Hii Ni Kwa Wale Wanaotaka Kupanga Malengo Ya Kifedha Lakini Hawajui Wafanyaje...

Habari Yako Rafiki Yangu? Ni Matumaini Yangu u mzima wa afya!

Leo king Mentorship Program imekuandalia somo linalohusu; "Hatua Za Kuzingatia Ukiwa Unapanga MALENGO Ya Kifedha"

Zingatia hatua hizi ili ufanikiwe kifedha, kama unaamini ya kwamba kuwa na fedha ni dhambi usifuatilie somo hili!

Pia, kama huna mpango wa kufanikiwa kifedha hata usijisumbue kusoma!

Hata hivyo kama umeridhika na hali ya kutengeneza kipato duni usifuatilie!

Si hivyo tu kama umeridhika na Mshahara (pingu ya dhahabu mkononi mwako) a.k.a mbio za panya+utumwa usifuatilie!

Kama Unataka Ubadili hali yako ya kifedha karibu hapa ndipo nyumbani!

Nini maana ya malengo ya kifedha?

Malengo ya kifedha ni kiasi fulani cha fedha ambacho mtu anakusudia kukipata Ndani Ya kipindi fulani cha muda!

Kwa mfano; "ninatengeneza 12,000,000/= kwa mwaka 2025"

Ukisoma vizuri utagundua kuwa hilo lengo ni mahususi, linapimika, ni halisi, linawezakana na lina ukomo wa muda"

Kwa kusema hivyo mtu anayekuwa ameazimia Lengo hilo manake anakuwa na picha KAMILI juu ya Pato analotakiwa alitengeneze kwa mwaka 2025.

Unatakiwa kujua kwamba huwezi ukatimiza lengo ikiwa hukuazimia lengo, hivyo basi ili ufanikiwe kutekeleza MALENGO yako ni lazima uanze kuazimia malengo kwanza!
 
Kama ulikuwa na shauku ya kutaka kujua kuhusu kuazimia malengo ya kifedha basi somo la leo linaenda kukusaidia!

Je zipi ni hatua za kuzingatia wakati napanga MALENGO Ya Kifedha?

1. Andika Kiasi cha Fedha Unachotaka Kukipata.

Uwazi katika pato unalotaka kulitengeneza ni muhimu, usiseme unataka utengeneze kiasi kingi cha fedha taja kiasi mahususi, kingi ni nini? 

Watu wengi wanashindwa kufanikiwa kifedha kwa sababu hawaweki kwa uwazi ni kiasi gani cha fedha wanachotaka kukitengeneza!

Unatakiwa udokeze kiasi cha fedha unachotaka kukitengeneza, kiasi kwamba hata mtoto wa darasa la kwanza akisoma lengo lako aelewe kile unachotaka kukikamilisha!

Ukiona lengo lako linakuchanganya hata wewe uliyeazimia, basi ndivyo utakavyochanganyikiwa katika kutekeleza na hautafanikiwa kabisa!

Je, 2025 umeazimia utengeneze kiasi gani cha fedha? Au nikuache uendelee kujifukiza? 😂😂😂

2. Andika Ukomo wa Muda Ambao Unataka Lengo Lako La Kifedha Litimie...

Huwezi ukafanikisha lengo lako pasipo kuweka ukomo wa muda ambao unataka lengo lako liweze kutimia!

Pasipo kuweka ukomo wa muda huwezi ukajua ni lini hasa lengo lako la kifedha linatakiwa liwe limekamilika, kwa kusema hivyo utaona muda ukizidi kwenda huku lengo lako likibaki pale pale!

Kuna watu wanaweka MALENGO mazuri shida hawaweki ukomo wa muda!

Kutokuweka ukomo wa muda kutafanya usiwe na mipaka, hutajua ukomee wapi!

Kitakachotokea ni kwamba, lengo litageuka na kuwa lengo la maisha! Matokeo yake utaweza hata ukafa nalo kwa sababu hujaweka ukomo wa muda!

Unatakiwa uazimie hivi; "Natengeneza 12,000,000/= Mwaka 2025"

3. Gawanya Pato Lako Katika Vipindi Vifupi Vitakavyokurahisishia Utekelezaji Wake...

Njia ya kumla tembo aliye mkubwa ni kupitia kumkata katika vipande vidogo vidogo! 

Kwa kusema hivyo unatakiwa uligawe lengo lako katika vipindi vifupi vya muda, ili ulifanikishe lengo lako kirahisi, ikiwa ni pamoja na kuepuka kukata tamaa!

Kwa mfano kama lengo langu ni kutengeneza 12,000,000/= nitafanya kama ifuatavyo;

Katika mwezi; 12,000,000÷12=1000,000/=

Katika Siku; 12,000,000÷365= 32876. 7

Katika wiki; 12,000,000÷52= 230,769.2

Nikishagawa pato langu katika vipindi vya muda, sina budi kuhakikisha ninatengeneza kiasi cha fedha kwa kadri ya kipindi mahususi cha muda!

Kila siku ni lazima nitengeneze hicho kiasi cha fedha, kila wiki ni lazima nifanye hivyo na kila mwezi ni lazima nitengeneze hicho kiasi cha fedha!

Mwishowe ukifika mwezi wa 12 nitakuwa na 12,000,000/=

4. Orodhesha Vyanzo Vya Mapato Utakavyotumia Kupata Pato Hilo...

Hakuna lengo ambalo hujitekeleza lenyewe, kwa maana hiyo ili ufanikiwe lazima uorodheshe vyanzo vya mapato vitakavyotumika.

Angalia mfano huu wa mapato kwa kila mwezi: 

500,000/=Mshahara.
200,000/= huduma ya usimamizi.
280,000/= ROI (return on investment)
200,000/= mauzo ya vitabu
100,000/= huduma ya ushauri. N.k
Huo ni kwa mfano tu, hivyo ndivyo unavyopaswa kufanya...

5. Panga mkakati wa jinsi ya kutimiza malengo yako ya kifedha...

Kanuni ya kichocheo na matokeo inasema; "kila kitu hutokea kutokana na sababu"

Hii ni sawa na kusema kuwa na lengo la kifedha pasipo kuweka mkakati wa kulifanikisha lengo hilo ni kazi bure!

Kwa mfano kama unataka kuongeza idadi ya wateja wa huduma yako unaweza kuweka mkakati kwa kusema; "nitatafuta wateja wapya kila siku kwa kulipia matangazo Instagram na Facebook ili nipate wateja wengi...

Nitafundisha kila siku mtandaoni kama nyenzo ya kuwavuta na kuwasogeza watu kwenye huduma yangu! 

Unatakiwa kujua kwamba kuna wakati mwingine ili uweze kutekeleza malengo yako unatakiwa uwe mtu ambaye hukuwahi kuwa...

6. Anza kufanya kwa vitendo mara.

Hapa unatakiwa kuweka mikakati yako kwenye vitendo...

Kwa mfano Kama umeweka mkakati wa kutafuta wateja wapya anza kutafuta, Kama ni kufanya kazi anza kufanya kazi, Kama ni kuweka akiba anza kuweka akiba na kama ni kulipa madeni anza kulipa madeni.

Hutakiwi kupoteza muda! Kumbuka iii jambo fulani litokee ni lazima kipindi fulani cha muda kipite.

7. Fanya tathmini ili kupima mwenendo wako kama unapiga hatua au laah...

Ni muhimu kufanya tathmini ili ujue umefika wapi na ufanye nini ili ufike kule ulikopanga kufika!

Kumbuka, maisha ambayo hayafanyiwi tathimini hayana maana!

Pia, unatakiwa kufanya tathmini ya kifedha kwa kuzingatia kila kipindi cha muda ulichokigawa, kama tulivyoona kwenye hatua ya nne.

Kama una Chanzo kimoja tu cha mapato nakupa pole sana, safari yako ya kufanikiwa kifedha itakuwa ndefu mno! 

Kwa mfano, fanya tathmini ya lengo la siku ili kujua kama kipato ulichopanga kupata kwa siku kimetimia!

Fanya tathmini ya wiki ili kujua kama Lengo lako la wiki limetimia...

Fanya tathmini ya kila mwezi ili kupima kile Kiasi ulichopanga kuingiza kwa mwezi kimetimia...

Fanya tathmini ya mwaka ili kubaini umefika wapi!

8.Fanya kwa mwendelezo mpaka lengo lako Litimie...

Hakuna kitu ambacho huua ndoto za watu kama kukosa kwa Sanaa ya mwendelezo...

Kwa mfano Kama umeazimia kuweka 1000,000/= basi fanya kwa mwendelezo kwa kuweka kila mwezi hadi Lengo Lako Litimie..

Unatakiwa kufanya kila jambo kwa mwendelezo yaani kuanzia tathmini na kila unachopaswa kufanya kifanye kwa mwendelezo..

Ndugu pambana sana ili kutimiza malengo yako ya kifedha.

Unatakiwa ujijengee tabia ya kuwa mchapakazi, tabia ya kuweka akiba, tabia ya kuamka mapema, tabia ya kufungua ofisi mapema, tabia ya kutokughairisha mambo, tabia ya kujifunza pamoja na tabia ya kujiwazia mema muda wote..
Mpaka kufikia hapo utakuwa ni unstoppable! 

No one will stop you from going!

Hebu kuwa na mwendelezo katika kutekeleza malengo yako ya kifedha! Usifanye kwa kudonoadonoa!
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwalimu, Mwandishi Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329/0773284329 Au tembelea blog yangu kwa kuandika kingmentorshipprogram.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...