Je, Kazi Yangu Ndiyo Kusudi Langu? Kama Jibu Ni Hapana, Je, Kazi Yangu Ni Nini?...

Hivi unafahamu kuwa watu wengi wanafanya kazi ambazo zipo nje na kusudi la kuumbwa kwao? 

Ukweli ni kwamba, upo uwezekano mkubwa sana wa kazi yako kutokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na Kusudi lako! 

Na endapo ikatokea kazi yako ikawa ipo nje na kusudi lako, hilo halitakuwa kusudi la kuumbwa kwako, bali ni utakuwa ni mfumo uliotengenezewa ili ukusaidie kutengeneza kipato kwa mateso na msumbufu mengi hapa duniani!

Upate kujua kwamba, Kazi ni shughuli yoyote ile iliyo halali aifanyayo mtu ili kujitengenezea kipato.

Hata hivyo wafanyakazi wengi huwa ni wabobevu na wana uelewa mpana kuhusu shuguli hizo.

Aidha, wengi wao huwa wameajiriwa na huwa na vyeti vya kitaaluma. Na elimu ndiyo hutumika kama kibali cha kuwaidhinisha kuwa wanastahili kufanya kazi hizo.

Mbali na hilo hata kiwango cha mshahara hutegemeana na kiwango cha elimu alichonacho mtu huyo!

Kwa mfano, mtu ambaye hajasoma huweza kufanya kazi za kutumia Nguvu (vibarua) na malipo yake huwa ni kidogo...

Ukilinganisha na mtu ambaye amesoma aliyeajiriwa ambaye hulipwa kiasi kikubwa cha pesa kumzidi kibarua, ijapokuwa hata yeye huyonyonywa kwa sababu kile anacholipwa hakiendani na thamani yake!

Tofauti na kusudi ambalo huwa ni lile jambo ambalo mtu anatakiwa aliishi kama jukumu kuu la kuumbwa kwake, kwa sababu ndilo lililosababisha maisha yake yawepo hapa duniani!

Mara nyingi jambo hilo siyo lazima awe amelisomea kama ilivyo kwa kazi! 

Ukiachilia hilo, kusudi huwa siyo jambo ambalo ukilifanya lazima utengeneze kipato, bali ni jambo ambalo unatakiwa uliishi ili kutimiza ule mpango wa kuumbwa kwako, maadamu utaliishi maisha yako yatafanyika na kuwa Baraka kwa watu wengine! 

Lakini ni mara chache sana ukakuta mtu analiishi kusudi lake na asilipwe, labda awe ameamua mwenyewe kutokudai maslahi kutokana na ufwanyaji wa jambo hilo! 

Lakini kwa vile kusudi ni jambo linalotoa thamani, na kwa vile watu hutumia fedha zao ili kubadilishana na vile vitu wanavyovithamini, inamaanisha kwamba watakuwa tayari kukulipa ili wabadilishane na ile thamani unayoitoa!

Ukiachiilia mbali hilo, endapo utafanikiwa kuliishi kusudi lako unaweza ukaligeuza na kulifanya liwe kama kazi.

Kwa mfano katika kuishi kwangu nilijikuta tu nikipenda sana kuwa mwandishi nitakayeielimisha jamii hii. 

Na hili jambo limekuwa ndani ya nafsi yangu tokea nilipokuwa mdogo. Nakumbuka kwa wakati huo nilikuwa kidato cha pili huko. 

Nilikuwa nikiandika mada mbalimbali zinazoelimisha jamii kwenye makaratasi.

Kwa hiyo mara baada ya kukua nimekuja kugundua kumbe uelimishaji kupitia uandishi huenda ndiyo sababu iliyosababisha maisha yangu yawepo, kwa sababu ni kitu nilichokuwa nasukumwa kukifanya, na ni kitu ambacho ninafurahia kukifanya na ninakifanya kila leo! 

Na nimeweza kuligeuza kusudi langu na kuwa kama kazi kwa kujiita muelimisha jamii, na kupitia kufanya hivyo ninatengeneza kipato huku nikitimiza furaha yangu pamoja na kurahisisha maisha ya watu wengine!

Na, nimegundua kwamba kuliishi kusudi kuna manufaa zaidi kwa sababu:-

1. Kipato chako hakikadiriwi na mtu!
2. Unaweza ukaamua kuongeza kipato chako muda wowote ule!
3. Unaweza ukalipwa hata usipofanya kazi itategemeana na mfumo uliouandaa!
4. Inaakisi uhalisia wa thamani yako na uwezo wako!
5. Unaepuka utumwa, mateso na manyanyaso ambayo watu hupitia kazini!

Je, wewe unaelewa nini kuhusu Kusudi?
 Je, unaelewa nini kuhusu Kazi?

Je, kipi ni bora, kati ya kufanya kazi iliyo nje na kusudi lako au kugeuza kusudi lako liwe kama kazi?

Naomba nipokee mrejesho Kutoka Kwako na kwa namna gani makala hii imekubadilisha kimtizamo!

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!

Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwalimu, Mwandishi Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329/0773284329 Au tembelea blog yangu kwa kuandika kingmentorshipprogram.blogspot com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...