Mwili Wako ni Akaunti ya Akiba: Unachoweka Ndicho Utakachotoa!
Rafiki yangu, leo nakukumbusha jambo moja muhimu sana – *mwili wako ni kama akaunti ya benki.
Kila siku unaamua kuweka akiba nzuri au *madeni ya baadaye kupitia yale unayokula, jinsi unavyotembea, jinsi unavyolala, na vile unavyoishi kwa ujumla.
👉 Ukila vyakula vyenye virutubisho – umeweka akiba.
👉 Ukinywa maji ya kutosha – umeweka akiba.
👉 Ukijipa muda wa kupumzika na kulala vizuri – umeweka akiba.
👉 Ukifanya mazoezi hata kwa dakika 30 tu – umeweka akiba.
Lakini pia...
❌ Ukila chakula cha haraka haraka (fast food) kila siku – unaweka deni.
❌ Ukikwepa maji na kubeba soda kila saa – unaweka deni.
❌ Ukilala saa 3 usiku kila siku ukiwa na simu mkononi – unaweka deni.
❌ Ukikaa muda mrefu bila kusogea mwili – unaweka deni.
Na siku moja, mwili wako *utataka kutoa* kwenye hiyo akaunti – na kama hakuna akiba ya afya, gharama inaweza kuwa kubwa mno.
💥 Magonjwa ya moyo, kisukari, shinikizo la damu, uchovu wa mara kwa mara, matatizo ya figo – yote haya huwa hayaji kwa bahati mbaya, bali huwa ni matokeo ya mambo tuliyofanya kimya kimya kila siku.
🔔 Leo chukua hatua 3 rahisi kuweka akiba ya afya:
1. Kunywa glasi 8 za maji.
2. Tembea walau dakika 30.
3. Kula matunda au mboga angalau mara moja leo.
Afya njema si matokeo ya bahati, ni matokeo ya tabia zako za kila siku.
👑 King Mentorship Program – Tunaangaza Maisha Yako!
Unataka kujifunza zaidi kuhusu afya, nidhamu binafsi, na utambuzi wa ndani unaoleta mabadiliko ya kweli?
Jiunge na programu yetu leo na anza safari yako mpya!
📞 Mawasiliano: 0744 284 329
🌐 Blog: kingmentorshipprogram.blogspot.com
Comments
Post a Comment