Maisha Pasipo Kusudi: Je, Unaishi Sababu Yako Halisi ya Kuumbwa...?
Umeshawahi kujiuliza kwa nini uliumbwa? Ni kusudi gani hasa lililokuletea hapa duniani?
Tunaishi hapa duniani kwa mwendelezo. Maisha yetu siyo kitu kipya kilichojitokeza ghafla, bali ni sehemu ya safari ndefu ya maelfu ya miaka.
Wale waliotutangulia waliweka msingi, wakapita, na sasa sisi tumepewa nafasi ya kuendelea pale walipoishia. Dunia ni moja, kizazi ni kimoja kikikabidhi kijiti kwa kingine.
Lakini je, umewahi kujiuliza:
Ni kusudi lipi lililokufanya uwepo katika dunia hii, baada ya safari ndefu ya takribani miaka milioni 11 ya uwepo wa kiumbe MTU?
Kwanini wewe umezaliwa katika kizazi hiki na si kizazi kilichopita?
Kwanini ulipewa nafasi ya kupumua hewa hii, kuishi leo, na kushuhudia dunia hii katika hali yake ya sasa?
Hakuna kitu kilichotokea kwa bahati. Uwepo wako ni sehemu ya mpango mkubwa unaoendelea, mwendelezo wa historia ya viumbe watu. Lakini swali kubwa linabaki: Wewe upo kwa ajili ya lipi?
Wengine huishi maisha yao yote bila kugundua. Wanasoma, wanapata kazi, wanazeeka na kuondoka duniani bila kugusa sababu halisi iliyowaleta.
Wanaishi wakiendeleza tu yale ya mfumo, bila kugundua kiini cha wao kuwepo.
Ukweli ni mchungu: zaidi ya asilimia 80 ya watu duniani wanaishi bila kuishi kusudi la uumbaji wao.
Wengi wamefungwa na mifumo ya kijamii, kielimu na kimaisha ambayo imewatengea “kusudi dogo” lisilo lao.
Wameaminishwa kwamba kazi waliyoipata, shahada waliyosoma, au nafasi waliyopewa na mfumo, ndiyo sababu ya wao kuwepo duniani.
Lakini tafakari kidogo…
Je, kazi unayoifanya sasa ni matokeo ya kusudi lako la kweli, au ni matokeo ya mfumo uliokutengeneza?
Je, elimu uliyoisomea imekupeleka kwenye ndoto yako halisi, au imekupeleka kwenye kazi inayolisha tumbo tu?
Na je, ukiweka kando mfumo uliokufunga, moyo wako ungependa kufanya nini, kwa ajili yako na kwa ajili ya dunia?
Kwa bahati mbaya, wengi wamekamilisha masomo, wamepata vyeti vizuri na ajira nzuri, lakini bado wanatembea na utupu wa ndani kwa sababu hawajui kusudi la kweli la maisha yao.
Wamefanikiwa kwa nje, lakini wamefilisika kwa ndani.
Kitu cha msingi cha kutambua ni hiki: maisha pasipo kusudi si kitu.
Maisha yanapata maana yake tu pale unapogundua na kuishi kusudi lako halisi. Ukishapoteza kusudi lako, tayari umeshapoteza maana ya maisha.
Hakuna kitu cha kuogopesha kama kutumia miaka yako 40 kufanya kazi isiyo yako, kisha kugundua kwamba ulikuwa unaishi ndoto za mfumo na si ndoto zako.
Hakuna mateso makubwa kama kutumia nguvu zako katika jambo ambalo hukuzaliwa kulifanya.
Kila mmoja wetu aliyezaliwa ana kusudi.
Lakini kusudi hilo halipatikani kwa kufuata mkondo wa mfumo, bali kwa kusikia nafsi yako, kujitafakari na kutafuta kwa makini sababu ya wewe kuwepo duniani.
Mtu anapoligundua kusudi lake, hutembea na nguvu mpya, huishi maisha ya furaha na hubadilisha historia yake binafsi na ya wengine.
Swali langu kwako leo ni moja:
👉 Je, unajua kusudi lako halisi?
Kuhusu Mwandishi
Emmanuel Samuel King’ung’e ni mwandishi, mnasihi (mentor) na mwanzilishi wa King Mentorship Program.
Ametumia miaka kadhaa kuwasaidia vijana, wazazi, na watu wa rika mbalimbali kugundua kusudi la maisha yao, kuondoa mafundisho potofu, na kuishi kwa ubora wa hali ya juu.
Kupitia vitabu, semina na mafunzo yake, amekuwa mwanga wa mabadiliko kwa mamia ya watu wanaotafuta maana ya kweli ya maisha.
Mwito
Rafiki yangu, maisha yako ni ya thamani kubwa mno kuishi nje ya kusudi lako halisi.
Uamuzi wako wa leo unaweza kubadilisha historia ya kesho yako.
Jiunge na King Mentorship Program, program iliyoundwa mahsusi kukusaidia:
* Kugundua kusudi lako.
* Kuondoa vizuizi vya mfumo vilivyokufunga.
* Kujenga tabia za mafanikio.
* Na kuishi maisha yenye maana na matokeo makubwa.
👉 Huu ndio mwaliko wako wa kipekee kuanza safari ya kugundua kusudi lako la kweli.
Usiishi tena kusudi dogo—ishi kusudi kuu uliloumbwa nalo!
Mawasiliano:0744284329
Comments
Post a Comment