Kama Hujui Kusudi Lako, Hujui Maana Ya Maisha Yako...

Mbali na kuwa kila mwanadamu ana uhuru wa kuishi hapa duniani pasipo bugudhi wala usumbufu, kuna wakati ukifika, uhuru huo hugeuka na kuwa uchungu na majuto makubwa sana, hasa pale inapotokea mtu huyo akashindwa kujua kwanini anaishi na kwanini maisha yake yapo…

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika, zimeonesha kwamba wapo watu wengi sana ambao wanaishi huku wakiwa wamechanganyikiwa maishani mwao kwa sababu hawana majibu sahihi juu ya maswali mbalimbali ambayo daima hujiuliza, na mara nyingi maswali hayo huwa yamelenga zaidi katika kuhoji kwanini maisha yao yapo. 

Ukweli ni kwamba, katika ulimwengu huu ulio mpana sana, karibu kila mtu aliye hai huwa anajikuta akijihoji juu ya maswali yafuatayo; “Hivi mimi ni nani”, “Kwanini nilizaliwa” na “Kwanini ninaishi.” 

Mbali na kuwa wengi wao hujiuliza maswali kama hayo, huishia kutopata majibu muafaka, matokeo yake hubaki wakiwa hawajui wafanye nini na maisha yao! 

Bila shaka hata wewe ulishawahi kujiuliza maswali kama hayo na hukupata majibu sahihi!

Habari mbaya ni kwamba, siyo wewe tu, bali wapo watu wengi sana ambao wanapitia hali kama yako. 

Kwa hiyo basi kutokana na watu hao kujihoji juu ya maswali hayo na kukosa majibu fasaha hujikuta wakichanganyikiwa zaidi katika kuishi kwao. 

Na ndiyo maana hapa duniani hakuna mtu ambaye huishi kwa kuchanganyikiwa zaidi maishani mwake kama mtu anayeishi huku akiwa hajui kusudi la maisha yake!  

Na pale inapotokea mtu akawa anajihoji juu ya uwepo wa maisha yake inamaanisha kwamba anakuwa anatafuta maana ya maisha yake.

Na maana halisi ya maisha ya kila mwanadamu ipo kwenye lile kusudi lililobebwa maishani mwake. 

Kwa bahati mbaya watu wengi hawajui kwamba kuna kitu kinaitwa kusudi na wanatakiwa wakiishi! 

Na hii ndiyo sababu kubwa ambayo imesababisha zaidi ya asilimia 80 ya watu duniani kote wasiliishi kusudi la kuumbwa kwao, wakaishia kufanya masuala mengi sana ambayo hawakuumbiwa waje wayaishi kwa minajili ya kutengeneza fedha huku wengine wakikosa kabisa hata kitu cha kufanya! 

Huenda hata wewe umekuwa ni mtu ambaye mpaka sasa hujajua kwanini uliumbwa, upo hapa duniani kwa kusudi gani na unatakiwa ufanye nini ili uweze kutimiza kusudi la kuumbwa kwako!

Rafiki, unatakiwa kujua kwamba maisha pasipo kusudi si kitu, kwa sababu maana halisi ya maisha imebebwa na kusudi. 

Hii ni sawa na kusema kuwa, kama haujui kusudi la kuumbwa kwako maana yake umeshapoteza maana halisi ya maisha yako!  

Na, ikiwa umeshapoteza maana halisi ya maisha yako, maana yake hakuna ulazima wa wewe kuendelea kuishi tena. 

Kwa sababu hata kama utaendelea kuishi hakuna kitu chochote cha maana ambacho unaweza ukakifanya kwa ajili ya maisha yako, dunia yako, jamii yako pamoja na maisha ya watu wengine.

Ukweli ni kwamba kila mtu kaumbwa kwa kusudi Fulani, lakini kuligundua kusudi siyo kitu rahisi na ndiyo maana huwa naelimisha kupitia kuchapisha makala mbalimbali ili zikusaidie!

Na, moja ya sababu ambayo husababisha watu wengi washindwe kugundua kusudi la kuumbwa kwao, ni kutokana na uwepo wa mifumo mbalimbali ambayo huwatengenezea kusudi dogo lililo tofauti na kusudi kuu la kuzaliwa kwao.  

Unatakiwa kujua kwamba, ukishatengenezewa kusudi na mfumo Fulani utajikuta ukiridhika kabisa na ukaishia kuona kama hilo ndilo lilikuwa kusudi la kuumbwa kwako kitu ambacho siyo kweli kabisa! 

Kutokana na hilo watu wengi hujikuta wakitumia muda wa maisha yao yote kuliishi kusudi dogo na siyo lile kusudi kuu la kuumbwa kwao, hali ambayo hushusha hadhi ya maisha yao pamoja na kuwasababishia wapige hatua ndogo kimaisha. 

Mara nyingi hali hii huchangiwa na watu hao kuiamini zaidi mifumo iliyowatengenezea kusudi hilo, pasipo kuangalia wao wenyewe wanapenda kufanya nini na wanaweza wakatumikaje hapa duniani, ukiachilia mbali na vile ambavyo mifumo imewatengeneza.

Mpenzi msomaji upate kujua kwamba hakuna raha yoyote ile utakayoipata ikiwa utaliishi kusudi dogo tu, zaidi ya yote utakutana na changamoto pamoja na makwazo ya hapa na pale.  

Hii ni kwa sababu mfumo uliokutengeneza utakuonesha kwamba unastahili kuwa mtu Fulani kwa sababu umekutengeneza uwe hivyo, ilihali katika uhalisia huenda hakuzaliwa ili uje uwe huyo uliyetengenezwa uwe!

Na, huenda ukawa unatumia nguvu kubwa sana katika kufanya hicho unachokifanya kwa sababu umetengenezwa ili ukifanye, na siyo kitu ambacho uliumbiwa uwezo asili uje ukifanye! 

Na hakuna kitu kigumu kama kufanya kitu ambacho hukuumbwa uje ukifanye.

Unaweza ukawa unajiuliza, hivi Kusudi ni nini? Usijalii mwendelezo wa somo hili utadokeza hilo!

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!

Mwendelezo Wa SoMo Hili Utaendelea Kwa Siku Ya Kesho!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwalimu, Mwandishi Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329/0773284329 Au tembelea blog yangu kwa kuandika kingmentorshipprogram.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...