Asilimia 99 Ya Matukio Unayokutana Nayo Maishani Mwako Umeyavuta Mwenyewe Kupitia Fikra Zako...
Wadau walipata kusema kuwa kila kitu hutokea kutokana na sababu, na hakuna kitu hata kimoja ambacho hutokea chenyewe bila sababu inayosababisha kutokea kwake!
Moja ya kanuni ambayo imesababisha kutokea kwa hali mbalimbali ambazo watu wanakutana nazo katika maisha yao ni kanuni ya uvutano!
Hii ni kwa sababu kanuni hii inasema; "wewe ni kama sumaku inayoishi kwa maana hiyo unaweza ukavuta watu, matukio, rasimali na fursa mbalimbali maishani mwako kutokana na fikra kuu zinazotawala na kuongoza maisha yako."
Kwa kusema hivyo kumbe, mawazo na hisia zetu huvuta hali na matukio yanayolingana na nguvu zake katika maisha yetu.
Hii inamaanisha kuwa kile unachofikiria kwa nguvu, iwe ni chanya au hasi, kinaweza kudhihirika katika maisha yako.
Je, mpaka hapa maisha yako yanatawaliwa na fikra hasi au fikra chanya? Huna budi kujipa Jibu!
Misingi ya Kanuni ya Uvutano
1. Nguvu ya Mawazo – Unachokifikiria mara kwa mara kinaathiri hali yako ya maisha. Mawazo chanya huvutia matokeo mazuri, wakati mawazo hasi huleta changamoto.
Kwa mfano unapowaza kuwa hakuna mahusiano yanayodumu nyakati hizi ndivyo unavyovuta mwenzi wa mpito kwa sababu mawazo yako hayamtaki mtu wa kudumu!
2. Nishati na Mitetemo (Vibrations) – Kila kitu, ikiwemo mawazo na hisia, kina mtetemo fulani wa nishati.
Ikiwa una mtetemo wa furaha na matumaini, utavuta hali zinazolingana na nishati hiyo.
Bila shaka huwa unaona kuna baadhi ya watu muda wote wako wamechangamka, ni kwa sababu wana furaha na matumaini...
3. Imani na Matarajio – Unachokiamini na kukitarajia kwa dhati kina nafasi kubwa ya kutokea.
Ikiwa unaamini unaweza kufanikisha jambo, unajiweka katika hali ya kulipokea.
Kumbuka kanuni ya matarajio inasema; "chochote utakachotarajia kuhusu wewe na maisha yako kwa imani kitakuja kudhihirisha ule unabii uliotabiri kuhusu wewe "
4. Shukrani na Mtazamo Chanya – Kuwa na shukrani kwa kile ulichonacho tayari kunasaidia kuvuta mambo mazuri zaidi.
Shukruni kwa kila jambo, kuwa hai ni muhimu kuna wengine hawajafanikiwa hata kuifikia saa hii!
Jinsi ya Kutumia Kanuni ya Uvutano
1. Kuwa Na Mawazo Chanya – Jitahidi kudhibiti mawazo yako na kuelekeza akili kwenye mambo unayotaka, badala ya yale unayohofia.
3.Tumia Uthibitisho (Affirmations) – Maneno kama "Mimi ni mwenye mafanikio", "Ninavutia fursa njema", huweza kusaidia kuimarisha imani yako.
4. Tengeneza Taswira ya Malengo Yako – Wazia mafanikio yako kwa kina, kana kwamba tayari yamefikiwa.
5. Chukua Hatua – Uvutano hauwezi kufanya kazi bila vitendo. Chukua hatua kuelekea malengo yako huku ukiwa na mtazamo chanya.
6. Zingatia Hisia Zako – Hisia zako ni kiashiria cha kama unalingana na kile unachovutia.
Furaha na matumaini vinaonyesha uko katika njia sahihi.
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwalimu, Mwandishi Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329/0773284329 Au tembelea blog yangu kwa kuandika kingmentorshipprogram.blogspot.com
Comments
Post a Comment