Jinsi Ambavyo Mazingira Na Mapendekezo Hasi (Negative Heterosuggestions) Huathiri Maisha Ya Mwanadamu...

Habari yako champion wangu wa nguvu? Ni matumaini yangu uko salama! Pole na mizunguko ya hapa na pale ya kutwa nzima ya leo!

Kwa Siku Ya Leo King Mentorship Program imekuandalia somo linalohusu; "Jinsi Ambavyo Mazingira na pendekezo hasi, vinavyoathiri fikra za Mwanadamu."

Kama Unataka kubadili fikra zako Ubadili maisha yako, ninakushauri usome makala hii mpaka MWISHO, endapo utafanya hivyo hutajutia kabisa muda wako uliotumia kusoma makala hii...

Duniani, ingawa tunazaliwa tukiwa sawa kwa msingi, tunatofautiana kwa kiwango kikubwa kiuwezo, kifikra, na kujitambua kulingana na mazingira tunayokulia. 

Mazingira haya yana mchango mkubwa katika kupima uwezo wetu binafsi na kiwango cha kujitambua. 

Kwa mfano, mazingira bora yanaweza kukuza uwezo wa mtu na kumsaidia kuona fursa za maisha, wakati mazingira yasiyo na msaada yanaweza kumfunga mtu kwenye ukomo, kumfanya ajione kama hana uwezo wa kutosha na bila matumaini.

Mazingira ni nguvu isiyoonekana wala isiyo halisi inayokutawala kwa namna kubwa, ikihusisha fikra zako, mitazamo yako, mawazo yako, na mienendo yako. 

Watu wengi wanajikuta wakifungwa na mazingira waliyokulia, hali inayowafanya wajione wanyonge au wasiostahili. 

Hali hii inachangia kupunguza kiwango chao cha kujitambua na uwezo wao wa kufanya mabadiliko chanya maishani mwao.

Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba mazingira haya mara nyingi hutengenezwa na wengine na siyo lazima yaendane na uwezo wetu au vipaji vyetu. 

Kuishi katika mazingira haya kwa kujilazimisha kunaweza kudhoofisha uwezo wetu wa kufikiri kwa uhuru na kujitambua. 

Tunahitaji kuwa na mtazamo wa kubadilisha mazingira haya au kutafuta mazingira mapya ambayo yanashawishi na yanamsaidia mtu kufikia kilele cha uwezo wake.

Ukiachiilia mbali hilo, kuna kitu kinachoitwa pendekezo hasi, hili ni oni hasi linalotoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine ambapo yule anayeambiwa akilipokea kama lilivyo pasi na kulichuja humletea athari kifikra pamoja na kushusha kiwango chake cha Kujitambua! 

Je ushalipokea mojawapo kati ya haya?
Kutoka utotoni, wengi wetu tumepokea mapendekezo hasi kutoka kwa watu wa karibu bila kujua jinsi ya kuyakataa, na hivyo yakawa sehemu ya maisha yetu. 

Mapendekezo haya yameathiri jinsi tunavyojiona, tunavyojiwekea mipaka, na jinsi tunavyoshughulikia masuala mbalimbali. 

Hali hii imeweza kutufanya tukakubali hali ya kuwa vile tulivyo, wakati kumbe tungeweza kuwa tofauti kabisa kama tungemkataa ushawishi huu hasi.

Mapendekezo haya mabaya, kama vile “Huwezi! Utashindwa Tu! Hutopata Nafasi! Wewe Ni Mkosaji!” na mengineyo, yanachangia sana kudhoofisha fikra zetu na uwezo wa kujitambua.

Yanaweza kumfanya mtu ajione hana thamani au uwezo wa kufanikiwa, na hivyo kupunguza motisha yake.

Kama unavyochunguza kwa karibu, utagundua kwamba watu wa karibu ambao tunaamini ndio wamekuwa wakituambia mapendekezo haya.

Hawa ni pamoja na wazazi, marafiki, ndugu, walimu, na viongozi wa dini. Mara nyingi, tunapopokea mapendekezo kutoka kwa watu hawa, tunachukulia kuwa ni ukweli bila kuangalia uhalisia wa maoni yao. 

Matokeo yake, tunajikuta tukishindwa kujitambua na kutumia uwezo wetu wa kufikiri ipasavyo.

Maoni hasi yapo kila mahali: nyumbani, ofisini, shuleni, na mtaani. Hata hivyo, ikiwa hatutakuwa na uwezo wa kuyakataa na kuyapitia kwa umakini, tutajikuta tukiendelea kuishi chini ya kiwango chetu halisi. 

Ili kujitambua vizuri, ni muhimu kujifunza jinsi ya kuyakataa mapendekezo hasi na kuunda mtazamo chanya wa maisha. 

Hii itatusaidia kuongeza kiwango chetu cha kujitambua na kuboresha fikra zetu.

Nini kifanyike?
Ukichunguza kwa makini, utagundua kwamba mapendekezo hasi mara nyingi yana lengo la kukuongoza kufikiri, kuhisi, na kutenda kulingana na njia wanazotaka wengine. 

Hata hivyo, njia hizi zinaweza kuwa mbaya kwako na kuathiri maisha yako kwa njia hasi. Watu wengine wanaweza kutoa mapendekezo hasi ili kufanikisha maslahi yao wenyewe badala ya yako, hivyo ni muhimu kuwa makini na kuchambua mapendekezo haya kwa umakini.

Katika hali ya kawaida, mapendekezo hasi yanaweza kutufanya tusichukue hatua muhimu katika maisha yetu, kwa sababu tunajikuta tukiruhusu maoni haya kuwa mwongozo wetu.

Huna budi kujipatia muda wa kutafakari kwa kina kuhusu mapendekezo haya na uamuzi wako juu yao. 

Jiulize kama kuendelea kuruhusu maoni haya kuendesha maisha yako ni sahihi au la. Tafakari kuhusu athari za mapendekezo haya kwenye maisha yako na uamuzi wako wa kuweka mipaka.

Kwa ujumla, kusudi la maisha ni jambo la kibinafsi na inabidi litimizwe na wewe mwenyewe. Huwezi kutegemea baba, mama, kaka, mwalimu, mchungaji, au rafiki zako kutimiza kusudi lako.

Anza sasa kujipambanua, kujithamini, na kujiona katika viwango vya juu. 

Kumbuka kwamba unaweza kuwa yeyote unayetamani kuwa, kwa sababu dunia haina mipaka kwa wale wanaoamini na kutenda kulingana na malengo yao.

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwalimu, Mwandishi Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329/0773284329 Au tembelea blog yangu kwa kuandika kingmentorshipprogram.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...