Jinsi Ya Kuwa Mtu Usiyesimamishwa Na Chochote Kile...



Bila shaka ulishawahi kukutana na wale watu ambao hufanya baadhi ya mambo halafu wanaishia njiani kutokana na sababu mbalimbali. 

Ukweli ni kwamba mbali na watu hawa kuthubutu kuchukua hatua maishani mwao, matokeo yake wamejikuta wakishindwa kuzifikia hatima zao nzuri! 

Unatakiwa kujua kwamba baadhi yao wameishia njiani siyo kwamba wanatakiwa kuishia njiani, bali ni kwa sababu nyuma ya pazia kuna sababu ambazo zimesabababisha washindwe kukamilisha safari zao walizozianzisha! 

Na endapo itatokea hivyo watu hawa hujikuta wakishindwa kufanikiwa maishani mwao, kwa hivi badala ya kwenda mbele hujikuta wakirudi nyuma.

Mara nyingi hushindwa kuzifikia hatima zao kwa sababu ya kukosa hamasa, shauku, nguvu na kiu ya kufika huko.

Ukweli ni kwamba, hali hii husababishwa na watu hao kutokuweka kwa uwazi kile wanachokitaka kukikamilisha katika maisha yao. 

Huenda hata wewe ni miongoni mwa wale watu ambao wamekuwa wakianzisha vitu vipya na kutokuvikamilisha, na pangine labda umeteseka kwa muda mrefu sana na tabia hii, hali ambayo imesababisha ushindwe kupiga hatua kimaisha.

Habari njema ni kwamba, majibu ya tatizo lako yapo kwenye Makala hii, mara baada ya kusoma Makala hii kwa umakini ni imani yangu kwamba, utaifikia ile hadhi ya kuwa mtu usiyeweza kusimamishwa na chochote kile. 

Hivyo basi ili uweze kupata shauku, hamasa na nguvu za kufanikiwa katika mambo yako huna kutumia mbinu zifuatazo:-

1. Jitambue Wewe Ni Nani
Hauwezi ukapata shauku ya kufanya jambo fulani hadi kukamilika kwake pasipo kusimamishwa ilihali hujitambui wewe ni nani, na ifahamike kwamba, kama hutajitambua wewe ni nani hutaweza kujua ya kuwa unatakiwa uwajibike kama nani! 

Hata mimi mwenyewe ninapata ujasiri wa kusema ya kwamba, nilifanikiwa kubadili maisha yangu siku nilipojitambua kuwa mimi ni nani. 

Tokea hapo sikuweza kuruhusu kitu kitokacho nje kinisimamishe wala kibadili Kusudi langu.

Rafiki unatakiwa kujua kwamba, ninapozungumzia kujitambua namaanisha ile hali ya mtu kutambua utu wake na thamani yake. 

Nilipogundua ya kuwa mimi ni wa thamani na ninatakiwa niliishi kusudi langu ndipo sasa nikawa ni mtu mwingine kabisa ambaye sikuwahi kuwa.

Unapojitambua wewe ni nani inamaanisha kwamba, unagundua kusudi la kuumbwa kwako.

Unapogundua kusudi lako unapata uelekeo kamili juu ya kule utakapolifikisha katika kuliishi kwake.

Unapogundua kule unakokwenda maana yake utapata njia sahihi itakayokupeleka huko, kwa hivi hutaongozwa na kila njia bali utachagua njia itakayokupeleka kule iliko hatima ya kusudi lako.

Na ifahamike kwamba njia inayokupeleka kwenye ukuu huwa haionwi na wengi. Kwa hiyo haijalishi wengine watasemaje hautaweza kusimama kwa sababu tayari unajitambua wewe ni nani na unajua kule unakokwenda. 

Kwa upande wangu sikuruhusu maoni ya watu wengine yanisimamishe.

Nakumbuka kitabu changu cha kwanza kukiandika kinachoitwa; “Toleo Jipya La Maisha Yako; Ishi Upya.” Nilikiandika kwa kutumia simu kwa kuwa sikuwa na kompyuta. 

Nilipata shauku ya kufanya hivi pasipo kuweka kisingizio, kwa sababu nilijitambua mimi ni nani, na kusudi langu ni lipi!

Hivyo basi hata wewe ili uwe mtu asiyesimamishwa huna budi ujitambue kwanza kwa kugundua thamani yako pamoja na kusudi la kuwepo kwa maisha yako hapa duniani. 

Kwa sababu endapo utajua thamani yako hutaweza kuruhusu mambo yasiyo na thamani yakusimamishe bali utaendelea kupambana ili kuliishi kusudi lako pamoja na kuendelea kupandisha hadhi thamani ya maisha yako.

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri...

Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0773284329 Au tembelea blog yangu kwa kingmentorshipprogramblogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...