Je, Unataka Kufahamu kufahamu Tatizo ni Nini, Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...

Tatizo Ni  Hali Yoyote Ile Iliyo Kinyume Na Matarajio. 

Kwa Mfano tufanye Ulitarajia upate Furaha Maishani yako yote Lakini ikatokea Ukajikuta Ukikumbana Na Huzuni Zaidi kuliko furaha! 

Hii Inamaanisha kwamba Huzuni Ni Tatizo Kwako Kwa Sababu ni Hali ambayo ipo kinyume na kile ulichokitarajia yaani furaha!

Ina Maana Kwamba, Badala Ya Kukutana Na Furaha (Matarajio Yako) Umejikuta Ukikutana Na Huzuni Tu (Tatizo)…

Hata hivyo Kwa asilimia kubwa wengi wetu huwa tunatamani tuishi maisha mazuri kwa kutengeneza kipato kikubwa cha fedha (matarajio yetu), Lakini inapotokea tukawa  tunaishi maisha magumu huku tukitengeneza kipato cha chini linakuwa ni tatizo kwa sababu ni hali iliyo kinyume na matarajio yetu.

Na hii ndiyo sababu ambayo imesababisha umaskini uonekane kana kwamba ni tatizo!

Au Neno Tatizo linaweza kufafanuliwa kama kitu chochote kile ambacho huibuka kama kikwazo, ambacho husababisha kitu kingine kisitokee au kama kitafanyika kisifanikiwe! 

Kwa mfano kuwa na afya njema maisha yako yote ni haki yako ya kuzaliwa Lakini ukishambuliwa na ugonjwa ni tatizo kwa sababu unakuja kuathiri afya yako pamoja na kusababisha mwili wako ushindwe kufanya kazi kwa ufanisi!

Kwa hiyo kiasili unatakiwa udumu huku ukiwa na kuwa afya njema maisha yako yote na ndiyo maana kanuni ya maisha inasema; "
Na, kila palipo na watu pana matatizo mengi sana lakini siyo kila mtu huyagundua matatizo hayo!

Ukweli ni kwamba watu wengi wanapitia kwenye matatizo, na hawajui kwamba wanayapitia, kwa hivyo akipatikana mtu atakayetatua matatizo hayo basi ataweza kulipwa kupitia utatuzi huo!

Kwa hiyo mwisho wa kozi hii ni matumaini yangu utakuwa mtu utakayeweza kutatua matatizo ya watu, kwa maana umekuwa kiufahamu kiasi kwamba watu wote wapo kiganjani mwako!

Yapo Mambo Mengi Ambayo Wanadamu Hukumbana Nayo, Wakidhani Kuwa Ni Matatizo Ilihali Mambo Hayo Siyo Matatizo, Bali Tatizo Ni Wao Wenyewe Kwamba Hawana Uelewa Wowote Juu Ya Mambo Hayo Pamoja Na Kuwa Na Mitizamo Hasi Juu Ya Mambo Hayo.

Na, Ndiyo Maana Ishawahi Kusemwa Kwamba; "Tatizo Siyo Tatizo Bali Namna Unavyoliona Tatizo Hilo Ndiyo Tatizo Lenyewe" 

Hii Ni Sawa Na Kusema kuwa, Unaliona Tatizo Kutegemeana Na Wewe Ulivyo Na Siyo Kwamba Tatizo Hilo Liko Hivyo…

Ukiona Unakumbana Na Shida Au Changamoto Fulani Ambazo Hazikuzuii Usifanye Jambo Fulani Hayo Siyo Matatizo Bali Ni Maisha Tu… 

Yes Boss, Ni Sehemu Ya Maisha Tu Kwani, Hakuna Mtu Ambaye Huwa Hakumbani Na Tatizo, Adha Au Changamoto Fulani Bali Kila Mtu Hukumbana Nazo. 

Kwa Kusema Hivyo, hivi Ni Vitu Unavyotakiwa Upitie Ili Mradi Uko Hai. 

Na Kama Wewe Hutaki Ukutane Na Matatizo Ni Nani Unayemtaka Akutane Nayo?

Ndugu Matatizo Yapo Ili Kukoleza Ladha Maisha Yetu, Yes Yapo Ili Kuyapa Maisha Ladha… 

So, Kuanzia Saa Hii Hutakiwi Tena Kuogopa Kuhusu Matatizo!

Fahamu Ukweli Kuhusu Matatizo..

1. Matatizo Hayakwepeki...

Maisha Yetu, Ni Kama Shule Na Matatizo Ni Kama Mtihani ambao Tunatakiwa kuufanya na kuufaulu ili tupande hadhi au daraja!

Kuna Baadhi ya matatizo Ukishaanza Kuyatutua Tu Mpaka Cheo Chako Kitababadilika!

Kwa mfano Mara baada ya Kuanza Kutoa Huduma Ya Usimamizi Sasa Hivi Natambulika Kama Mentor!

Hii Ni Sawa Na Kusema Utambulisho Umebadilika Mara Baada Ya Kuanza Kutatua Matatizo Ya Watu.

Hivyo Basi Unatakiwa Kujua Kuwa Ukiwa Hai Kukutana Na Tatizo Ni Hali Ya Kawaida, Na Matatizo Hutukumba Ili Yatudhihidrishie Uwezo, Thamani, Ukomavu Wetu Na Ukuu Wetu.

Vilevile Matatizo Yapo Ili Kudhihirisha Ukuu Wa Mungu Wetu, Kwamba Kwa Macho Yako Uliona Hili Halitatatuliwa Ila Yeye Katenda Na Kaliondoa Kabisa, Kwanini Yeye Ni Mungu Wa Wazekenayo Na Si Mungu Wa Yasiyowezekana…

 2. Matatizo Yote Hutatulika.

Hakuna Tatizo Ambalo Huwa Halitatuliki.

Na, Ukiona Hakuna Njia Ya Kutatua TATIZO Maana Yake Hakuna TATIZO...

Kwa kusema Hivyo Mbinu Utakayotumia Katika Kulikabili TATIZO Ndiyo Itakayoliondoa TATIZO hilo au Ndiyo Itakayoliendeleza TATIZO Hilo... 

Na, Ukiona Hakuna Njia Ya Kutatua Tatizo, Maana Yake Hapo Hakuna Tatizo Kwa Maana, Matatizo Yote Hutatulika…

 3. Matatizo Ni Fursa.

Kila Tatizo Ni Mbegu Iliyopandwa Kwa Ajili Ya Fursa Zako. 

Matatizo Hudhiridhisha Thamani Yako Na Uwezo Wako. 

Kwa Mfano Kutokana Na Ukosefu Wa Elimu Ya Kujitambua Kama Tatizo Nimeanza Kutatua Na Ninalipwa, Na Thamani Yangu Inazidi Kukua Kila Leo..

Hii Inamaanisha Kutokana Na Uwepo Wa Matatizo Ya Watu Mimi Nimepata Fursa Ya Kutengeneza Kipato Pamoja Na Kujitengenezea Thamani Zaidi Na Zaidi...

Ndimi Emmanuel Samuel King’ung’e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 0744284329/0773284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika kingmentorshipprogram.blogspot.com 

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...