Kama Una Roho Nyepesi Tafadhali Usisome Ujumbe Huu…
Ila Hapa Duniani Kuna Watu Ni Ving’ang’anizi... Ndugu, Si Umeshatahadharishwa Kwamba Usisome Lakini? Ama Hakika Unachokitafuta Utakipata...
Je, Una Roho Ngumu Kiasi Kwamba, Utaweza Kuyakabili Mambo Mazito Yatakayojadiliwa Humu? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Basi Songa Nayo…
Hivi Unafahamu Kuwa Hapa Duniani Tunaishi Watu Wenye Matabaka Mawili Tofauti, Ambao Ni: Watawala Na Watawaliwa? Na Katika Haya Makundi Mawili Watawala Ni Wachache Huku Wanaotawaliwa Wakiwa Ndiyo Wengi Zaidi?
Huenda Hata Wewe Ukawa Unatawaliwa Na Hujui, Leo Nipo Hapa Kukusanua Kwa Kukuletea Ukweli Unaopaswa Kuujua, Lakini Sikuamuru Ufanye Nini Kwa Sababu Wajibu Wangu Mimi Ni Kukuonesha Tu! Nawe Utachukua Hatua Ikiwa Utakuwa Na Nia Thabiti Ya Kubadilisha Maisha Yako!
Mara Zote, Tabaka Tawala Huweza Kuanzisha Mifumo Fulani Hivi Ambayo Wale Wanaotawaliwa Wasipotizama Kwa Undani Huona Kana Kwamba Wananufaika Nayo, Ilihali Mifumo Hiyo Imetengenezezwa Ili Iwanyonye Pamoja Na Kuwazuia Wasiuishi Uwezo Wao Na Maono Yao...
Matokeo Yake, Mifumo Hiyo Huwageuza Na Kuwafanya Wawe Wafanyakazi Wao, Ili Watumie Maisha Yao Yote Kufanya Kazi Kwa Kumtimizia Mwajiri Wao Malengo Yake, Huku Malengo Yao Yakishindwa Kukamilika Kutokana Na Kupewa Maslahi Kidogo Pamoja Na Kutumia Muda Wao Mwingi Kufanya Kazi Za Watu!
Na Moja Ya Mfumo Hatari Sana Ambao Wanautumia Ni Mfumo Wa Elimu, Kwamba Unakuta Mtu Anafundishwa Vitu Visivyo Halisi Huku Vingine Vikiwa Havina Na Matokeo Ya Moja Kwa Moja Katika Maisha Yake Ili Uwezo Wake Ufungwe, Na uwezo Wake Ukishafungwa Maana Yake Mtu Huyu Atasoma Ili Tu Apate Vigezo Vya Kuajiriwa.
Baada Ya Kuajiriwa Apate Mshahara, Na Kwa Vile Mshahara Huo Utarahasisha Maisha Yake Basi Atatulizwa Kwa Huo! Ama Hakika Pesa Ni Sabuni Ya Roho!
Kwa upande Wangu Hata Mimi Ni Msomi, Ninao Ujasiri Wa Kusema Kuwa Nilisoma Ili Nije Nipate Ajira, Kwa Sababu Kile Ambacho Nimesomea Hakina Matumizi Halisi Kwenye Maisha Yangu Zaidi Ya Kukitumia Ajirani TU, Ili Nilipwe mshahara, Na hakuna Kitu Kibaya Kwenye Mshahara Kwa Sababu Kila Mtenda Kazi Anastahili Posho Yake!
Sasa Kama Nimesoma Halafu Siwezi Nikatumia Kile Nilichojifunza Kukabili Maisha Yangu Nitafanyaje? ...Ndiyo Upo Sahihi, Ni Lazima Nitafute Kazi Nipate Maokoto Ili Maisha Yaendelee!
Na Hivi Ndivyo Ambavyo Watu Wengi Tumegeuzwa Na Kuwa Tegemezi Kwenye Kazi. Na Hatuoni Kwamba Kuna Kitu Kingine Ambacho Tunaweza Tukakifanya Kwa Sababu Uwezo Wetu Binafsi Umefungwa!
Matokeo Yake Fikra Zetu Huhama Na Kuwa Tegemezi Kwenye Mshahara Tu, Kiasi Kwamba Tutakuwa Tunafanya Kila Linalowezekana Ili Tusifukuzwe Kazi, Huku Na Mabosi Wetu Nao Wakituahidi Kutuongezea Maslahi Zaidi Ili Tufanye Kazi Katika Mazingira Rafiki.
Hili Pambano Linakuwa Kali Sana, Unakuta Mfanyakazi Anapambana Sana Ili Bosi Asimfukuze Kazi, Na Bosi Naye Anakuwa Anapambana Sana Ili Asiache Kazi Kwa Sababu Akiacha Kazi Atakosa Mtu Wa Kumtimizia Malengo Yake.
Matokeo Yake Mtu Huyo Hujikuta Akiwa Tegemezi Kwenye Kazi, Hali Ambayo Husababisha Ashindwe Kuyaishi Maisha Halisi Ambayo Alitakiwa Ayaishi Hapa Duniani Yakiwa Ndiyo Maono Yake!
Na Ikifika Wakati Akawa Tegemezi Zaidi Kwenye Kazi Basi Bosi Ataanza Hadi Kumtishia Kumuachisha Kazi, Na Kwa Vile Mtu Huyo Huwa Hajui Kuwa Kuna Kitu Kingine Ambacho Anaweza Kufanya Zaidi Ya Kile Alichokisomea Ili Akifanye Basi Huvumilia Manyanyaso Yote.
Na Watu Wengi Hufanyiwa Hayo Kwa Vile Wamekosa Maono Kwenye Maisha Yao, Hii Inamaanisha Kwamba Watu Hao Huwa Hawaoni Thamani Kubwa Waliyoibeba Maishani Mwao Pamoja Na Ule Uwezo Walioumbiwa Ili Uwasaidie Katika Kuishi Hapa Duniani!
Ukweli Ni Kwamba, Ukitaka Kumuweza Mtu Mvivu Asiye Na Maono Maishani Mwake Mpe Kazi Nzuri Na Mshahara Mzuri, Na Akitaka Kuacha Kazi, Muahidi Kumuongezea Mshahara.
Cheza Na Akili Zake Ili Atumie Muda Wake Wote Kutimiza Malengo Yako Na Ndoto Zako, Huku Ndoto Zake Na Malengo Yake Yakibaki Hewani!
Hivi Ndivyo Ambavyo Watu Hucheza Na Akili Zako Ili Wakutumie Watakavyo. Ukweli Ni Kwamba Kukosa Maono Katika Maisha Kumewafanya Watu Wengi Waone Wapo Hapa Duniani Ili Waishie Kuwa Waajiriwa TU, Huku Wakibadilisha Thamani Kubwa Ya Maisha Yao Na Mshahara!
Na Ndiyo Maana Wengi Huridhika Na Kazi Zao Na Mshahara Wakashindwa Kugundua Kwamba Kuna Kitu Kinaitwa Kusudi Na Maono Na Huenda Wangeviishi Wangefanikiwa Kwa Urahisi Zaidi Kuliko Hata Yale Mafanikio Wanayoyapata Pindi Wakiwa Wanatumikia Ajira Zao!
Kwa Kusema Hivyo Kuwepo Kwa Mshahara Na Kazi Hufunga Ubongo Wa Watu Na Kuwafanya Hao Watu Washindwe Kuona Upande Wa Pili Wa Sarafu Uliobeba Kusudi La Kuumbwa Kwao Pamoja Na Maono Yao.
Kwa hiyo Leo Hii Kabla Hujawa Bize Kutafuta Kazi Ili Ulipwe Mshahara, Jaribu Kujihoji Unaweza Ukafanya Nini Na Umebeba Maono Gani Kuhusu Maisha Yako!
Na Endapo Utayaishi Maono Yako Utatengeneza Fedha Kirahisi Zaidi Kwa Sababu, Watu Watakuwa Tayari Kukupa Pesa Ili Kubadilishana Na Thamani Unayoitengeneza Kupitia Kuyaishi Maono Yako!
Kumbuka Fedha Huwa Haitafutwi Bali Huvutwa, Na Mbinu Rahisi Ya Kuvuta Pesa Ni Kupitia Kuyaishi Maono Yako!
Unatakiwa Kujua Kwamba Moja Ya Athari Kubwa Ambayo Watu Wanaoishi Kwa Kutegemea Kazi Wanapitia Ni Kugeuzwa Na Kuwa Watumwa.
Na Ifahamike Kwamba Kuna Aina Mbili Za Utumwa Yaani: Utumwa Wa Kulazimishwa Na Utumwa Wa Hiari.
Watu Wengi Ni Watumwa Wa Hiari Na Hawajui Kuwa Ni Watumwa! Unatakiwa Kujua Kwamba, Kufanya Kitu Ambacho Kukuumbiwa Uje Ukifanye Maana Yake Ni Utumwa!
Hebu Jaribu Kuvuta Picha Ulitakiwa Uweze Kuwa Mgunduzi Wa Madawa Fulani Yawatibu Watu, Ulitakiwa Uwe Mgunduzi Wa Kifaa Fulani Kirahisishe Maisha Ya Watu, Ulipaswa Uanzishe Huduma Fulani Ili Uwasaidie Watu, Na Pengine Labda Ulitakiwa Uwe Mwalimu Wa Mataifa Ukifundisha Watu Ukweli Uhusuo Maisha, Lakini Sasa Hivi Uko Zako Bize Ajirani!
Na, Kwa Vile Unafanya Kitu Ambacho Hukuumbwa Uje Ukifanye Wewe Huna Tofauti Na Mtumwa. Hata Hivyo Mbali Na Kuwa Unafanya Kazi Au Umeajiriwa Na Unalipwa Mshahara Mzuri Tu Endapo Utakuwa Unaishi Nje Ya Kusudi Lako Na Maono Yako Wewe Bado Utakuwa Ni Mtumwa Asiye Na Faida!
Hata Mimi Ninayeandika Hili Ni Mtumwa, Lakini Afadhali Ya Mimi Kwa Sababu Nimeshatambua Kuwa Ni Mtumwa Na Ninachukua Hatua Tayari, Ndiyo Maana Nimekuja Hapa Kukusanua Na Wewe Mwenzangu Ili Utafute Namna Ya Kuukataa Utumwa.
Je, Wewe Ni Mtumwa Wa Hiari Unayejificha Kwenye Mwamvuli Wa Kulipwa Mshahara? Je, Unataka Utengeneze Kipato Huku Ukiwa Huru?
Kama Jibu Ni Ndiyo Ninakushauri Usome Kitabu Changu Kinachoitwa; Nguvu Ya Maono Kwa Mwanadamu…
Ukweli Ni Kwamba, Kitabu Hiki Kitakufundisha Ukweli Wa Maisha Usiofundishwa Popote Pale, Na Ukishakisoma Tu, Utaanza Kuuepuka Utumwa, Nawe Utaanza Kuwa Mtawala.
Unasubiri Nini? Unataka Uendelee Kubaki Utumwani? Rafiki, Kama Unataka Uendelee Kubaki Utumwani Nakupa Pole Sana, Ama Hakika Utapata Taabu Sana.
Kujipatia KITABU Nakala Ngumu Ya KITABU Hiki Tuma Neno KITABU Kwenda Whatsapp No 07 44284329...
Kujipatia Nakala Laini Ya KITABU Hiki, Tuma 5000/= Kwenda No 0744284329. Halafu Tuma Screenshot Ya Muamala WAKO Whatsapp!
Comments
Post a Comment