Tatizo Siyo Connection... Tatizo Ni Thamani Yako!
Amani ya yake idumu kwako na kwa wale unaowapenda!
Leo, ningependa tuketi pamoja – si kwa muda mrefu, hata dakika mbili tatu za tafakari zinaweza kuwa zawadi kubwa kwako.
Kuna jambo moja ambalo watu wengi wamekosea kulielewa...
Connection si kitu cha kutafuta kwa pupa, ni kitu kinachovutwa! Na kinachovuta ni hadhi yako.
Hadhi yako ni ile thamani ya ndani unayoibeba na kuimwaga kwa wengine. Kama hadhi yako iko chini, utajikuta unaishi maisha ya kutegemea huruma, kukumbatia unafiki na kubembeleza nafasi – badala ya kuitwa kwenye nafasi kwa thamani yako mwenyewe.
"Hadhi yako ya ndani ndiyo inayoamua nani anavutwa kwenye maisha yako." - Emmanuel Samuel King'ung'e.
Watu wa maana huvutwa na watu wa maana.
Ukiwa wa kawaida, utavutwa na wa kawaida. Ukiwa chawa kwa fikra, utatumiwa kama chawa katika maisha.
Lakini ukiinuka na kuwa wa thamani – utaanza kuvuta viongozi, wasanii, wafanyabiashara, na watu wakubwa bila hata kuwaomba.
Kanuni za Ulimwengu Hazina Upendeleo
Ulimwengu huu unaendeshwa na KANUNI. Na moja ya kanuni hizo ni kanuni ya uvutano inayosema:
“Wewe ni kama sumaku, unavuta watu, matukio na fursa kulingana na kiwango cha fikra zako na hadhi yako ya ndani.”
Sasa jiulize:
Unaota kuunganishwa na watu wakubwa, lakini je, umejiandaa kuwa mtu mkubwa anayevutia fursa hizo?
Au unakazana tu kuonekana karibu na watu maarufu ilihali ndani yako una hofu, mashaka na huna msimamo?
Pandisha Thamani Yako – Badala ya Kuomba Connection
🔑 Anza kuwa mtu wa maono
🔑 Toa thamani halisi kwa watu
🔑 Jijenge kwa kujitolea, kujifunza na kujiendeleza kila siku
🔑 Kuwa mtu wa msimamo, si wa kujikomba kwa viongozi
Utakapoanza kuwa mtu wa tofauti, watu wa tofauti watakufuata. Na utakapoacha kuomba nafasi, nafasi zenyewe zitakuomba.
Mimi ni shahidi hai wa hili. Sijawahi kuomba nafasi kwa mtu yeyote maarufu – lakini tokea nianze kuendesha programu zangu za maendeleo ya watu, viongozi, na watu wakubwa wenye ushawishi wamekuwa wakinitafuta. Tunabadilishana mawazo, tunashirikiana – bila unafiki wala kujikomba.
Jiulize Sasa:
Ninatengeneza hadhi au natafuta huruma?
Natoa thamani au natafuta kubebwa?
Niko tayari kuvutia fursa au natafuta kubembelezwa?
Maisha yako yanaweza kugeuka! Lakini tu ikiwa utachukua hatua ya kubadili thamani yako ya ndani.
✍️ Kuhusu Mwandishi
Emmanuel Samuel King’ung’e ni mtaalamu wa utambuzi binafsi, mwandishi wa vitabu vya maendeleo binafsi, na mwanzilishi wa King Mentorship Program– programu mahiri inayowawezesha watu kugundua uwezo wao, kujitawala, na kujenga maisha ya mafanikio.
Kupitia maandiko yake, semina na mafunzo ya moja kwa moja, amewasaidia mamia ya watu kuamka kutoka usingizi wa maisha na kuanza safari ya mabadiliko halisi.
Jiunge na King Mentorship Program Leo!
Ikiwa unataka:
✅ Kuijenga thamani yako ya ndani
✅ Kuvutia watu wa maana katika maisha yako
✅ Kuweka msingi wa mafanikio yako ya kifedha, kiakili na kiroho
✅ Kujifunza kanuni za maisha zinazoleta matokeo ya kweli
Jiunge sasa na King Mentorship Program – tunaangaza maisha yako!
📞 Mawasiliano: 0744 284 329
🌐 Blog: kingmentorshipprogram.blogspot.com
💥 *Chukua Hatua Sasa – Usiendelee Kuishi Maisha ya Kukosa Thamani!
✉️ Nitafute kwenye inbox yako, tuanze safari ya kuijenga thamani yako ya kweli. Maisha yako mapya yanaanza na uamuzi mmoja – kuinuka!
Comments
Post a Comment