Jinsi Ya Kuwa Mtu Usiyesimamishwa Na Chochote Kile...
Mbinu Ya Tatu Jiboreshe Kila Leo
Kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika zimeonesha kuwa, karibu kila ujuzi huweza kupitwa na wakati kila baada ya miaka miwili na nusu hadi miaka mitatu.
Kwa hivi kujua kitu Fulani siyo kigezo cha kufanikiwa kimaisha, bali kuendelea kujiboresha ndiyo mbinu itakayokusaidia uwe mtu usiyesimamishwa katika kufanya kitu Hicho.
Kwa sababu hata kama mabadiliko yatatokea wewe pia utabadilika kuendena na mabadiliko hayo, na hakuna kitu ambacho hubadilika haraka kama mabadiliko yenyewe.
Rafiki unapojiboresha kila leo inamaanisha kwamba, utakuwa unapata mbinu mpya za kufanya mambo yako. Kwa hiyo basi utakuwa mtu muafaka muda wote!
Kwa mfano sikuweza kujua kwamba kuna kitu kinaitwa online coaching, lakini mara baada ya kujifunza nimeweza kutoa huduma hii na mpaka sasa huwa nasimamia watu waliopo nje na eneo nililopo!
Na kuna baadhi ya wanafunzi wangu ambao huwa tunamaliza nao huduma nzima ya coaching bila kuonana kabisa!
Nakumbuka maneno ya mtaalamu mmoja hivi yaliyosema; “Ukilishalijua jambo jua limepitwa na wakati jifunze mbinu mpaya za kufanya jambo hilo.”
Ndivyo unavyopaswa kujua. Unatakiwa ujiboreshe kila leo, sunajua hata wamiliki wa magari huwa wanapeleka magari yao gereji kwa ajili ya kukarabatiwa?
Ndivyo unavyopaswa kufanya hata wewe, kwa maana hiyo huna budi kuikarabati akili yako kwa kuitafutia maarifa mapya kila leo!
Ukweli ni kwamba miongoni mwa njia nzuri itakayokusaidia utengeneze matokeo yanayodumu ni kutokuacha kujiboresha.
Hutakiwi kuacha kujiboresha kwa sababu pindi tu unapoacha kujiboresha ndipo unapopitwa na wakati. Matokeo yake utajikuta ukishindwa kufanya jambo lako kwa sababu umeshapitwa na wakati!
Na ndiyo maana ukiona unashindwa kufanya jambo Fulani maana yake kuna ujuzi umepungukiwa.
Kwa hiyo basi ili uwe na mwendelezo mzuri nawe uepuke kutokusimamishwa huna budi kujiboresha kwa kujifunza ujuzi mpya ili upate mbinu mpya za kufanya jambo hilo.
Unatakiwa kujua kwamba unapojiboresha maana yake unapata mbinu mpya za kufanya mambo, unapopata mbinu mpya za kufanya mambo ndipo na ujasiri wa kufanya mambo hayo unapoongezeka.
Kadri unavyozidi kuwa jasiri ndivyo unavyokuwa yule mtu ambaye huwezi ukasimamishwa.
Na ndiyo maana awali nilisema kwamba, kadri unavyokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu jambo Fulani ndivyo na hofu ya kufanya jambo hilo inavyopungua.
Kwa hivi kama unataka uwe ni mtu yule ambaye huwezi ukasimamishwa huna budi kujiboresha kila leo kwa kutafuta maarifa mbalimbali.
Na hivyo ndivyo ambavyo kujiboresha huwasaidia watu na kuwafanya wawe ni wale watu wasiosimamishwa na kila kitu, kwa sababu wanajua mbinu za kutumia ili kufanya mambo yatokee. Hata wewe huna budi kujiboresha.
Jiboreshe kiroho, kiakili, kimwili pamoja na kijamii nikimaanisha namna ya kujenga uhusiano na watu wengine!
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri...
Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0773284329 Au tembelea blog yangu kwa kingmentorshipprogram.blogspot.com
Comments
Post a Comment