jinsi Ya Kuwa Mtu Usiyesimamishwa Na Chochote Kile

Mbinu Ya Sita Yapuuzie Maoni Hasi...

Kila mahali ulipo fahamu kwamba, umezungukwa vyanzo mbalimbali vinavyotoa maoni na mapendekezo kuhusu maisha yako. 

Kwa hiyo basi endapo maoni hayo yatakuwa ni maoni hasi utajikuta ukisimamishwa na kushindwa kukamilisha harakati zako. 

Kwa kusema hivyo kama unataka kuwa aina ya yule mtu ambaye hawezi kusimamishwa huna budi kupuuzia mapendekezo hasi.

Unatakiwa kujua kwamba maoni hasi yapo kila mahali kuanzia: nyumbani, ofisini, shuleni, mtaani, makanisani pamoja na misikitini. 

Hata hivyo, ikiwa hautakuwa na uwezo wa kuyakataa na kuyapuuzia, utajikuta ukisimamishwa hali itakayosababisha anguko lako. 

Ili kuepuka kusimamishwa, ni muhimu kujifunza jinsi ya kuyakataa mapendekezo hasi na kuunda mtazamo chanya wa maisha. Hii itakusaidia kuongeza kiwango chako cha bidii na juhudi katika mambo yako!  

Mbali na hilo endapo utachunguza kwa undani, utagundua kwamba watu wa karibu ambao tunawaamini ndio wamekuwa wakituambia mapendekezo haya. 

Hawa ni pamoja na wazazi, marafiki, ndugu, walimu, na viongozi wa dini. 

Mara nyingi, tunapopokea mapendekezo kutoka kwa watu hawa, tunachukulia kuwa ni ukweli bila kuangalia uhalisia wa maoni yao. Matokeo yake, tunajikuta tukisimamishwa na kelele zao na kutokuwa washindi! 

Na ifahamike kwamba, mapendekezo hasi yapo ili kukufanya utende kama wanavyotaka wao na siyo kama unavyotaka wewe...

Ndugu ili uwe yule mtu usiyeweza kusimamishwa huna budi kuyapuuzia mapendekezo hasi kama yafuatayo; 

Huwezi! Utashindwa Tu! Hutapata Nafasi! Wewe Ni Mkosaji! Mapenzi ni kwa ndege tu! Hakuna anayejali kuhusu wewe! Hutafanikiwa, na mengineyo, yanachangia sana katika kusimamisha harakati zetu tuzifanyazo kila siku! 

Siku moja nilipokuwa mtoto mdogo miongoni mwa watu walionizunguka alisema kwamba; “Tutakuja tuone maisha yako kama yatakuwa mazuri.” 

Na alisema hivyo akilenga kwamba maisha yangu yataishia kuwa ya kimaskini! 

Ukweli ni kwamba nilipuuzia maneno yale na mpaka sasa ninaishi maisha yangu na sifikirii kwamba kuna umaskini na kwamba mimi nitakuwa maskini.

Habari mbaya ni kwamba maoni haya hasi yanaweza kumfanya mtu ajione hana thamani au uwezo wa kufanikiwa, na hivyo kupunguza motisha yake. 

Kwa kutumia mapendekezo haya, mtu anaweza kujiona katika mwanga wa udhaifu badala ya kutambua uwezo wake halisi. 

Kwa hivi akajikuta anasimamishwa. Maadamu unataka kuwa yule mtu asiyesimamishwa huna budi kuyaapuzia mapendekezo hasi yote!

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri...

Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0773284329 Au tembelea blog yangu kwa kingmentorshipprogram.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...