Jenga Mahusiano Yatakayodumu, Hakuna Kuachana Tena..
"Umewahi kujiuliza kwa nini mahusiano mengi yanavunjika, hata yale yanayoanza kwa moto mkali...?
Safari yangu ya kujibu swali hilo ilianza mwaka 2019. Nilipoingia kwenye mahusiano na mtu ambaye kwa kweli hakuwa na nafasi ya kuwa mwanandoa. Alijua kabisa hawezi kufika huko, lakini bado alitaka tu tuhusiane.
Kwa ustaarabu nilikubali. Nikajikuta nikiwa ndani ya mahusiano ambayo hayakuwa na malengo, na hata mbaya zaidi, nikaanza kuwekewa vizuizi - nikakatazwa kuingia kwenye mahusiano mengine yenye mwelekeo.
Nikajiuliza kimya kimya: “Kwa nini nibaki mahali ambapo hakuna mwisho mzuri? Kwa nini ninyimwe nafasi ya kuanzisha kitu cha kweli?”
Wakati huo nilikuwa kijana tu, mwenye ndoto nyingi lakini asiye na mwelekeo wa ndoa.
Nilijipa taswira ya maisha yangu - kijana handsome, mwenye urefu, nyusi zilizonyooka na nywele zilizokuwa zinasimama kwa wima.
Nilihisi nina kila sababu ya kuvutia, lakini ghafla nikajiona nikipoteza muda kwenye kitu kisicho na maana.
Nikachukua muda kutuliza akili. Nikaanza kujiuliza maswali mazito:
Kwa nini nipo kwenye mahusiano haya?
Malengo yangu ni nini?
Naona wapi mwisho wake?
Sikupata majibu.
Ndipo safari ya tafiti ilipoanza. Nilianza kuangalia mahusiano ya watu wengine.
Nikasikia maumivu yao, nikashuhudia vilio vyao, nikagundua wengi wanapitia machungu yale yale.
Nikatambua jambo moja: wengi wanaingia kwenye mahusiano bila malengo.
Wanaingia kwa ajili ya starehe.
Kwa ajili ya kusukuma siku.
Kwa ajili ya kuepuka upweke.
Na mara nyingine - kwa ajili ya majaribio.
Hapo ndipo nikagundua chanzo cha kuvunjika kwa mahusiano mengi. Wengi wanatumika tu kama majaribio, kama “field” ya mafunzo – kisha wanapotimiza kusudi la muda, wanatupwa.
Ndiyo maana niliamua kuandika mwongozo huu.
Sio kitabu kingine tu cha simulizi. Ni ramani ya maisha kwa yule anayetaka kujenga mahusiano yenye mwelekeo, yenye kupelekea ndoa imara na familia yenye furaha.
Ndani yake utakuta:
Aina za mahusiano (utajua upo kwenye lipi)
Sababu za mahusiano mengi kuvunjika
Athari za kuachana
Na zaidi ya yote - hatua kwa hatua jinsi ya kujenga mahusiano yatakayodumu
Kwa hiyo, kama umechoka na mahusiano ya maigizo…
Mahusiano yanayokupa maumivu badala ya furaha…
Mahusiano yasiyo na mwisho mzuri…
Basi kitabu hiki ni chako.
Nakuahidi ukisoma na kufanyia kazi kilichoandikwa humo, utajua kwa nini nimekiita:
Hakuna Kuachana Tena.
Kinakuja muda wowote kuanzia sasa.
Ikiwa unataka kuwa wa kwanza kupata nakala yako, andika neno “mwongozo” sasa hivi.
Comments
Post a Comment