USICHEZE NA MAISHA: TUNAISHI MARA MOJA TU!


Kuna vitu unaweza kuvichezea na bado ukapata nafasi nyingine ya kuvirekebisha. Lakinimaisha si mojawapo ya vitu hivyo. Maisha ni zawadi ya kipekee — na unayo moja tu. 

Hakuna duka la maisha la akiba, hakuna bonasi ya maisha, na hakuna kurudia kama michezo ya video. Hili ulilonalo ndilo pekee.

Na kwa sababu hiyo, afya yako ndiyo rasilimali ya kwanza na ya msingi.

Bila afya, kila ndoto inakufa, kila malengo yanasimama, kila furaha hupotea. 

Hakuna mafanikio yanayozidi kuwa na afya bora — hata pesa haziwezi kuinunua ukishaiharibu.

Jiulize leo:
🟠 Unakula vyakula vyenye virutubisho au vya haraka haraka?

🟠 Unafanya mazoezi au unasubiri ugonjwa ukupeleke hospitali?

🟠 Unalala vya kutosha au unaishi kwa mihangaiko bila kupumzika?

🟠 Unafuatilia afya ya akili yako au unajipuuza kwa visingizio?

Huu ndio wakati wa kusema: Inatosha!
Jifunze kuipa afya yako nafasi ya kwanza. 

Si kwa ajili yako tu, bali kwa ajili ya familia yako, ndoto zako, na hatima yako. Kuishi kwa kujitunza si chaguo tena — ni WAJIBU.

“Usingoje ugonjwa ndio ukumbuke maana ya afya.”

Anza leo. Tembea, kunywa maji, kula vizuri, pumzika, cheka, tafakari — ishi kwa akili na kwa heshima ya maisha yako.

Usisubiri uanze kutunza afya yako siku utakapolazwa kitandani — anza sasa ukiwa na nguvu zako zote.

Kwa sababu, rafiki yangu...
Maisha haya unayo sasa, ni ya pekee — na hujayapewa mara mbili.

📲 Kwa mwongozo zaidi kuhusu afya, akili na mafanikio ya kweli, jiunge na King Mentorship Program kupitia 0744 284 329

✍️ Imeandikwa na Emmanuel Samuel King’ung’e – Mshauri wa Maisha na Mwalimu wa Utambuzi Binafsi.

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...