UNAISHI MAISHA HALISI AU MAISHA YA KUTUNGWA?
Tatizo kubwa la dunia ya leo ni hili:
WENGI WETU TUNAISHI MAISHA YASIYO HALISI KWENYE DUNIA HALISI!
Tumefundishwa mambo mengi yasiyo na msaada. Tumeaminishwa uongo, tukashikishwa maisha ya kubuni, tukasahaulishwa asili yetu. Tumeishi kwa habari za mbinguni bila kuelewa ukweli wa dunia.
Leo, kama hukuwahi kujua, upate kujua:
Dunia hii ndiyo asili yetu.
Ndiyo mama yetu.
Ndiyo msingi wa maisha yetu.
Babu zetu wa kale walijua – kwamba mtu wa kwanza aliumbwa hapa hapa duniani, kwa udongo uliokusanywa kutoka mabara yote saba. Alikuwa ni kielelezo cha dunia nzima – umbile halisi la mwanadamu.
Mwili wako umeundwa kwa madini yaliyopo duniani – Iron, calcium, magnesium, copper...
Yote yapo duniani – yote yapo mwilini mwako.
Sasa fikiria:
Unawezaje kuishi maisha halisi bila kuijua asili yako halisi?
Unawezaje kuongozwa na habari zisizo halisi, kwenye dunia halisi?
Hii ni kuikosesha nafsi yako haki ya kweli.
Ni kuikana roho yako.
Ni kuua utambulisho wako.
Ukweli huu hauhitaji kufunuliwa na roho.
Uumbaji si fumbo. Uumbaji ni kitu halisi!
Maisha yako siyo fumbo. Maisha yako ni halisi.
Mungu si kiumbe. Mungu ni uwepo wenye uwezo na nguvu usiotathminika kikawaida na vinavyoishi uliofanya vyenye uhai vikaishi.
Uwepo huu hauna wivu, hasira, chuki wala kisasi.
Ni sisi viumbe tunaojiumiza wenyewe – kwa kukosa kujua ukweli wa maisha, kwa kupotea mbali na chanzo chetu halisi: Mungu mwenye vyote.
Maelezo mengi yaliyotolewa kuhusu Mungu yamekuwa ya kufumba, si kufumbua.
Ukimwuliza mtu Mungu ni nini – hatajua!
Atakupa majina: Baba, Mfalme, Bwana, Yehova...
Lakini hataeleza kiini.
Kosa si kusoma hayo. Kosa ni kushindwa kuchanganua.
Na hapo ndipo faraja za uongo huanza:
Watu huishi maisha magumu, lakini wanabembeleza nafsi zao kwa faraja zisizo za kweli.
Kwa nje – wanatabasamu.
Lakini kwa ndani – wanavuja damu.
Wanadai wamekombolewa...
Lakini bado: Wanahangaika kupata mlo wa siku. Wanaishi kwa mkopo hadi pumzi ya mwisho. Wanategemea miujiza kuliko kuchukua hatua. Wanashindwa kufikiri nje ya mafundisho ya kiwindaji. Wanashiriki ibada lakini hawana amani. Wanakusanyika kila wiki lakini hawana mshikamano wa kweli.
Je, huu ndio ukombozi unaozungumziwa?
UKOMBOZI WA KWELI SI MANENO, NI MABADILIKO
Kama hujakombolewa katika fikra zako, hata uwe na maombi kiasi gani, bado utakuwa mtumwa.
Basi jiulize upya: Ukombozi wangu ni wa kweli au wa kufikirika?
Siku ya ukombozi wako si ile uliposoma tangazo la kiroho.
Siku ya ukombozi wako ni ile ulipoanza kuhoji, kutafuta, kujifunza, na kuamua kuishi katika kweli – hata kama inauma.
“Ukombozi wa kweli huanza pale mtu anapoamua kuamka!”
KWAKO wewe uliyekombolewa;
Je, huwa unaomba giza liingie? Huombi.
Je, huwa unaomba jua lichomoze? Huombi.
Je, huwa unaomba oksijeni unayoivuta? Huombi.
Basi tuliza kichwa.
Tafakari juu ya ukuu wa Mungu mwenye vyote.
Usitishwe na sauti za dini au biashara za kiroho.
Tafakari. Tambua. Amka.
Pole sana kwa maisha uliyolazimishwa kuyaishi.
Pole kwa kubadilishwa kuwa bidhaa ya kibiashara kwenye kila jambo – kuanzia maombi hadi miujiza.
Lakini bado kuna tumaini.
Ukielewa kwamba malaika na majini ni viumbe kama wewe – wenye maisha yao, kwenye sayari zao – utaanza kutofautisha hadithi za sayari zao na ukweli wa dunia yako.
Naam, ijue dunia yako.
Ijue sayari unayoishi.
Ijue asili yako.
Kwa sababu asili yako ndiyo kila kitu kwako.
Ndimi Emmanuel Samuel King’ung’e.
Ninakupenda, ninakujali – hata kama huwezi kuelewa upendo wangu kwako sasa.
Siku moja utaelewa.
Mawasiliano: 0744284329 kingmentorshipprogram.blogspot.com
Comments
Post a Comment