Jinsi Ya Kuwa Mtu Usiyesimamishwa Na Chochote Kile..
Mbinu Ya Tano Jifunze Kuamua Vyema...
Umefika hapo ulipo, umekuwa hivyo ulivyo, unatengeneza hicho kipato unachotengeneza, unafanya hiyo kazi unayoifanya, unaishi hapo unapoishi, unaishi maisha ya hadhi hiyo unayoishi, umekuwa na mwenzi huyo uliyonaye na kila kila unachokifanya katika maisha yako unakifanya kwa sababu umeamua kukifanya.
Ukweli ni kwamba, huwa unafanya maamuzi ukiwa huru, lakini mara baada ya kuamua unageuka na kuwa mfungwa na mtumwa wa maamuzi yako.
Kwa hivi huna budi kufanya maamuzi ambayo hayatakufanya usimame bali fanya yale maamuzi ambayo yatakufanya uwe mtu wa kusonga mbele tu.
Unatakiwa ufanye maamuzi ambayo kesho yako itakuja kukushukuru kwa kile ulichokiamua jana.
Unapokuwa ni mtu wa kufanya maamuzi sahihi maana yake utakuwa ni yule ambaye huwezi ukasimamishwa kwa sababu ya usahihi wa maamuzi yako kunyoosha mapito yako.
Kwa mfano mara baada ya kuamini kuwa ninaweza kuwa yoyote yule na nikachagua yule ninayetaka niwe.
Niliamua kutokuingia kwenye mahusiano mpaka pale nitakakapokamilisha ndoto zangu. Nilitambua kwamba mahusiano yanaweza kusimamisha harakati zangu ndiyo maana niliamua hivyo.
Amua leo hii kuwa mtu mkuu, amua leo hii kuwa mtu bora, amua leo hii kufanikiwa kimaisha, amua leo hii kufanikiwa kifedha, amua leo hii kuijenga kesho nzuri.
Unatakiwa kujua kwamba unapoamua vyema ndivyo unavyopata vyema. Hivyo ndivyo unavyopaswa kujua na ndivyo unavyopaswa kufanya.
Kumbuka kuwa kila kitu kinachotokea maishani mwako ni kwa sababu ya maamuzi yako, au kuna mtu mwingine aliakuamlia nawe hukuwa na chaguo.
Maadamu umejua kuwa una nguvu ya kuamua, huna budi kuamua vema ili uwe ni yule mtu asiyesimamishwa.
Kumbuka kuamua ni sawa na kujifunga gerezani. Usifanye maamuzi yatakayokufunga na kusababisha usimamishe harakati zako.
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri...
Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0773284329 Au tembelea blog yangu kwa kingmentorshipprogram.blogspot.com
Comments
Post a Comment