Jinsi Manyanyaso Na Masimango Husababisha Kuvunja Kwa Mahusiano...


Kuna watu ambao hutumia nguvu zao, mamlaka yao, vipaji vyao, akili zao, fedha zao, hadhi zao Pamoja na uzuri wao kama fimbo ya kuwachapia na kuwanyanyasa wenzi wao! 

Rafiki, Mungu hajakujalia hivyo vyote ili utumie kama fimbo ya kumkomesha mwenzi wako, bali amekujaalia hivyo vyote ili ukafanyike kuwa baraka kwa mwenzi wako Pamoja na kujenga mahusiano yako yadumu!

Kwa mfano baadhi ya wanawake (siyo wote) humezeshwa sumu na wazazi au watu wao wa karibu kwa kuambiwa: “pambana sana, soma kwa bidi na tafuta fedha kwa nguvu zako zako zote ili mwanaume asije kukunyanyasa.” 

Maneno haya huathiri fikra kwa wanawake wanaoambiwa. Matokeo yake huanza kuona mahusiano kama ni uwanja wa vita na mapambano. 

Na hujikuta wakipambana sana kama njia ya kuja kulipa kisasi kwa waume zao!

Na, ndiyo maana asilimia kubwa ya wanawake (siyo wote) walio maarufu, wazuri sana kisura na kiumbo, wenye nyadhifa Fulani, wasomi Pamoja na wafanya biashara wakubwa huwa hawadumu katika mahusiano. 

Hii ni kwa sababu hutumia umaarufu wao, uzuri wao, usomi wao Pamoja na mafanikio yao kama fimbo ya kuwanyanyasia waume zao, na kwa vile wanaume huwa hawapendi dharau basi huvunja mahusiano hayo!

Hata hivyo kuna baadhi ya wanaume ambao hutumia mafanikio yao kuwanyanyasa wenzi wao.

Utamsikia akisema; “hujachangia chochote hapa, ulikuja hapa huna kitu kwa hiyo huna mamlaka yoyote hapa kwangu”, "una nini kingine cha kunipa zaidi ya tendo?" n.k. 

Hali hii huwafanya wake zao wajihisi vibaya mwisho wa siku huvunja mahusiano. 

Watu hawa hufanya hivyo ili kuponya nafsi zao kutoka kwenye maumivu kwa maana huona ni heri wabaki pekee yao kuliko kunyanyaswa.

Rafiki, epuka kumsimanga mwenzi wako kutokana hadhi yako! Epuka kumfanya mwenzi wako ajione hana thamani mbele yako! 

Binafsi huwa nashangwazwa na hizi jinsia mbili kutokana na mambo yake. Hali hii imechangiwa na tofauti ya kimtizamo pengine labda! 

Kwa mfano endapo itatokea mwanaume akafanikiwa na alikuwa kwenye mahusiano tayari, mwanaume huyu hujikuta akiongeza idadi ya wanawake huku akimdharau kabisa yule aliyeanza naye. 

Na, endapo ikatokea mwanamke akafanikiwa yeye huanza kutokuona umuhimu wa kuwa na mwanaume kwenye maisha yake, hali ambayo humjengea dharau na chuki dhidi ya wanaume!

Kutokana na hilo, basi mahusiano mengi yamekuwa yakivunjika. 

Na, ndiyo maana nimekuandikia makala hii ili ujue ya kwamba, kujaliwa jambo Fulani haimaanishi iwe fimbo ya kumchapia mwenzi wako, bali litumie jambo hilo kama baraka ya kudumisha mahusiano yenu.

Ndugu, kuna watu wanahusiana na hawajabarikiwa mafanikio kama yenu na wanapenda na kuheshimiana. 

Halafu wewe unaanza kumringia mwenzi wako eti kwa madai ya kile ulichojaaliwa?

Rafiki, muombe Mungu akuondelee roho ya kiburi na majivuno ili usimnyanyase mwenzi wako!

Kiburi ni zao la shetani akiwa kazini, roho wa Mungu hawezi kukusukuma uweze kutenda hayo yote kwa mwenzi wako, ilihali ndoa ni taasisi iliyoasisiwa na Mungu mwenyewe!

Ndugu, mshinde shetani kwa kumjali mwenzi wako haijalishi utafanikiwa kiasi gani mthamini mwenzi wako kwa maana huenda ndiyo kabeba baraka za mafanikio yako!

Mpenzi msomaji, kufanikiwa kwako kisiwe kikwazo cha kudumu kwa mahusiano yako! 

Bali kufanikiwa kwako uwe ni mwanzo mzuri wa kujenga mahusiano bora yatakayodumu mpaka milele. 

Kamwe usimpige mwenzi wako wala usimtamkie kwamba mahusiano yenu yameisha na hakuna mapenzi tena! 

Busara haijatufundisha hivyo, na mtu mwenye busara huwa hafanyi hivyo!

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Founder Wa King Mentorship Program, Mwalimu, Mwandishi Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329/0773284329 Au tembelea blog yangu kwa kuandika kingmentorshipprogram.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...