Je Na Wewe Ulikuwa Ukifanya Kosa Hili Kwenye Ndoa Yako?

Katika ulimwengu huu mpana na ulio mkubwa sana, wapo watu wengi sana ambao huteseka kwenye eneo la ndoa!

Takwimu zimeonesha kwamba, wanaume wengi wamekuwa wakinyimwa haki ya tendo la ndoa na wake zao!

Ninaandika hivi kwa sababu huko nyuma nilishawahi kukutana na kesi kama hizi, ijapokuwa nilifanikiwa kuzitatua!

Nilijiuliza sana kwanini wanawake hao huamua kuwatesa wanaume zao kiasi hicho? 

Ndipo nikagundua kuwa hali hii inachangiwa na ujinga wa kutokujua kile ambacho Mungu kaamuuru kwenye neno lake kuhusu ndoa! 

Na ifahamike kwamba ndoa ni taasisi iliyoasisiwa na Mungu mwenyewe!

Katika Maisha haya nimegundua kwamba, ili ufanikiwe katika kitu fulani unatakiwa ujue Mungu kasema nini kuhusu hicho kitu, baada ya kujua ndipo sasa unatakiwa ufanye kama vile ambavyo ameamuru!

Hata katika haki ya kupeana tendo la ndoa Mungu kashatoa mwongozo unaotakiwa uzingatiwe!

Ngoja tuangalie andiko linasemaje, kuhusu hilo...

1 Wakorintho 7:3 “Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake bali mkewe”

Nimenukuu kifungu hicho ili utambue kwamba kwa wanandoa tendo la ndoa ni haki yao kabisa.

Tafadhali elewa maandiko! Maandiko hayajadokeza wachumba au wapenzi, ikiwa huna ndoa subiri kwanza mpaka uifikie hatua hii, niko hapa nazungumza na wanandoa tu! 

Na, kama andiko limeshaamuru inamaanisha kwamba, wajibu wako mkubwa uwe ni kutii tu kile kilichoamriwa!

Na endapo utamnyima mwenzi wako ilihali umeamriwa usifanye hivyo, maana yake utakuwa unaenda kinyume na maandiko matakatifu, ilihali maandiko huwa hayatanguki!

Kumbe sasa tukiwa watii kwa kile ambacho Mungu kaamuru, maana yake tutadumisha ndoa zetu kwa vile hatutapata upenyo wa kunyimana Tena!

Sasa inakuwaje umeoa/kuolewa halafu humtimizii mtu wako haki yake? 

Swali linakuja unataka akaipate wapi hiyo haki? Je, uliolewa/kuoa kwa lengo gani? Je, ulioa/kuolewa ili uwe gogo kitandani? 

Inakuwaje unaoa/kuolewa halafu unashindwa kumtimizia mwenzako haki yake ya ndoa?

Ndugu mwanandoa, hutakiwi kumnyima mtu wako. Akitaka mpe tena mpe bila masharti.

Siku moja mwanaume mmoja alinitafuta kwa ajili ya huduma ya ushauri. Katika maelezo yake alisema kuwa; 

“Mke wangu ananinyima haki yangu ya tendo la ndoa ni miaka miwili imepita sasa, na kwa sababu mimi sikutaka nimsaliti (yaani nitoke nje ya ndoa) nikaamua niwe najichua ili nipunguze tu hamu kwa minajili ya kufidia ile haki  aliyotakiwa anipe.”

Hakuishia hapo akaendelea kusema.... "Nimeweza kujichua kwa muda wa miaka miwili sasa, kwa hiyo naona kuna athari nimeipata kwenye nguvu zangu za kiume, kwa sababu uume wangu hausimami tena. Hapa nilipo sijielewi kabisa na akili yangu haifanyi kazi vizuri, na hata nikijaribu kulala sipati usingizi vizuri."

Akahitimisha kuwasilisha kesi yake kwa kusema; “Ninaamini kesi yangu utaitatua kwa sababu nimeona wewe mtumishi utaweza. Binafsi sijaona mtu wa kumueleza shida yangu isipokuwa wewe…”

Nakumbuka niliishiwa nguvu kwa kile alichosema. Baada ya hapo nikampa pole, halafu nikasema; “kesi yako imeshaisha na utakuwa sawa muda mfupi ujao” 

Nikaanza kutafakari ukatili wa ajabu unaofanywa na mke wake, kiukweli sikupata jibu. 

Nikajikuta nikisema; “Ewe mwanamke kwanini unamtesa mumeo kiasi hicho? Kwanini umemuingiza mume wako kwenye tatizo kubwa kama hili, hii dhambi ya kujichua ni nani ataibeba?”

Baada ya hapo nilimuweka sawa kwanza kiakili, kwa kutoa kile kitu kilichokuwa kinatatiza akili yake isifanye kazi vizuri!

Nilipomaliza nikamfundisha mazoezi anayotakiwa kufanya ili kuimarisha misuli ya uume wake!  Hata hivyo nikamtajia aina ya vyakula anavyopaswa kula ili arejeshe heshima yake ya kiume!

Namshukuru Mungu alibadilika mapema sana, akawa vizuri kiakili na kimwili yaani kibaiolojia.

Baada ya hapo nikampa jukumu la kumchunguza mkewe kimya kimya, akabaini kuwa mkewe huwa anamsaliti, tena amamsaliti na mwimba kwaya, salute kwenu waimba kwaya haha 😅...

Halafu anajifanya anamuimbia Mungu ilihali hata neno lake halijui, huu ni upumbavu wa kiwango cha juu!

Hebu jaribu kuvuta picha mume anajichua ili asimsaliti mkewe, halafu mke anamnyima mume wake ili amsaliti na mwimba kwaya sauti ya tatu 😂😂😂

Umeona hiyo gemu ilivyo ngumu ee! Kwa kweli iliniumiza sana. 

Lakini namshukuru Mungu kwa kuwa tulilimaliza na wote wanaendelea vyema kabisa, na siku hizi mke hamnyimi tena...

Je, unataka kujenga mahusiano yatakayodumu? Kama jibu ni ndiyo basi usimnyime mwenzi wako.

Tendo la ndoa lina nafasi yake katika kudumisha mahusiano. Mpe mwenzi wako haki yake, ukimnyima utampa mwenzi wako nafasi ya kukusaliti, matokeo yake atatoka nje ya ndoa.

Kwa maana tafsiri ya kumnyima mwenzi wako ni sawa na kumwambia; toka kwangu nenda kwingine huduma kama hii inapatikana!  

Tuhitimishe kwa kuangalia andiko takatifu linachosema...

1 Wakorintho 7:5 “Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu” 

Rafiki, usimnyime mwenzi wako! Mpe haki yake! Hukuoa/kuolewa kwa ajili ya ufahari bali ulioa/kuolewa ili umtimizie mwenzi wako hitaji lake la kihisia! 

Sasa unapomnyima unataka alipate wapi? Kama kweli unataka kujenga mahusiano yatakayodumu basi epuka kumnyima mwenzi wako!

Hiki ni kipande cha KITABU changu kiitwacho; Mwongozo Wa Kujengeka Mahusiano Yatakayodumu, Hakuna Kuachana Tena ...

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri...

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0773284329 Au tembelea blog yangu kwa kingmentorshipprogramblogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...