Je, Unataka Kujua Sifa Pambanuzi Za Kusudi? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...

2. Kusudi Ni Jambo Linaloendana Na Wewe Ulivyo

Upo hivyo ulivyo kwa sababu upo hivyo. Na upo hivyo ulivyo ili uweze kuliishi kusudi lako!

Umeumbwa na rangi hiyo uliyonayo kwa sababu kuna kusudi la uwepo wa rangi hiyo maishani mwako. 

Umeumbwa na huo mwili ulionao kwa sababu kuna kusudi la wewe kuumbwa hivyo.

Katika hali ya kawaida hata mionekano ya vitu alivyovitengeneza mwanadamu hupima kusudi la vitu hivyo. 

Kwa mfano vile gari la kuchukua mchanga lilivyo ni tofauti kabisa na vile gari la kuchukua abiria lilivyo kimuonekano. Vile ndege ilivyo ni tofauti kabisa na meli ilivyo.

Kwa kusema hivyo, ndege imetengenezwa kwa kusudi la kuweza kupaa, ilihali meli imetengenezwa ikiwa na uwezo wa kuelea juu ya maji. 

Na aliyetengeza ndege, aliiunda kwa kulinganisha na vile ndege asilia walivyo. Huku hata aliyejenga meli alijenga sawa na na vile samaki walivyo kwa sababu wana uwezo wa kuelea juu ya maji.

Kwa hivyo hata wewe upo hivyo ulivyo, ukiwa na mwili huo ulionao, ukiwa na hilo umbile ulinalo, ukiwa na hiyo rangi uliyonayo kama nyenzo za kukusaidia kuliishi kusudi lako. 

Na usijaribu hata kubadilisha muonekano wako ukawa tofauti na vile Mungu alivyokuumba kwa sababu utakuwa unajitoa kwenye mfumo wa kuliishi kusudi lako.

Kwa mfano kwa upande wangu nimeumbwa na mwili mwepesi ili niweze kufanya kazi ya uandishi kwa urahisi zaidi, ninaweza hata nikaa masaa nane bila kuchoka huku nikiendelea na kazi zangu. 

Hata wanamichezo mbalimbali ukiwaangalia utagundua kwamba miili yao ni myepesi ili iwasaidie katika kufanya ile kile wanachokifanya, na ndiyo maana siyo rahisi ukamkuta mtu mwenye mwili mkubwa kama tembo, akishiriki kwenye mashindano ya mbio za kukimbia, ijapokuwa inaweza kutokea.

Hata Yesu Kristo alikuwa na umbile la kawaida sana ambalo lilimfanya aliishi kusudi lake. Ukija kusoma Kitabu cha nabii Isaya utaona uhalisia wa umbile la yesu lilivyokuwa. 

Isaya 53:2-3 “… Yeye hana umbo wala uzuri; na tumwonapo hana hata uzuri tumtamani. Alidharauliwa na kukataliwa na watu…”

Najua kuna picha Fulani hivi BANDIA ya Yesu inakujia akilini mwako, na picha hiyo inamuonesha mwanaume mmoja hivi mwenye sura nzuri na umbo zuri, ndugu hiyo siyo picha halisi ya Yesu.

Ukweli ni kwamba Yesu hakuwa na umbo zuri, alikuwa ni kama kituko hivi. Hebu jaribu kuvuta picha mtu mzima halafu anapanda mwanapunda, ilihali hata wewe mwenyewe ukimpanda mwanapunda atavunjika. 

Na hii ndiyo sababu kubwa ambayo iliwafanya watu wamdharau sana Yesu. Wakamwambia ana pepo, mara hajasoma, mara anajishuhudia mwenyewe na dhihaka nyingine nyingi. 

Lakini mbali na kufanyiwa hayo yote aliweza kuyatimiza mapenzi ya yeye aliyempeleka. Yohana 19:30 

Kwanini watu walikuwa wakimdharau sana? Ni kwa sababu vile walivyokuwa wakimuona walikuwa wanaona hafananii na vile anavyofanya, anavyotenda na kuvisema. 

Na ifahamike kwamba walikuwa wakimuona kama kituko hivi. Na Mungu alimruhusu Yesu awe na umbile hilo ili adhirihirishe uwezo wake wa ajabu.

Wewe pia haijalishi upoje, unatakiwa kujua kwamba upo hivyo ulivyo kwa sababu kuna kusudi umelibeba linalolandana na hivyo ulivyo. 

Haijalishi watu wanakuonaje, haijalishi wewe mwenyewe unajionaje, lakini unachopaswa kujua ni kwamba upo hivyo ulivyo kwa sababu upo hivyo, na unatakiwa uliishi kusudi lako kutokana na wewe ulivyo. 

Je, kutokana na hivyo hivyo ulivyo unahisi unastahili kufanya jambo gani kiurahisi zaidi?

Ndugu unatakiwa kujua kwamba hapa duniani, hakuna kinyonge kwa sababu hata Mungu huweza kutumia vitu vinyonge ili aweze kudhihirisha ukuu wake na uweza wake wa ajabu!

1 Wakorintho 1:27-28 “Bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alichagua vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko.” 

Hivyo ulivyo umebeba ukuu, hivyo ulivyo una uwezo wa kubadilisha jamii hii iliyobatilika kwa kuliishi kusudi lako! 

Usijidharau wala usijipuuze, kumbuka hivyo ulivyo ndivyo ulivyopaswa uwe ili uliishi kusudi lako!

Mimi mwenzako tayari ninakifanya kile kilicho kwenye mapenzi yangu na ninajisikia kufanya kile kitu ninachopenda kukifanya!

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwalimu, Mwandishi Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329/0773284329 Au tembelea blog yangu kwa kuandika kingmentorshipprogram.blogspot com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...