Je, Unataka Ufahamu Afya Hutengenezwaje? Kama jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...
Hivi unafahamu kwamba afya huanza kutengenezwa mara tu mimba inapotungwa?
Ijapokuwa, huwa unakuwa kimwili kutokana na kile unachokula, lakini afya yako ilianza kutengenezwa tokea siku mimba yako ilipotungwa...
Kwa maana Hiyo, mtindo wa maisha ya mama pamoja na mazingira yaliyopolekea ujauzito ndiyo hupima afya ya mtoto akiwa tumboni...
Kwa mfano Ni juzi tu hapo watu wamefanya miruko wakiwa wanaadhimisha brithday ya Yesu, wakashindwa kufanya yaliyo ya Kiyesu. Nasikia guest na Lodge zilijaa haha utani kidogo ila usicheke, ona sasa unacheka...
kwa hiyo basi kama kuna mwanamke hakujipanga akafanya miruko na mwanaume pasi maandalizi ya msingi ya kulea mimba kwa utaratibu unaotakiwa, halafu akaendelea na mtindo mbovu wa kuishi huku akiwa mjamzito, kuna uwezekano wa kuja kuzaa mtoto mwenye tatizo la kiafya...
Si hao waliofanya miruko tu, pia wapo hata wanandoa ambao hawana taarifa sahihi juu ya kipi kinatakiwa kifanyike pindi mama akiwa mjamzito...
Wengi hawajui mama anashauriwa ale vyakula vya aina gani, hawajui ni vyakula gani hatakiwi kula, hawajui ni aina gani ya vinywaji haruhusiwi kunywa na vitu vingine vingi huu ni kwa mfano tu...
Kwa hiyo basi kama utaratibu hautafuatwa kuna uwezekano wa kuzaa mtoto mwenye changamoto kiafya...
Ndugu unatakiwa kujua kwamba, baadhi ya magonjwa yanayowakumba watu wengi siku hizi yalitengenezwa kipindi cha ujauzito..
Kwa mantiki hiyo kipindi cha ujauzito ni muhimu kwa sababu ndicho kinaweka msingi wa ukuaji wa mtoto kimwili, kiakili, na kihisia.
Ngoja nikupeleke kwenye hatua zinazohusika katika mchakato unaojenga afya ya mtoto:-
◾ Trimester 1 Miezi (0-3)
Huu ni wakati ambapo viungo muhimu kama moyo, ubongo, figo, na mapafu vinaanza kuumbika.
Hata hivyo mfumo wa fahamu (nervous system) huanza kutengenezeka wiki ya tatu au ya nne.
Kwa kipindi hiki mama anashauriwa atumie vyakula vyenye virutubisho kama vile: folic acid, madini ya chuma, na kalsiamu ni muhimu sana katika kipindi hiki ili kusaidia ukuaji mzuri wa neva na kuzuia matatizo ya kimaumbile kama spina bifida.
Trimester 2 (Miezi 4-6)
Hiki kipindi ambacho viungo vya mtoto vinaendelea kukua na kuwa imara. Mtoto anaanza kusikia na hata kuhisi harakati zinazoendelea huko ulimwenguni...
Vyakula vinavyotakiwa vitumike na mama katika hatua hii ni: lishe bora yenye protini, matunda, mboga za majani, na maji ya kutosha.
Si hivyo tu pia uchunguzi wa mara kwa mara kwa daktari unahitajika ili kufuatilia maendeleo ya mtoto na afya ya mama.
Trimester 3 (Miezi 7-9)
Katika hatua hii mtoto anakuwa na uzito na mafuta zaidi ili kusaidia katika kudhibiti joto la mwili baada ya kuzaliwa.
Mama anahitaji kupumzika vya kutosha na kuepuka msongo wa mawazo, ukiona unataka kupata msongo wa mawazo nicheki, mimi ni comedian pia hahaha.
Mazoezi mepesi kama kutembea husaidia kuboresha mzunguko wa damu.
Angalizo: Afya ya mama ina athari kubwa kwa ukuaji na afya ya mtoto.
Hivyo Basi ili mama aweze kuwa na afya bora hana budi kuzingatia lishe bora kama ifuatavyo:
Mama anapaswa kula chakula chenye protini, vitamini, madini, na mafuta yenye afya.
Folic acid (kabla na wakati wa ujauzito) husaidia kuzuia kasoro za mishipa ya fahamu kwa mtoto.
Pia ili kuwa na afya njema mama hana budi kuepuka vitu hatari kama vile: Tumbaku, pombe, na dawa za kulevya huweza kusababisha matatizo makubwa kwa mtoto. Mama anapaswa kuepuka kemikali hatari na mionzi.
Hata hivyo kwa upande wa afya ya akili mama mjamzito hana budi kufahamu kwamba, msongo wa mawazo unaweza kuathiri mtoto.
Najaribu kuwaza mtu kapata mimba kwa bahati mbaya, halafu mwanaume kaikataa, amejaribu kuitoa halafu imegoma...
Sijui itakuwaje, kwa namna hii kweli msongo wa mawazo utaepukika?
Kwa wewe ambaye upo na mume wako, epuka Kabisa msongo wa mawazo, fanya maombi ya kutosha wachawi huwa wanavimendea sana vitoto vichanga, omba mpaka mbengo zifunguke...
Mbali na hilo mama mjamzito anashauriwa kufanya uchunguzi wa mara kwa mara (clinic visits) kwa minajili ya kufuatilia maendeleo ya mtoto na afya ya yake.
Pia Mama hana budi kutumia chanjo na vidonge vya kuongeza madini ya chuma husaidia kuimarisha afya.
Kwa hivyo, afya ya mtoto inaanza kuimarika mara tu mimba inapopatikana, na afya ya mama ina nafasi kubwa katika kuhakikisha mtoto anakua salama na mwenye afya njema.
Nimeamua kutoa elimu hii kwa sababu mtoto ni mtu mzima anayekua na mtu mzima ni mtoto aliyekua!
Hivyo badi ili tumpate kiumbe mwenye afya bora mama mjamzito hana budi kuzingatia kilichoandikwa hapa...
Kwa msaada zaidi karibu inbox! Pia Kama una mpango wa kushika ujauzito hivi karibuni karibu inbox kwa ushauri zaidi...
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi na afya, Life Coach And Consultant!
Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329/0773284329 Au tembelea blog yangu kwa kuandika kingmentorshipprogram.blogspot.com.
Comments
Post a Comment