AHADI NI DENI

Babu wetu wa kale walituachia methali yenye uzito isiyo na mwisho wa maana: *“Ahadi ni deni.”* 

Walijua fika kuwa unapomwahidi mtu jambo, kwake hiyo ahadi inageuka kuwa hitaji. Ukishindwa kutimiza, unabaki umebeba deni.

Na mimi sitaki ukubaki na deni lolote lile, nilikuahidi kuwa nitatoa SoMo linalohusu sanaa ya kuazimia na kutimiza MALENGO. 

Nipo hapa kusawazisha akili zako na kuzipa utimamu ili uweze kufanikisha matokeo makubwa. 

Furaha yangu ni kukuona ukifanikiwa. Furaha yangu ni kushuhudia unapambana bila kikwazo mbele yako, ndiyo maana niko hapa kukupa taarifa sahihi na maarifa ya kweli ili yawe mwongozo KWAKO!

Unaona ilivyo raha? Naam, ni raha isiyo na kifani.

Sasa turudi kwenye maana ya lengo. Watu wengi wanaishi kwa matamanio, wakidhani ni malengo. 

Mara nyingi utawasikia wakisema: *“Siku moja nitakuwa tajiri, nitakuwa na maisha mazuri, nitamiliki mali nyingi.”* 

Hayo ni maneno mazuri, lakini ukweli mchungu ni huu: hayo si malengo, ni ndoto za mchana!

Ni mitazamo isiyo na mfumo wa utekelezaji.

Ndiyo maana watu wengi hujikuta wakisubiri kesho bora ambayo hawajaiandaa.

Kwenye fahamu zao huona kesho zao Nzuri sana, lakini hawajawahi kuandaa mchakato wa kufikia uzuri huo.

Kwa tafsri nyepeso lengo ni nia, tarajio, au kusudio analoliweka mtu ndani ya muda fulani.

Ili kupata maana kamili ya lengo, lazima tufafanue mambo matatu. 

Kwanza, lengo ni nini? Ni kile unachotaka kukamilisha. 

Pili, unakusudia nini? Hapa lazima ueleze njia, mfumo, au mchakato wa kufanikisha lengo lako. 

Tatu, baada ya muda gani? Ni muhimu kueleza kwa uwazi muda uliopanga ili lengo lako litimie. 

Hii ndiyo inakusaidia kuwa na nidhamu binafsi na kufanya tathmini ya maendeleo yako.

Mfano halisi: *Nataka kutengeneza milioni moja kila mwezi.* Hilo ni kusudio. (Lengo)

Lakini sasa angalia mchakato: 

Nitawekeza kiasi fulani cha fedha ili kiwe chanzo cha mapato.

Nitatafuta kazi ya pili ili kuongeza kipato.

Nitatumia fedha kwa nidhamu na kuweka akiba.

Nitaweka mkakati wa kila siku wa kutafuta wateja wapya ili kuongeza mauzo.

Mfano huu unaonyesha maana kamili ya lengo. Ukiweka lengo, lazima ueleze pia mchakato wa kulifikia. Bila mchakato, lengo hubaki kuwa tamanio tu.

Ni muhimu kufahamu kwamba mchakato ni mkubwa zaidi kuliko lengo lenyewe, kwa sababu ndilo daraja linalolifanya lengo litokee. 

Bila mchakato, lengo linabaki kuwa wazo. Kwa hiyo, kila unapoazimia, weka wazi hatua na njia utakazotumia.

Je, ungependa kuelewa zaidi kuhusu sanaa ya kuazimia na kutekeleza malengo kwa usahihi?

Wasiliana nami, nitakuongoza hatua kwa hatua kwa kukushirikisha yale ambayo mimi mwenyewe hutumia kupata matokeo makubwa.

*Ndimi,
Mbulwa King’ung’e*
📞 Mawasiliano: 0744 284 329

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...