Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...

Siku Moja Nilikuwa Nikitafakari Kwa Kina Ni Kipi Hasa Chanzo Halisi Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? 

Na Kwa Vile Unaweza Ukaituma Akili Yako Irudi Miaka Ya Nyuma Huko Ikatalii Ili Ione Baadhi Ya Mambo Yaliyotokea Miaka Hiyo, Basi Nilifanya Hivyo Hatimaye Nikagundua Kuwa Matatizo Mengi Tunayokumbana Nayo Ni Ya Kutengenezwa!

Unaweza Ukawa Unajiuliza Tatizo La Kutengenezwa Ni Nini Na Lipoje Hilo?

Hili Ni Tatizo Ambalo Mtu Anakumbana Nalo Sasa Lakini Huko Nyuma Kuna Kundi La Watu Ambalo Lilihusika Katika Kulitengeneza Aidha Kwa Kujua Ama Kutokujua.

Na Kwa Vile Tatizo Hili Huwa Limetengenezwa Basi Hurithishwa Kutoka Kizazi Kimoja Hadi Kingine Bila Ya Kupatiwa Ufumbuzi.

Na Wengi Hulichukulia Kikawaida Sana, Matokeo Yake Hujikuta Wakiishia Kuhalalisha Kwa Kusema; "Tuishi Nalo Tu, Huenda Ndivyo Ambavyo Maisha Yetu Yalipaswa Yawe"

Kwa Mfano Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika, Yalitengenezwa Kipindi Cha Miaka Ya Nyuma Sana! Na Miongoni Mwa Hayo Yaliletwa Na Ukoloni!

Na Hata Hii Dharau Iliyopo Juu Ya Bara La Afrika Na Waafrika Imesababishwa Na Kitendo Cha Kuchukua Mitaala Ya Elimu Ya Kikoloni Iliyokuwa Ikiwakandamiza Waafrika Na Kuwadunisha Kifikra Ili Wasijitambue Wasije Wakagundua Kuwa Wanatawaliwa, Na Kuiingiza Kwenye Mifumo Yetu Ya Elimu Pasi Na Kuangalia Uhalisia Wa Mazingira Yetu Pamoja Na Kile Tunachopaswa Tukifanye!

Na Ikumbukwe Kwamba, Kabla Ya Ujio Wa Wakoloni Waafrika Walikuwa Na Elimu Yao Asilia! Mara Nyingi Ilikuwa Imelenga Zaidi Katika Kumfanya Huyo Mjifunzaji Aingiliane Vizuri Na Mazingira Yanayomzunguka Pamoja Na Kuyamudu Mazingira Hayo!

Rafiki Unatakiwa Kujua Kwamba, Moja Ya Tatizo Kubwa Sana Lilolotengenezwa Na Linatutafuna Wengi Wetu Ni Ujinga Wa Kutokujua! 

Ukweli Ni Kwamba Ujinga Huu Umerithishwa Kutoka Kizazi Hadi Kizazi Na Hata Sisi Wenyewe Tusipojielewa Tutaurithisha Kwa Vizazi Vyetu!

Jaribu Tu Kuwaza Unafundishwa Ya Kwamba Mwanadamu Alikuwa Sokwe, Aliyepitia Mabadiliko Kadhaa! 

Kwa Upande Wangu Sijawahi Kuona Umuhimu Wa Fundisho Hilo, Na, Ikiwa Mungu Ndiye Mwenye Vyote Na Kupitia Yeye Vitu Vyote Vilipata Kuwepo, Je, Kulikuwa Na Haja Gani Ya Kumuumba Sokwe Ili Abadilike Kuwa Mwanadamu Na Siyo Kumuumba Binadamu Moja Kwa Moja?

Usinielewe Vibaya Tafadhali Sipingani Na Mfumo, Lakini Kwa Vile Nimeumbwa Na Akili Ya Kuchanganua, Siwezi Kumeza Kila Kinachofundishwa. 

Nafahamu Fika Kabisa Ya Kuwa Kuna Vitu Vingine Hufundishwa Vikawa Sumu, Matokeo Yake Vikaishia Kuua Ubongo Wa Yule Anayefundishwa!

Sawa Tufanye Dogo Anamezeshwa Huko Ya Kuwa Mwanadamu Alikuwa Sokwe, Tunatakiwa Tujiulize Hili, "Hivi Hilo Fundisho Linaleta Badiliko Gani Kwenye Fahamu Zake?"

Swali La Pili, Mbona Masokwe Yaliyopo Sasa Hayabadiliki Na Kuwa Binadamu Tena? Na Kama Sisi Binadamu Tulibadilika Kutoka Hali Ya Usokwe, Je, Tunavyoendelea Kuishi Tunaweza Tukabadilika Tukawa Viumbe Gani Tofauti Na Vile Tulivyo Sasa? 

Huenda Tupo Kwenye Hatua Ya Mabadiliko Ndiyo Maana Sasa Hivi Tunafanya Matendo Ya Kinyama Zaidi Kuliko Hata Yale Yanayofanywa Na Wanyama Halisi Wa Msituni...

Hili Fundisho Hata Wewe Mzazi Ulifundishwa, Hata Wewe Kijana Unayesoma Ujumbe Huu Ulifundishwa, Na Pengine Labda Hata Watoto Wako Watafundishwa, Na Tunafundisha Hivyo Kwa Kuwa Tumepata Mpenyo Wa Kuishi Na Kutengeneza Fedha!

Tunapaswa Tujiulize Tena, Je, Haya Ndiyo Tulitarajia Tufundishwe Tukienda Shule?

Ujue Nini Tunaendeleza Ujinga Kwa Sababu Hatuwaulizi Wajifunzaji Kile Ambacho Wao Wanataka Kujifunza, Bali Tunawafundisha Kile Ambacho Sisi Tulikaririshwa Hata Kama Hakijatusaidia Na Wala Hakimsaidii Kabisa Yule Anayejifunza Katika Huu Ulimwengu Wa Kisasa! 

Vipo Vipengele Vingi Sana Ambavyo Wanafunzi Hufundishwa Ambavyo Binafsi Nikiviangalia Huwa Sioni Msaada Wake Kwenye Fahamu Zao, Na Ndiyo Maana Sasa Hivi Si Ajabu Ukakutana Na Msomi Kutoka Chuo Kikuu Ambaye Yu Mjinga!

Na Ikiwa Elimu Ipo Kwa Ajili Ya Kuondoa Ujinga, Halafu Mtu Anakuwa Amesoma Na Bado Akabaki Kuwa Mjinga Hii Ina Maana Gani! Je, Mtu Huyu Alienda Shule Ili Kufundishwa Awe Mjinga?

Ukitafakari Kwa Undani Ndipo Utabaini Kuwa, Kumbe Tatizo Huwa Siyo Ujinga Bali Kile Alichofundishwa Ndicho Ambacho Ni Tatizo Kwa Sababu Kimeshindwa Kuleta Badiliko La Fikra Kwenye Fahamu Zake!

Hata Kama Tunatakiwa Tujifunze Kutoka Kwenye Historia Lakini Ikiwa Historia Yenyewe Hainifundishi Vitu Vyenye Mantiki, Je Nitawezaje Kuleta Mawazo Yenye Mantiki Yatakayonisaidia Nibadilishe Maisha Yangu Na Jamii Yangu Kwa Ujumla? 

Unakuta Shuleni Mwanafunzi Hafundishwi Namna Ya Kuwa Mbunifu Badala Yake Anakaririshwa Mawazo Ya Watu Wengine Hali Ambayo Huua Kiwango Chake Cha Ubunifu, Hata Hivyo Mawazo Hayo Hukaririshwa Ili Ajibie Mtihani, Afaulu Ili Apate Vigezo Vya Kupata Ajira! 

Badala Ya Kufundishwa Namna Ya Kutumia Ubongo Kiubunifu Ili Afanye Mambo Yatokee, Yeye Anafundishwa Namna Ya Kuutumia Ubongo Wake Ili Kukariri, Kwa Bahati Mbaya Mambo Mengi Anayoyakriri Yameshapitwa Na Wakati!

Matokeo Yake Hata Yeye Atapitwa Na Wakati, Kwa Kuwa Kwenye Ubongo Wake Ameingiza Maarifa Yaliyopitwa Na Wakati, Na Ndiyo Maana Sasa Hivi Wasomi Wengi Hawana Cha Kufanya Kwenye Ulimwengu Huu Wa Sayansi Na Teknolojia Zaidi Ya Kuishia Kutumia Kwenye Ajira, Kwa Sababu Hawajajifunza Jinsi Gani Wanaweza Kukabiliana Na Ulimwengu Huu Unaobadilika Kila Leo

Swali Linakuja Kwa Namna Hii Ujinga Utaisha?

Wazazi Nao Wamekuwa Kimya Na Hawaoni Kuwa Kuna Tatizo, Kwa Sababu Hata Wao Wamepitishwa Kwenye Mfumo Sawa Kabisa Na Ule Ambao Watoto Wao Wanapitishwa!

Na Sababu Kubwa Inayosababisha Washindwe Kubaini Ya Kuwa Kuna Tatizo Ni Kwa Kuwa, Hata Wao Walikaririshwa, Wakabahatika Kupata Kazi Kupitia Mfumo Huo Na Maisha Yakaendelea!

Na Kwa Vile Wao Walinufaika Nao Ndiyo Maana Hutoa Shinikizo Kwa Watoto Wao Kwa Kuwaambia; "Nenda Shule Kasome Kwa Bidii, Upate Alama Za Juu, Uje Upate Ajira Serikalini Upate Mshahara Wa Maisha Pamoja Na Pensheni Wakati Wa Kustaafu Kwako Ili Ufurahie Maisha Yako"

Ndugu, Maana Kamili Ya Maisha Haimaanishi Kusoma Mambo Yasiyo Na Msaada Ili Upate Kazi Ulipwe Mshahara Kutokana Na Kile Unachokifanya Hapana Maisha Ni Zaidi Ya Hapo...

Tafadhali Usinielewe Vibaya Sina Maana Kwamba Elimu Yetu Haina Maana Kabisa! Lahasha! Yapo Mazuri Kwa Sababu Kupitia Elimu Hii Tumepata Madktari, Tumepata Wahasibu, Tunapata Wahandisi, Tunapata Walimu Na Wengine Wengi Wanaotumika Katika Sekta Mbalimbali!

Tatizo Linakuja Mbali Na Kuwa Na Manufaa Hayo Yote Ni Kwa Nini Kwenye Eneo La Ubunifu, Uvumbuzi Na Ugunduzi Tunakuwa Nyuma? Ndivyo Unavyopaswa Kujiuliza!

Hii Inamaanisha Kwamba, Hata Sisi Tusipofikiri Kwa Mapana Tutajikuta Tukiwapa Uzao Wetu Urithi Wa Elimu Tukidhani Ni Urithi Wa Thamani, Kumbe Usipofanyiwa Mabadiliko Utakuwa Ni Urithi Usio Na Maana Tena Matokeo Yake Utaishia Kuua Uwezo Wa Watoto Wetu!

Nini Kifanyike? 

Naona Unawaza Huyu Mwandishi Anataka Elimu Yetu Iweje Sasa! Kwa Upande Wangu Ninapendekeza Itolewe Elimu Itakayomfanya Mtu Ajitambue, Kwa Minajili Hiyo Elimu Inayopaswa Itolewe Ni Ile Ambayo Itaacha Kupima Mfumo Wa Ufaulu Kwa Kutumia Mitihani, Badala Yake Sasa Iwe Ni Aina Ya Elimu Itakayopima Kiwango Cha Ubunifu Na Uwezo Wa Mwanafunzi Kuunda Mambo Kutoka Vyanzo Mbalimbali, Iwe Ni Ile Elimu Itakayomuandaa Msomi Ajitegemee Na Asiwe Tegemezi, Iwe Ni Ile Elimu Itakayokuwa Imeegemea Katika Kukuza Maendeleo Binafsi Ya Mjifunzaji! 

Kwa Mujibu Wangu Hakuna Anayepaswa Kwenda Shuleni Kama Hatafundishwa: 

1. Elimu Ya Uchumi Na Fedha!
2. Nadharia Za Vitendo Kuhusu Namna Ya Kufanikiwa Kimaisha.
3. Jinsi Ya Kutengeneza Kipato Nje Ya Ajira.
4. Elimu Ya Ujasiriamali.
5. Kusudi Kuhusu Kusudi La Maisha Ya Kila Binadamu.
6. Elimu Inayohuhusu Vipaji Na Uwezo Binafsi Ambao Kila Mtu Huzaliwa Nao Pamoja Na Namna Ya Kuendeleza! 

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0773284329 Au Tembelea Blog Yangu Kwa Kuandika kingmentorshipprogram.blogspot.com

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...