Je, Unataka Kujua Kusudi Huwa Na Sifa Gani? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...

3. Kusudi Ni Jambo Ambalo Huwa Na Manufaa Kwako Na Kwa Wengine...

Mungu kaumba kila kitu kwa sababu kuna kusudi la kuwepo kwake. Hata jua, mwezi na nyota vipo kwa sababu nyuma yake kuna sababu za kuwepo kwake. 

Kwa mfano mbali na kuwa jua huwa chanzo kikuu cha nuru, lakini inasadikika kwamba, endapo itatokea jua likawa halipo, dunia yote itaganda na kuwa barafu!

Hiyo miti, ardhi, maji na viumbe vyote alivyovifanya Mungu kwa jinsi yake vipo kwa sababu nyuma yake kuna sababu zinavyovifanya viwepo! 

Hata kama huwa unavipuuza, haimaanishi kwamba umuhimu wake haupo kwa sababu kutokujua umuhimu wa kitu Fulani haiondoi umuhimu wake. 

Kwa mfano miti husaidia kupunguza kiwango cha gesi za ukaa ambazo huharibu safu ya ozoni inayofanya kazi ya kuilinda dunia dhidi ya mionzi ya moja kwa moja itokayo kwenye jua.

Kwa kusema hivyo hata maisha yako yamebeba kusudi Fulani hivi ambalo linayafanya yawe na manufaa kwako na kwa wengine. 

Yaani kama vile ambavyo jua lina manufaa kwetu ndivyo na kusudi lako linavyotakiwa liwe na manufaa kwa wengine. 

Kwa kusema hivyo kupitia kuliishi kusudi lako, unatakiwa ufanye jambo ambalo linawanufaisha watu wengine. 

Na ukiona kwenye maisha yako haufanyi jambo ambalo linawagusa watu wengine kwa namna chanya inamaanisha kwamba bado hujaanza kuliishi kusudi lako. 

Ukiona haufanyi jambo ambalo linaboresha maisha ya watu wengine maana yake bado hujaanza kuishi maisha yako halisi.

Kwa mfano ninapoliishi kusudi langu kwa kutoa ujinga kwenye fahamu za mtu Fulani na kumletea nuru kwa minajili ya kumfanya ajitambue ya kuwa yeye ni nani na anaweza akafanya nini, inamaanisha kwamba nakuwa nimemsaidia aweze kuona upande wa pili wa sarafu wa maisha yake!   

Kwa kusema hivyo mtu huyo ataweza kugundua thamani ya maisha yake pamoja na umuhimu wake, kwa kupitia kusudi la mtu Fulani atakayemuonesha. 

Swali linakuja vipi kama huyo mtu aliyemuonesha asingefanya hivyo, je, angeweza kugundua umuhimu wa maisha yake pamoja na thamani yake? Ndivyo unavyopaswa kujiuliza! 

Ukweli ni kwamba Mungu alimpa kila mtu kusudi Fulani ili akiliishi liwanufaishe watu wengine. 

Kwa kusema hivyo ulimwengu huu umekamilishwa kutokana na uwepo wa kusudi lililobebwa na kila mtu. Huyu atafanya hivi, na huyo atafanya hivyo kwa kadri ya kusudi lake.

Kwa mfano mwandishi ataandika ili afichue ukweli, msomaji atasoma atachukua hatua kutokana na kile kilichofichuliwa na mwandishi.

Inapotokea mwandishi kaandika kuhusu namna ya kuwa kiongozi bora, na kikamtengeneza msomaji huyo akawa bora maana yake ubora wa kiongozi huyo unakuwa umetokana na kusudi la kuwepo kwa mwandishi aliyempa mfumo huo! 

Kumbe hata kusudi lako linategemea mfumo mwingine. Na mfumo ulio mkuu ambao ni chanzo cha yote ndiyo Mungu mwenyewe mwenye vyote. 

Kwa mfano sisi sote tuko hai kwa sababu ni Mungu ndiye katufanya tuwe hivi. Kwa kusema hivyo tunatakiwa tufanye maisha yetu yawe na maana kwa kuhakikisha kuwa tunagusa maisha ya watu wengine. 

Kwa hiyo hakikisha kuwa kuna jambo fulani hivi ambalo unalifanya kwa mianjili ya kugusa maisha ya watu wengine. Ndivyo ambavyo Mungu katuumba sisi sote! 

Kwa mfano tangu nimeanza kuliishi kusudi langu nimeshuhudia watu wengi sana wakibadilika kimtizamo huku wengine wakitambua hazina zao, uwezo wao waliozaliwa nao na wengine wakiahidi ule mchango ambao wanaenda kuufanya kwa ajili ya watu wengine, na hii inachangiwa na watu hawa kugundua ya kwamba huwa tunaishi kwa ajili ya watu wengine. 

Hata hivyo ninachelea kusema kwamba, kusudi ni jambo ambalo huwa lina manufaa kwa sababu endapo utaliishi utaweza kujitengenezea kipato. 

Mimi mwenyewe ni miongoni mwa wale watu ambao wanalipwa kupitia kuliishi kusudi lao, hata makala hii ambayo unaisoma imeweza kunivutia wateja inbox!

Na haya ndiyo manufaa yanayopatikana kutokana na kusudi la kuumbwa kwako.

Na ndiyo maana nimesema kwamba kusudi lako ni jambo ambalo limebeba thamani yako, limebeba jina lako, limebeba ukuu wako, na limebeba mafanikio yako kwa ujumla! 

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwalimu, Mwandishi Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329/0773284329 Au tembelea blog yangu kwa kuandika kingmentorshipprogram.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...