Jinsi Maendeleo Ya Sayansi Na Teknolojia Yamesababisha Watu Wajione Vile Wanavyojiona...
Angalizo: sipingani na maendeleo ya sayansi na teknolojia wala sitaki mtu apuuze haya maendeleo kwani yamerahisisha maisha, lakini ninaibua hoja inayoonesha ni kwa namna gani maendeleo ya sayansi na teknolojia yameathiri watu kimtizamo yaani vile wanavyojiona na ifahamike kwamba kila chenye faida huwa hakikosi kuwa na hasara!
Tafadhali elewa nazungumzia ni kwa namna gani sayansi na teknolojia imesababisha watu wajione vile wanavyojiona!
Kwanini nasema sayansi na teknolojia imebadilisha watu kimtizamo? Sababu kubwa inayonisukuma niseme ni kwamba watu wengi wamejikuta wakitumia sayansi na teknolojia kama kioo cha kujitazamia!
Matokeo yake wameishi kujiona wao ni wabaya kimuonekano (hasa wakihusisha rangi zao pamoja na muonekano wa maumbile yao).
Kutokana na hilo wakaanza kujishushia hadhi kwa kujiona wao kama siyo kitu, pasi na kujua kwamba kioo walichotumia kujitizamia siyo kioo halisi!
Kwa mfano maendeleo ya sayansi na teknolojia yamekuja na ugunduzi wa baadhi ya viungo bandia vinavyopachikwa mwilini mwa mwanamke ili kumfanya aonekane na umbo murua, uzalishaji wa baadhi ya vidonge vinavyomsababishia huyo mwanamke awe na shepu zuri pamoja ugunduzi wa baadhi ya vidonge vinavyotumika kuchubua rangi, yaani kutoka nyeusi hadi rangi nyeupe.
Hii inamaanisha kwamba, kutokana na kasumba iliyoletwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia mwanamke mweusi, mwenye umbo la kawaida, ambaye ana rangi nyeusi anajiona yeye si kitu na hana thamani, mbele ya mwanamke mwenye rangi nyeupe, (inayotokana na kujichubua), mwenye umbile la kutengenezwa na mwenye mwonekano mzuri kutokana na matumizi ya vipodozi, asijue kwamba hakuna uhusiano wowote kati ya hao wanawake walivyo na yeye alivyo!
Wanawake hawa hujiona wao si kitu na hawawezi hata wakaolewa eti kwa sababu ya rangi zao, maumbile yao pamoja na muonekano wao kitu ambacho hakina ukweli wowote!
Na ndiyo maana wengi wao huhangaika wajichubue, wakafanyiwe upasuaji kwenye nyonga na kupandikizwa baadhi ya viungo bandia ili hata wao waonekane kuwa ni matawi ya juu!
Hata hivyo, kimtizamo, maendeleo ya sayansi na teknolojia yamewafanya watu wengi wajione kana kwamba waliumbwa waje watumikie ngono tu hapa duniani.
Kutokana na hilo baadhi ya watu wamejikuta wakijali zaidi mvuto unaolenga zaidi kwenye eneo la mapenzi wakasahau kuhusu kusudi la kuumbwa kwao, na hata umuhimu wa uwepo wa maisha yao hapa duniani pamoja na mchango wao katika kuibadilisha jamii hii!
Rafiki hauhitaji kutumia nguvu kubwa sana kubaini hili, hebu jaribu kuangalia jinsi wanawake wa leo wanavyohangaika kila leo kuchubua rangi zao kisa wapendeze mbele ya wanaume. Unafikiri wanawaza nini kama siyo kukumbwa na fikra za kingono?
Kuna wengine wanahangaika kumeza vidonge ili waongeze nyonga zao pamoja na makalio yao kisa tu wapendeze na wavutie machoni pa wanaume hii nayo ni fikra hatalishi ya ngono na wala si kingine.
Wapo wengine wanahangaika kuvaa nusu uchi huku wakiacha maungo yao wazi kisa tu wawavute wanaume hawa nao wanakumbwa na fikra za ngono, na si kitu kingine. Wasijue kwamba sisi kama wanaume siku hizi tunaenda kwa imani na siyo kwa kuona hahahaha💪😎!
Hata hivyo ni mwaka mmoja umepita tokea Mr Elon Musk agundue midoli ya kike kwa ajili ya kufanya nayo ngono.
Ugunduzi huo unaleta athari kwa baaadhi ya wanaume na kuwafanya wazidi kujiona kwamba ngono ni kila kitu kwao, kwa sababu kuna hadi mtu kawatengenezea bidhaa inayotimiza hitaji lao la kingono!
Mara baada ya kufanya ugunduzi huo alidai kwamba, hiyo midoli itapunguza gharama ukilinganisha na ukiwa unaishi na mwanamke, baadhi ya wanaume wakadanyika kirahisi kama vile Eva alivyodanganywa pale bustanini na nyoka wakashindwa kugundua kuwa midoli haiwezi kuzaa watoto!
Baadhi yao hawakufikiria ni kipi ambacho hiyo midoli inaweza kuwafanyia zaidi ya ngono.
Hawakujiuliza kwanini Mungu aliweza kutuumbia wanawake wa nyama! Pengine labda walifikiri ya kwamba, Muumba wetu kutuumbia wanawake wa nyama alikuwa ni mpumbavu, ilihali Mungu aliumba vitu vyote kwa utaratibu!
Na kama walikuwa wanakwepa gharama basi kuna kitu hakikuwa sawa kwenye mfumo wa ubongo wao, kwa sababu hata wao wenyewe hutumia gharama katika kuishi kwao, basi si ajabu hata mwanamke naye akahitaji kugharamikiwa.
Kwa mfano kuna bajeti ya kula kila siku, mdoli hauwezi kula. Kuna bajeti ya mahitaji muhimu ya kila binadamu, lakini mdoli hauwezi kuhitaji, kwa hivyo wanaume walidanganyika tu, wakajikuta wameingizwa mjini kwa sababu ya kutengenezewa fikra za kingono.
Hata hivyo ukiingia kwenye tovuti mbalimbali utaona karibu kila mahali zimetapakaa video za ngono pamoja na picha chafu!
Kinachokisikitisha zaidi ni kwamba katika siku hizi za usoni baadhi ya watu wanatumia hata intanenti, mitandao ya kijamii pamoja na vyombo mbalimbali vya habari kupitia wasanii ili kueneza ushoga lengo likiwa ni kuingiza mtizamo wa ngono kwenye fahamu za kila mwanadamu!
Mpenzi upate kujua kwamba kile kinachoingia ndicho hupima kile kitakachotoka, kwa maana hiyo endapo kila siku utakuwa unaingiza masuala yahusuyo ngono na mawazo yako yatakuwa ni ngono tu, hii inamaanisha kwamba utakuwa unaitikia kufanya ngono tu matokeo yake utajikuta ushakuwa mtumwa wa ngono na utakuwa mtumwa kweli kwa maana umejiona hivyo.
Rafiki, usiruhusu maendeleo ya sayansi na teknolojia yakufanye uwe mtumwa wa ngono.
Unapowaza jana nilikuwa na nani, leo nitakuwa na nani au nitafute milioni tisa nikafanyiwe upasuaji wa nyonga ili niwe na shepu mwanana, ndivyo unavyozidi kujifirisi na kumtajirisha mwenye kampuni inayotoa hudumua hiyo!
Pengine labda ungejua hata mpango wa Mungu kukuumba ungeutafuta ufalme wake kwanza ili uishi naye milele maadamu huyajui mapenzi yake unaweza ukaishia kufa na shepu lako na mchwa wakafaidi zaidi😒!
Leo nakusanua tu, kabla ya sayansi na teknolojia watu waliishi, na walifurahia maisha! Kwanza hakuna jipya chini ya jua!
Yote yanayofanyika yalishafanyika na yatafanyika, hii inamaanisha kwamba wewe siyo kwanza kufanya hivyo, kwa hivi usiruhusu ujinga wa kutokuijua sayansi na teknolojia ukuendeshe!
Achana na fikra za ngono, jione ukileta mchango mzuri kwenye jamii yako! Je kupitia ngono mchango gani zaidi ya kupata maradhi, kufirisika na kujizolea nuksi na mikosi?
Mungu hakukuumba kwa ajili ya hilo! Tafuta kusudi la kuumbwa kwako! Usiruhusu sayansi na teknolojia ikuendeshe bali itumie kwa manufaa uweze kubadili jamii yako na taifa lako!
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwalimu, Mwandishi Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329/0773284329 Au tembelea blog yangu kwa kuandika kingmentorshipprogram.blogspot com
Comments
Post a Comment