Je, Unataka 2025 Uwekeze Katika Afya Yako? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii..
Niliposoma KITABU cha "The Diary Of A CEO, The 33 Laws Of Business And Life"
Katika kanuni ya tisa amesema; "Always prioritise your first foundation "
Akimaanisha kwamba, huna budi kuweka kipaumbele kwenye afya yako kwa sababu huo ndiyo msingi wa maisha yako...
Na unatakiwa ujenge afya yako ili uishi muda mrefu huku ukifurahia maisha.
Mwandishi huyu amenukuu maneno ya Warren Buffett tajiri mkubwa sana hapa duniani katika nyakati hizi ambaye alisema;
"Nilipokuwa na umri wa miaka 16 vipaumbele vyangu vilikuwa ni wanawake na magari. Sikuwa na bahati kwa wanawake lakini nilikuwa na bahati kwa magari"
Huyu mwamba anadai kwamba, alitumia 80% ya maisha yake kwenye kazi, wanawake, marafiki, familia na katika kumiliki mali nyingine nyingi."
Lakini alipofikisha miaka 27 mambo yalibadilika kutokana na janga la COVID-19 lililoua zaidi ya watu milioni sita.
Baada ya ripoti iliyohusisha wagonjwa 400,000 kuonesha kwamba asilimia 113 ya watu wenye vitambi walifariki sana pamoja na wale waliokuwa na afya mgogoro...
Hapo ndipo alitambua kuwa afya ndiyo kila kitu, na huo ndiyo ukawa mwanzo wake wa kuanza kutunza afya...
Mwamba anadai kwamba, kupoteza mali, wanawake, fedha, marafiki na vitu vingine si kitu ukilinganisha na kupoteza afya...
Kwa Sababu ukipoteza afya umepoteza maisha, na ndiyo maana kujali afya ndicho kinatakiwa kiwe kipaumbele chako...
Rafiki unatakiwa kujua kwamba, unaweza ukapoteza Mali, fedha, wanawake na vitu vingine, lakini endapo utakuwa na afya njema utavirudisha hivyo vyote...
Si hivyo tu, pia kwa mujibu wa Mr Olumide Emmanuel katika kitabu chake kinachoitwa; "The school of money"
Alipokuwa akidokeza aina za mitaji ya biashara, alitaja afya kama moja ya mtaji muhimu sana unaotakiwa kuwa nao...
Akasema kwamba, kuwa na fedha bila kuwa na afya si kitu na kuna watu ambao wana fedha lakini hawana afya...
Watu hawa hukosa cha kufanya na fedha zao...
Naam, natambua kuwa upo bize kazini, natambua unapambana sana...
Katika kupambana kwako usisahau afya yako...
Usicheze na afya yako kwa sababu hauna maisha mawili...
Kwa kila unachokifanya jaribu kuvuta matokeo yake baada ya miaka kumi itakuwaje...
Rafiki, chakula ni dawa endapo kitatumika kwa utaratibu upasao, lakini pia, chakula ni sumu endapo utavunja kanuni za ulaji...
Na usipotumia chakula kama dawa, siku moja utatumia dawa kama chakula...
Siku hizi kuna magonjwa mengi sana tunaumwa kwa sababu kuna kanuni za ulaji tunakiuka...
Miili yetu inakuwa inahitaji baadhi ya virutubisho lakini kwenye vyakula tunavyokula vinakosekana...
Matokeo yake mtu anaumwa, anaenda hospitalini, huko anaenda kutibiwa ili kupunguza maumivu siyo kupambana na upungufu wa baadhi ya virutubisho mwilini mwake!
Swali linakuja, je, huyu mtu anakuwa amesaidika na tiba aliyoipata?
Au katuliza homa lakini tatizo lake limebaki pale pale?
Umeona madhara ya kulikabili tatizo bila kuangalia chanzo cha tatizo?
Sijui nataka kusemaje, lakini unatakiwa kujua kwamba, kuwa na afya njema ni haki yako ya kuzaliwa endapo utazingatia kanuni za ulaji...
Hata hivyo mwandishi Joseph Murphy katika kitabu chake kinachoitwa "the power of your subconscious mind" alitoa kanuni ya afya inayosema;
"Kila palipo na maisha pana ukuaji na kila palipo na ukuaji pana afya njema "
Kwa hiyo basi, kama unaishi huna budi kutunza afya yako ili uishi zaidi.
Wito wangu kwako hakikisha unakula vyakula vyenye virutubisho, usile kujaza tumbo, bali ule ili ujenge afya...
Fanya mazoezi, haijalishi una mwili mkubwa au mdogo, fanya ili kujenga mwili wako...
Tafuta maarifa kila leo, hakikisha unamiliki taarifa sahihi kuhusu afya na ulaji...
Usisubiri mpaka uumwe ili uchukue hatua, chukua hatua sasa, kumbuka kinga ni bora kuliko tiba!
Kwa ushauri, zaidi karibu inbox!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, na Afya, Life Coach And Consultant!
Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329/0773284329 Au tembelea blog yangu kwa kuandika kingmentorshipprogram.blogspot.com
Comments
Post a Comment