“Fikra Zako, Hatima Yako”


Je, unafahamu kwamba maisha yako yalivyo sasa ni kivuli cha fikra ulizoziruhusu jana? 

Kila hali unayoipitia leo - iwe ni mafanikio au changamoto - haijaja kwa bahati mbaya, imeanzia kwenye fikra ulizopanda akilini mwako. 

Fikra zako ndizo injini inayoratibu maisha yako. Kila unalolifikiri ni tendo la uundaji. 

Linapochukua nafasi moyoni mwako, dunia huanza kulipanga taratibu hadi liwe halisi. Ni suala la muda tu.

Huwezi kuvuta kitu ambacho hukukiwaza kwanza kupitia fikra zako.

Kila wazo ni kama mbegu. Ukipanda fikra za hofu, mavuno yake ni uoga na kukwama. 

Ukipanda fikra za kutokujiamini, mavuno yake ni kukosa nafasi nyingi maishani. 

Wewe ni kama sumaku inayoishi. Unavuta watu, matukio na hali vinavyoendana na fikra zinazoongoza maisha yako.

Mimi nimeona watu wanaojiambia mara kwa mara, “Sina bahati, maisha yangu ni magumu,” na matokeo yake kila wanalojaribu halifanikiwi kwa sababu tayari walishalipanda hilo wazo la kushindwa ndani yao.

Wengine hujiharibu kwa kusema: “Nitashindwa mtihani huu, sina akili ya kutosha,” na kweli huishia kushindwa kwa sababu akili ilikwishaamini mbegu hiyo ya kushindwa. 

Kuna wanaosema, “Sidhani kama nitaolewa,” au “Hakuna mtu atanipenda kwa dhati,” na matokeo yake maisha yao ya mapenzi hukwama kabisa kwa sababu walishajivuta wenyewe kwenye hali hiyo. 

Hata katika fedha, mtu akijiambia, “Mimi siwezi kuwa tajiri, pesa ni ngumu kupata,” basi hujikuta akivuta hali ngumu ya kifedha kila mara.

Nilipoanza kugundua kanuni hii, nilijiuliza: kwa nini maisha yangu yanakuwa namna yalivyo? Niliporudi nyuma nikaona wazi kabisa - kila nilichokuwa nakiwaza kiliishia kutokea. 

Mawazo yangu ya hofu yaliniletea hofu, mawazo ya kushindwa yaliniletea kushindwa. Ndipo nikajua kuwa ili kubadili maisha yangu, nilipaswa kubadili fikra zangu kwanza.

Maisha ni mduara wa fikra, vitendo, tabia na hatima. Kila kitu kinachoonekana sasa kilianzia kama wazo lisiloonekana. 

Ni rahisi kulalamika, “Nimekosa kazi kwa sababu hawakunipenda,” kumbe kiukweli hukupata hiyo kazi kwa sababu ulijiandaa kwa fikra za kushindwa hata kabla ya kuingia kwenye mahojiano.

Kuna siku nilimsikia mtu akisema, “Mimi nimeumbwa hivi tu, sitafanikiwa.” 

Nikatabasamu kwa uchungu, kwa sababu hakuna aliyeumbwa kushindwa. Sote tumepewa ubongo na uwezo wa kufikiri. Tofauti pekee ni aina ya fikra tunazozilea.

Kumbuka, wewe ni kama sumaku inayoishi. Ukifurahia fikra za furaha, utavuta furaha. Ukijaa fikra za huzuni, utavuta huzuni. Ukijaa fikra za uhaba, utavuta uhaba. Na ukijaa fikra za mafanikio, hakika utavuta mafanikio.

Niliwahi kuona maisha yangu yakikwama kwa sababu ya fikra nilizokuwa nazilea. 

Nilipoanza kubadili fikra, maisha yangu yakabadilika. Huo ndio ushahidi kwamba mtu anaweza kuunda upya hatima yake kwa kubadili anavyofikiria. 

Ndugu yangu, usijidanganye. Kama umechoka na hali ulizonazo sasa, usianze kwa kulaumu watu au mazingira. Angalia kwanza fikra zako. 

Usiendelee kujiambia, “Hali yangu ni mbaya, nitakufa maskini,” kwa sababu ni kama unapanda mbegu ya maskini moyoni mwako. 

Badala yake anza kujiambia, “Ninaweza kubadili maisha yangu. Ninaweza kufanikisha ndoto zangu.”

Leo hii, chukua dakika chache uanze kubadili fikra zako kwa makusudi. 

Jiulize: ni aina gani ya fikra zinazotawala maisha yangu kwa sasa? 

Je, ni fikra za kushindwa au za ushindi? Fikra za hofu au za matumaini? 

Kama umechoka na hali ulizonazo sasa, usianze kwa kulaumu mazingira, watu au historia. Badili fikra zako kwanza.

Chukua dakika 10 kila asubuhi kufikiria makusudi maisha unayotaka.

Andika fikra chanya tatu kila siku.

Lisha akili yako kwa kusoma vitabu na makala chanya.

Zunguka na watu wanaokutia nguvu.

Kumbuka, ili upate matokeo ambayo hukuwahi kuyapata, ni lazima ukubali kutengeneza fikra ambazo hukuwahi kuzitengeneza.

Kila unachopata maishani ni mwangwi wa fikra zako. Maisha si ajali, bali ni matokeo ya kile ulichopanda akilini. Hivyo, badili fikra zako, badili maisha yako.

Na hapa ndio mwisho wa makala hii rafiki yangu. Lakini ukweli ni kwamba safari yako haiwezi kuishia kwenye mistari michache uliyosoma sasa hivi. Ndiyo maana nakusihi kwa moyo wote -usiishie kusoma, chukua hatua.

Ndani ya King Mentorship Program nimeandaa kozi za Utambuzi Binafsi ambazo zitanishirikisha moja kwa moja na wewe. 

Tutakaa bega kwa bega, tukivunja kila imani potofu inayokuzuia, tukiziharibu fikra zinazokufunga, na tukijenga maisha yako mapya juu ya msingi wa uhalisia na uwezo wako wa ndani.

Nataka uone jinsi ulivyo na thamani kubwa kuliko hofu zako. Nataka ushuhudie macho yako yakifunguka kuona fursa ambazo hukuziona kwa miaka yote. Ndio maana nakualika rasmi leo: njoo tuanze safari hii pamoja.

Usisubiri tena - jiunge na King Mentorship Program sasa hivi, kwa sababu kesho yako bora inaanza na uamuzi unaoufanya sasa.

Ndimi Emmanuel Samuel King’ung’e; mwalimu, mwandishi, muelimishaji katika maendeleo binafsi, life coach and consultant*l.

Unaweza kuwasiliana nami kupitia WhatsApp:  +255744284329

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...