"Utu Kwanza, Fedha Baadaye: Siri Tulizosahau za Maisha...”
“Je, tunajua maana ya kuishi, au tumegeuza maisha kuwa mashindano ya pesa?”
Ukiona katika safari yako ya kuishi umefika hatua ya kujiangalia wewe tu, ukasahau kabisa kuhusu wengine, ujue bado hujajua maana ya maisha na bado hujaanza kuishi.
Kuishi siyo kula, siyo kulala, siyo kula bata, siyo kupumua tu - kuishi ni kuleta maana kwa wengine.
Maisha yakigeuka kuwa ubinafsi, hapo unakuwa mzigo, na badala ya kutoa pumzi ya uhai unakaba nafsi za wenzako.
Ukiona umekuwa ni mtu ambaye kila jambo lako linafungwa na maslahi binafsi ya kifedha kiasi kwamba uko tayari kuzuia wengine wasipige hatua, basi tambua ukweli huu mchungu: huna haja ya kuendelea kuishi kwa sababu unakwamisha maana halisi ya maisha.
Wengi wetu leo tumeshusha utu hadi kwenye kiwango cha thamani ya pesa.
Pesa ndiyo mizani ya ukubwa , pesa ndiyo kipimo cha mahusiano, pesa ndiyo kigezo cha nani anathaminiwa na nani anadharauliwa. Lakini kumbuka: maisha yalianza kabla ya pesa, na bado yataendelea hata pesa ikipotea.
Mpaka kufikia mwaka 2000, pesa ilikuwa na historia ya karibia miaka elfu kumi na sita tu, ilihali MTU ana historia ya zaidi ya milioni 15 toka aumbwe.
Ni jambo la juzi kabisa lililotuingiza kwenye mtego wa kuamini hatuwezi kuishi bila pesa.
Usishangae tukahesabu miaka kwa kalenda tuliyopewa, tukaambiwa sasa ni 2025, kumbe kwa hesabu za jadi za mwanzo wa utu, leo tungekuwa tunaishi kwenye mwaka wa 11,100,908 tangu mtu wa kwanza afe.
Utofautishe vizuri: siyo tangu mtu wa kwanza aumbwe, bali tangu afe. Hivyo, hii tunayoitukuza leo - pesa - ni kitu cha juzi sana, kilichotufanya tusahau utu wetu.
Na kwa tafsiri ya siri za kale, pesa haikubuniwa na Mungu.
Iliingizwa duniani na viumbe wa ulimwengu waliokuja na ajenda zao, wanaoitwa Konvodi kwa lugha ya Kibantu, lakini kisasa ni maarufu kama aliens.
Walileta mfumo huu kwa sababu moja: kutawala nafsi za watu kupitia tamaa.
Na leo tunaona matunda yake - dunia imejaa mikataba ya kificho, viongozi wanaoshirikiana na nguvu za giza, na jamii inayokubali hata mambo ya fedheha, kama vile kulazimishwa kukubali ushoga kwa mikataba ya kifedha, bila kuuliza utu wetu uko wapi.
Ukiwahi kusoma taratibu za kale, utashangaa. Kila noti unayoshika huenda imewahi kulipiwa kwa damu ya watu saba.
Ndiyo maana watu wanauana, wanaundana, wanajifanya walinzi wa fedha kwa gharama ya maisha ya wengine.
Ukitaka kuthibitisha hili, angalia mfano wa hivi karibuni: kashfa za kifedha kwenye mataifa yetu - watu wachache wanakula mabilioni kwa mikataba ya kifisadi huku maelfu wakifa hospitali bila dawa. Je, hiyo ndiyo maana ya pesa? Je, huo ndiyo uhai tunaoutukuza?
Tatizo kubwa siyo pesa, bali ujinga wa kutojua elimu yake. Ukikimbilia pesa bila elimu ya kifedha na bila kuzingatia utu, unajikuta mtumwa.
Hata ukiwa tajiri, ndani yako unakuwa maskini. Ndiyo maana tunaona watu wenye mabilioni wakijiua, wengine wakikimbilia mihadarati, wengine wakipoteza thamani zao - kwa sababu walipata pesa, lakini wakapoteza utu.
Mimi nimeyaona haya. Nimeona namna pesa inavyokuja kwa njia tofauti tofauti pale mtu anapoweka utu mbele.
Na nimegundua kuwa siyo rahisi kuvuta fedha iliyojazwa maovu ikiwa umejijenga kiutu kwanza.
Maisha yangu yamenifundisha: ukitanguliza utu, pesa itakufuata kwa mema. Lakini ukitanguliza pesa, utu utakukimbia, na mwisho wake hata pesa yenyewe itakutumia vibaya.
Ndugu zangu, leo tunaishi katika kizazi cha udanganyifu.
Wanaoshika maiki, wale wanaojitangaza kuwa watoa baraka, wengi wao si wema bali walaghai.
Wamepakaza maneno yao asali ya uongo ili kuwapumbaza watu. Hii ndiyo sababu lazima tuamke.
Tuelewe kwanza elimu hii: Konvodi hawakutumwa na Mungu, walikuja na mipango yao ya kutufanya watumwa wa mifumo ya kifedha.
Tukipuuza elimu ya utu, tutabaki tunauzana roho kwa pesa. Tutaendelea kuua ndoto za wengine, kuumiza maisha ya wengine, na kujifungia kwenye minyororo ya tamaa isiyo na mwisho.
Hivi kweli thamani ya fedha inalingana na maisha ya mtu? Hivi kweli tupo tayari kuuza utu wetu kwa pesa?
Ninawaambia kwa upendo na kwa uchungu: sisi watu tunahitaji elimu ya kiutu kwanza.
Tusijione kama adui kwa wengine, tusitafute njia za kukwamisha wengine, tusiuze utu wetu.
Ndiyo maana leo tunalalamika kuhusu wala rushwa, mafisadi na wahujumu uchumi - siyo kwa sababu wao wana nguvu kubwa kuliko sisi, bali kwa sababu sisi kama jamii tumekosa elimu ya kiutu. Tumekubali pesa itufundishe badala ya sisi kuitawala pesa.
Huu siyo mwito wa kawaida, huu ni wito wa kuamka. Tafakari, chukua hatua. Jiulize: je, utanufaika na pesa kwa kupoteza utu wako? Au utajijenga kiutu na bado ufanikiwe?
Mimi nimechagua njia ya pili. Nimechagua kuutukuza utu kwanza. Sipo radhi kudanganya mtu ili nipate pesa.
Sipo radhi kumnyang’anya mtu haki yake ili nifanikiwe. Nipo tayari kuishi kiutu na kupitia kufanya hivyo, nimeona fedha ikija kwangu kwa njia zisizo za uovu.
Ndiyo maana nimeanzisha King Mentorship Program. Hapa tunafundisha elimu ya kiutu, tunafundisha jinsi ya kuishi kwa maana, tunafundisha kujitambua na kujua kuwa maisha hayapimwi kwa kiwango cha pesa bali kwa thamani ya utu.
Ukijiunga nasi, utajua namna ya kuishi ukiwa mtu kamili - mtu anayeheshimika, mtu anayejua thamani ya utu wake, mtu anayejua namna ya kutumia pesa bila kugeuka mtumwa wake.
Ndugu zangu, ninawapenda. Ninatamani muijue elimu hii, ili tujenge kizazi kitakachothamini utu zaidi ya fedha.
Kizazi kitakachosema: “Ndiyo, natumia pesa, lakini mimi si mtumwa wa pesa. Mimi ni mtu, na utu wangu hauuzwi.”
Ndimi,
Mbulwa King’ung’e
📞 0744284329
Comments
Post a Comment