Jinsi Ya Kuwa Mtu Usiyesimamishwa Na Chochote Kile..

Mbinu Ya Saba Bobea Katika Eneo Fulani

Vile unavyokuwa unajua kuhusu jambo Fulani kwa undani  ndivyo unavyopata ujasiri na utayari wa kufanya jambo hilo. 

Kwa kusema hivyo, unapobobea katika eneo Fulani inamaanisha kwamba, utakuwa ni yule mtu ambaye huwezi ukasimamishwa kwa sababu tayari una ubobevu wa kutosha na unalijua eneo hilo kiundani.

Ndugu unatakiwa kujua kwamba hakuna nyota wa eneo zaidi ya moja, kwa sababu kila nyota huamua kubobea katika eneo moja ili adhihirishe uwezo wake. 

Ndivyo unavyopaswa kufanya kwa kuchagua eneo moja kisha lichimbue kiundani ili upate uelewa ulio mpana kuhusu eneo hilo! 

Baada yaa hapo dhihirisha ukomavu wako na uelewa wako katika eneo hilo ama hakika hakuna kitakachokusimamisha! 

Kwa mfano mbali na kugundua kuwa nina uwezo wa kuandika, sikuanza tu kuandika moja kwa Moja!

Niliamua nijifunze kwanza kozi ya uandishi ili niweze kuandika vizuri, nilitambua fika kabisa ya kuwa, kipaji pekee huwa hakitoshi, kwa sababu utahitaji maarifa na taarifa sahihi jinsi ya kutumia kipaji chako ili kikunufaishe. 

Kwa hivi mbali na kupenda sana kuandika. Ilibidi nichague eneo moja tu kati ya mengi ninalotaka nibobee ili nijikite zaidi katika kuliandikia! 

Nilipoona uhitaji wa watu wengi ni utambuzi binafsi, ndipo sasa nikaamua nijikite kuandikia eneo la maendeleo binafsi kwa minajili ya kuwafanya wasomaji wangu wapate kujitambua.

Mpaka sasa hii naandika Makala hii ni kwa sababu nimeamua kubobea katika eneo hili. 

Hata makala hii ni ya maendeleo binafsi kwa sababu inakufundisha namna gani unaweza ukabadili maisha yako kwa kubadili namna unavyojiona. 

Kwa hivi huwa Napata ujasiri na utayari wa kuandika kwa sababu tayari nimebobea kwenye eneo hili.

Huenda ukawa ni daktari, mwalimu, nesi, mhasibu au mfanyakazi yeyote yule. 

Unachopaswa kufanya ni kuamua kubobea kwenye eneo mojawapo kutoka kwenye kitengo ulichopo.

Mimi hapa ni mwalimu mtaalamu lakini nimebobea kwenye Ujasiriamali!

Lakini pia, kwa daktari unaweza ukabobea kwenye ugonjwa Fulani na kwa huo ukadhihirisha ukuu wako. Kwa mfano unaweza ukaamua kuwa daktari wa meno tu! 

Unapoamua kubobea eneo moja tu unapata ujasiri na uwezo mkubwa wa kukabili changamoto zote katika eneo hilo kwa sababu unalijua kiundani.

Tofauti na yule mtu ambaye analijua eneo hilo juujuu tu. 

Kwa hivi ukibobea eneo mojawapo utajikuta unakuwa ni aina ya yule mtu usiyeweza kusimamishwa. 

Na hivi ndivyo ambavyo ubobevu hufanya mtu asisimamishwe na chochote kile.  

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri...

Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No 07 44284329/0773284329 Au tembelea blog yangu kwa kingmentorshipprogram.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...