mwenyewe kutokana na mtindo wako wa kufikiri!
Kwa kusema hivyo umekuwa hivyo ulivyo, kwa sababu ndivyo ulivyotaka uwe, na kama hukuamua uwe hivyo inamaanisha kwamba kuna mifumo iliyokuamlia kwa kuwa hukuwa na chaguo jingine...
Kwa hiyo basi, endapo utaamua, unaweza kuwa yeyote yule na hakuna mtu wa kukuzuia.
Ukweli ni kwamba, hakuna cha kukuzuia wala kukusimamisha, bali ni wewe mwenyewe unaweza ukajisimamisha!
Rafiki, dunia ni mali yako, kuwa unachotaka! Hutakiwi kufungwa na utambulisho wa kutengenezewa tena, badala yake sasa unaweza ukajitengenezea utambulisho wako mwenyewe, na kuwa yule unayetaka uwe...
Leo hii huenda ukawa unatambulika kwa sababu ya kozi uliyosomea au kwa sababu ya kazi unayoifanya. Hilo pekee halitoshi.
Unachopaswa kujua ni kwamba, unaweza ukawa mtu mwingine kabisa endapo utaamua kubadilisha utambulisho wako.
Kwa mfano Mimi hapa ni mwalimu mtaalamu, lakini mpaka sasa watu wananitambuaje? Hakuna haja ya mimi kujitambulisha, jibu unalo mwenyewe! Na hilo Jibu ulilonalo ni ushuhuda tosha kabisa! Kwa Hivi Mimi nimekuwa uhalisia wa yule niliyetaka niwe!
Je, unataka kujua imetokeaje? Haijatokea kwa bahati mbaya, nilianza kwa kufanya maamuzi juu ya yule ninayetaka niwe, na hatimaye nimekuwa, na kama mimi nimeweza maana yake hata wewe unaweza!
Kwa maana moja ya kithibitisho tosha kwamba hata wewe unaweza ukafanya jambo fulani ni kwa sababu wengine wameweza kufanya jambo hilo!
Ndugu, hakuna mtu ambaye huzaliwa akiwa hawezi au hastahili.
Na ifahamike kwamba sote huja duniani tukiwa sawa, yaani: tukiwa uchi, wajinga, wenye kuogopa huku tukiwa hatujui kitu, lakini huwa tunaishia kupata matokeo tafauti katika maisha kutokana na maamuzi tunayoyafanya juu ya wale tunaotaka tuwe!
Je, unataka kuwa nani? Je, utafanya nini ili kuhakikisha unakuwa huyo unayetaka uwe?
Rafiki, unatakiwa kujua kwamba watu wakuu huamini katika; “vichocheo na matokeo, ikiwa watu wa kawaida huamini katika bahati”.
Hutakiwi kuamini katika bahati, amini katika vichocheo na matokeo.
Kwa mfano kama unataka kubadili maisha yako lazima uorodheshe ni aina gani ya matokeo unayoyataka, baada ya hapo tafuta vichocheo vitakavyopelekea matokeo hayo!
Pengine labda unataka uwe mjasiriamali ili uuze bidhaa zako mwenyewe, kwa hivi huna budi kutafuta vichocheo vitakavyopelekea matokeo ya wewe kuwa mjasiriamali!
Hivi ni baadhi ya vichocheo hivyo; kutafuta wazo la bidhaa unayotaka kuuza, kujifunza namna ya kudhibiti mzunguko wa fedha, kuwa na nidhamu Binafsi, kufanya kazi kwa bidii na juhudi, kujifunza namna ya kuhudumia wateja, kujifunza bila kuchoka, kuchukua tahadhari pamoja na kuamini katika wazo lako na uwezo wako!
Ndivyo unavyopaswa kufanya kwa kuwa hakuna Kitu ambacho hutokea kwa bahati, ikumbukwe tunaishi kwenye ulimwengu wa oda na komandi!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0773284329 au tembelea blog yangu kingmentorshipprogram.blogspot.com
Comments
Post a Comment