Fahamu Tafsiri KUU MBILI Za Fedha...


Hivi unafahamu kuwa watu wengi wametingwa muda wote kutafuta fedha Lakini hawajui fedha ni nini?

Kwa mujibu wa tafiti binafsi nilizozifanya nimebaini kwamba, baadhi ya watu hawafahamu fedha ni nini, hali ambayo imesababisha wakutane na masumbufu mengi katika kuipata na hata kama wakiipata waishie kuipoteza!

Ukweli ni kwamba watu wengi wanajua jinsi ya kupata fedha, lakini hawajui jinsi ya kuidhibiti fedha yao isipotee!

Hii ni sawa na kusema tunatengeneza fedha kwa kile tunachokijua, na tunapoteza fedha kwa kile tusichokijua!

Unatakiwa kujua kwamba jambo hili hutokea likichangiwa na ukosefu wa maana halisi ya fedha miongoni mwa watu wengi!

Ikiwa hata wewe, ulikuwa unaamini ya kwamba fedha ni karatasi au sarafu, nataka nikuulize hili; huwa unafanya nini mpaka upate hilo karatasi (noti) au hiyo sarafu unayoiita fedha?

Unachopaswa kujua ni kwamba kile ambacho unafanya kabla hujapokea malipo ya noti au ya sarafu basi hicho ndicho fedha yenyewe...

Kwa Sababu kile ulichokifanya kimebeba thamani ndani yake, ndiyo maana, mara baada ya kukifanya kimekuvutia fedha maishani mwako!

Na endapo usingekifanya usingepokea malipo ya kifedha!

Je wewe ulikuwa unaelewa nini 
 FEDHA?
Na, je, huu mtizamo nilioudokeza umeuonaje?

Ngoja nikupeleke kwenye Tafsiri KUU MBILI Za Fedha 

 1. Tafsiri Ya Kwanza Ya Fedha...

Tafsiri Ya Kwanza Ya Fedha ni ile inayosema: "Fedha ni zawadi anayoipata mtu mara baada ya kutatua matatizo ya watu"

Hii ni sawa na kusema matatizo yaliyopo ni fursa, na endapo utaweza kutatua matatizo hayo basi watu watakulipa kwa sababu umewaondolea karaha na adha walizokuwa wanakutana nazo! 

Unatakiwa kujua kwamba, kama hauna fedha ya kutosha manake hakuna tatizo lolote la watu unalolitatua.

Hata hivyo huna budi kufahamu kwamba kiwango cha tatizo utakachotatua ndicho kitapima kiwango cha fedha utakachotengeneza!

➡️Ukitatua tatizo dogo: utatengeneza kiasi kidogo cha fedha!

➡️ Ukitatua tatizo la wastani: utatengeneza kiasi wastani cha fedha!

➡️ Ukitatua tatizo kubwa: utatengeneza kiasi kikubwa cha fedha!

➡️ Ukitatua tatizo la kitaifa: utatengeneza fedha katika kiwango cha kitaifa!

➡️ ukitatua matatizo ya kimataifa: utatengeneza fedha katika kiwango cha kimataifa:

Unachopaswa kujua ni kwamba, wewe ni mtatua matatizo, na kiwango cha tatizo utakachotatua ndicho kitapima kiwango cha fedha utakachotengeneza!

Na, ndiyo maana wahenga walisema, "kila mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba yake". 

Hii ni sawa na kusema utatengeneza fedha kutokana na ukubwa wa tatizo utakalolitatua...

Je wewe unatatua tatizo gani hapa duniani linalokufanya utengeneze FEDHA? 

Au, unasubiri watu wengine wakutatulie matatizo ili uwalipe?

Unahitaji kufikiri juu ya hili pamoja na kujipa tathmini ya kutosha!

Kama umeshajipa tathmini ya kutosha nakusihi kuwa mtatua matatizo ya watu ili ulipwe..

Na Kama unatatua tatizo tayari na unatengeneza kipato cha chini basi nakushauri upanue wigo wa kutatua tatizo hilo!

2. Tafsiri Ya Pili Ya Fedha...

Tafsiri Ya Pili Ya Fedha ni ile inayosema, "fedha ni mbadilishano wa thamani"

Hii inamaanisha kwamba watu hutumia fedha ili kubadilishana na vitu wanavyovithamini...

Kutokana na ukweli huu, huna budi kukubaliana na mimi kuwa fedha hufuata thamani ilipo! 

Na, hii ndiyo sababu iliyosababisha kutokea kwa msemo wa wahenga usemao; "maji hufuata mkondo"

Hii ni sawa na kusema, kama utakuwa ni mtu wa thamani fedha itakufuataa...

Hata hivyo, unatakiwa kujua kwamba thamani ya huduma au bidhaa hupimwa na vitu vikuu vitatu, yaani: 

➡️Upekee wa bidhaa/huduma inavyotolewa...
➡️ Uhitaji wa bidhaa/huduma hiyo...
➡️Namna bidhaa/huduma inavyotolewa...

Je, katika kuishi kwako hapa duniani ni thamani gani unayoitengeneza?

Je, unatengeneza thamani gani ambayo watu watakuwa tayari kubadilishana nayo?

Je, kutokana na thamani unayoitengeneza unaamini watu watakuwa tayari kutumia fedha zao ili wabadilishane nayo?

Rafiki, unatakiwa uwe mtu wa thamani ili uweze kuvuta fedha maishani mwako, kumbuka fedha hufuata mahali pale penye thamani!  

Pia, unatakiwa kujua Kwamba ni muhimu kuongeza thamani kwa kila jambo utakalotakiwa ulifanye...

Huenda ukawa ni mfanyakazi, nipo hapa kukushauri kwamba, unatakiwa uongeze thamani katika kazi yako ili ulete matokeo mazuri, kwani kazini watu hawalipwi eti kwa sababu wanafanya kazi bali wanalipwa kutokana na matokeo wanayoyatengeneza!

Kama wewe ni mfanyabiashara basi huna budi kuongeza thamani katika utoaji wa hukduma yako ili uweze kuwashinda washindani wako! 

Na kama huna kazi maalumu, bado nakusihi uzidi kujifunza zaidi (Yaani jiongezee thamani ya kutosha), kwa kutafuta maarifa mengi ili ujitengenezee thamani ya Kutosha.

Unapaswa kujua kwamba siku hizi thamani ya mtu inapimwa kulingana na kiwango cha maarifa alichonacho, na sote tunafahamu fika kabisa kuwa maarifa ni nguvu. 

Hii ni sawa na kusema endapo utakuwa ni mtu mwenye maarifa mengi utakuwa ni mtu wa thamani, hivyo basi kuna uwezekano wa kuvuta fedha mahali popote pale utakapokuwepo! 

Tafuta maarifa ya kutosha ili ujiongozee thamani..

Mimi nafurahi sana kuwa hivi nilivyo na kila siku huwa najifunza vitu vipya! Wewe je?

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e, Founder Wa King Mentorship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/06773284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika, kingmentorshipprogram.blogspot.comu

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...