Je, Unataka Ubadili Fikra Zako Ili Ubadili Maisha Yako? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii..

Hivi unafahamu kwamba maisha yako yamekuwa hivyo yalivyo na yamefika hapo yalipo kutokana na fikra zako mwenyewe? 

Unatakiwa kujua kwamba katika maisha huwezi ukakivuta kitu ambacho hujakitengeza kupitia fikra zako!

Ukweli ni kwamba hata hatima za maisha yetu huanza kama fikra, ya kwamba, unapanda wazo/dhana unavuna kitendo, unapanda kitendo unavuna tabia, unapanda tabia unavuna utambulisho, unapanda utambulisho unavuna hatima ya maisha yako!

Ndugu, hivyo ndiyo mduara wa maisha yako ulivyo, kwa kusema hivyo maisha yako yamekuwa hivyo kwa sababu, yalianza kutokana na dhana/mawazo uliyoyatengeza kupitia fikra zako mwenyewe...

Kutokana na ukweli huo, ndiyo maana ilishawahi kusemwa Kwamba, maisha ya binadamu ni matokeo ya fikra zake mwenyewe!

Hii inamaanisha kwamba, umefika hapo ulipo kimaisha na umekuwa hivyo ulivyo kutokana na fikra zako mwenyewe!

Na utakuwa huyu ama yule kesho yako endapo utaamua kubadilisha fikra zako!

Unatakiwa kujua kwamba fikra zako ni kama mbegu inayopandwa ili ilete matokeo mbalimbali katika maisha yako!

Na ndiyo maana kanuni ya kupanda na kuvuna inasema kwamba "utavuna ulichokipanda" 

Kinachomaanishwa hapa ni kwamba, aina ya fikra unazozitengeneza ni mbegu unazozipanda ubongoni mwako, na ukishazipanda lazima utavuna mavuno yanayolandana na fikra zilizowasilishwa!

Hata hivyo hakuna mbegu ambayo huzalisha tunda lisilo la asili yake.

Kwamba ukipanda mchele tegemea kuvuna mchele, usitegemee kuvuna maharage!

Sijui unapitia hali gani ila nipo hapa kukufahamisha kuwa, unapitia hayo yote kama mavuno ya aina ya fikra ulizozipanda ubongoni mwako!

Hata hivyo tafiti nyingi za kisaikolojia kuwahi kufanyika zimeonesha kwamba, watu wa kawaida huishia kutumia 3% tu ya ubongo wao!

Jaribu kufikiri mtu anapanda mbegu kwa asilimia ndogo kiasi hicho je atapataje mavuno Kwa asilimia 100%?

Yaani mbegu unayopanda kupitia fikra zako ni sawa na hakuna kitu, itakuwaje upate matokeo makubwa kimaisha ilihali ulichopanda ni sawa ni sawa na si kitu? Unatakiwa kufikiri tena juu ya suala hili...

Hata hivyo unatakiwa kujua kwamba fikra ni kama injini ambayo huchakata ili kuleta matokeo katika maisha yako, hii ni kwa sababu mawazo yakitengenezwa ndiyo husababisha mambo yatokee!

Kwa mantiki hiyo kile unachokifikiri ni sawa na unakiumba, kumbe sasa kwa kutumia fikra zako una mamlaka ya kuumba!

Habari njema ni kwamba, kitu pekee ambacho mwanadamu unaweza ukakitawala hapa duniani ni fikra zako tu, hii inamaanisha kwamba, unaweza ukachagua fikra zozote zile kuhusu jambo fulani lililopo mbele yako!

Kinacholeta faraja na tumaini kubwa ni kwamba, moja ya viumbe vilivyopendelewa na Muumba ni binadamu pekee yake, kwanini nasema alipendelewa? 

Ni kwa sababu binadamu kapewa ubongo umsaidie katika kufikiri na ili aweze kuvumbua vitu na kukabili changamoto zake!

Hii inamaanisha kwamba wewe kama mtu una wajibu wa kutumia fikra zako ili upate matokeo unayoyataka...

Kutokana na hilo unatakiwa kujua kwamba utakuwa kwa kadri ya vile uyakavyojifikiria!

Ndugu, unatakiwa kufahamu kwamba ili uweze kubadili maisha yako, ni lazima uanze kubadili fikra zako kwanza!

Na kama hutabadili fikra zako hutabadili matokeo katika maisha yako, kwa sababu ili upate matokeo ambayo hukuwahi kuyapata ni lazima ukubali kutengeneza fikra ambazo hukuwahi kuzitengeneza!

Wapo watu wengi sana ambao wamejikuta katika hali ya sintofahamu, hasa wakiangalia mienendo ya maisha yao pamoja na hali wanazopitia...

Yaani kadri siku zinavyozidi kwenda mbele, ndivyo na hali mbalimbali katika maisha yao, zinavyozidi kwenda hatua mbaya Zaidi, wasijue shida ni nini...

kumbe, shida ni wao wenyewe kupitia aina ya fikra wanazozitengeneza! 

Mbali na hilo ni kanuni ya ulimwengu mzima kwamba, "maji hutiririka kufuata mkondo" kwa hivi hata, maisha yako yatalandana na fikra zako! 

Kwa mantiki hiyo kila fikra ni kisababishi na hali yoyote ile unayopitia ndiyo ni matokeo yake.
Kwa mfano: umaskini, hali ngumu ya maisha, mikosi, kipato, uhusiano tete, kutokuthaminiwa na mengine kama hayo...

Ukiachilia mbali hilo kanuni ya uvutano inasema; "wewe ni kama sumaku inayoishi, unayeweza kuvuta watu, matukio, hali mbalimbali, mafanikio na kitu chochote kile ambacho kitapatana na fikra kuu zinazotawala maisha yako"

Kwa mujibu wa kanuni hii ni kwamba siyo kila kitu unaweza ukakivuta, bali utakivuta kile kinacholandana na ile fikra kuu inayotawala maisha yako!

Je ni kipi kinatawala fikra zako Kwa asilimia kubwa? 

Unatakiwa kujua kwamba utavuta vitu vitakavyopatana na fikra zinazotawala mfumo wa maisha yako!

Mambo ya msingi unayopaswa kuyajua kuhusu uhusiano wa Fikra zako pamoja na kanuni ya uvutano:

๐Ÿ”น Fikra za uhaba huvuta uhaba...
๐Ÿ”น Fikra za mafanikio huvuta mafanikio...
๐Ÿ”น Fikra za umaskini huvuta umaskini...
๐Ÿ”น Fikra za kushindwa huvuta kushindwa...
๐Ÿ”น Fikra za furaha huleta furaha...
๐Ÿ”น Fikra za matumaini huleta matumaini...
๐Ÿ”นFikra za kuweza huvuta uwezo...
๐Ÿ”น Fikra za huzuni huleta huzuni...
๐Ÿ”น Fikra hasi huvuta matukio hasi...
๐Ÿ”นFikra chanya huvuta matukio chanya..
๐Ÿ”น Fikra za utajiri huvuta utajiri...

"Yule anayefikiri anaweza ataweza, ikiwa yule anayefikiri hawezi hataweza" 

Kuweza au kutokuweza siyo kitu halisi, na hakuna ambaye aliumbwa hawezi au anaweza, bali sote tumezaliwa tunaweza ila aina ya fikra tunazotengeneza ndizo hututofautisha...

Je mpaka hapa ni aina gani ya fikra zinazotawala maisha yako?

Unatakiwa kujua kwamba, kile unachokifikiri ndicho unachokivuta...

Kwa mantiki hiyo huna budi kufahamu kwamba, hata hali zote unazopitia katika maisha yako umezivuta kutokana na fikra zako!

Je umechoka na hali unazopitia maishani mwako?

Kama jibu ni ndiyo basi huna budi kubadili fikra zako kwanza!

Yes boss, badili fikra zako badili maisha yako! Yaani (change your thinking change your life)

Kumbuka unachopata kwenye maisha ni uakisi wa kile unachotengeneza ubongoni mwako kupitia fikra!

Na ndiyo maana hata Neno la Mungu linasema; apple apple sauce I"maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo" kasome mithali 23:7

Kwamba vile unavyojiona (kupitia fikra zako), ndivyo unavyokuwa katika maisha yako halisi... 

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; mwalimu, mwandishi muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi, life coach and consultant!

Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329/0773284329 Au tembelea blog yangu kwa kuandika kingmentorshipprogram.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...