Kuishi, Matumizi na Kujitibu..

Mwaka 2023 ulikuwa ni mwaka wa maumivu makali sana kwangu.

Hayakuwa maumivu ya mwili, bali ya ndani -maumivu ya nafsi na fikra. 

Na kila unapopitia maumivu, kumbuka ni ishara kwamba unapewa nafasi ya kufanikiwa; sharti ubadili mtazamo wako tu! 

Kupitia maumivu hayo nilitambua kuwa wapo wengi wanaoishi katika maumivu makali, lakini hawajui hata kama wamefungwa nayo.

Kisaikolojia, inasadikika kwamba watu wengi huteseka zaidi katika fikra zao kuliko kwenye uhalisia wa maisha. Nami nilipitia hali hiyo. 

Elimu nilokuwa nayo haikutosha. Nilijua namba na nadharia, lakini sikuwa na uwezo wa kufanya maisha yangu yawe tofauti - hata kutengeneza kipato kidogo ilikuwa ngumu. 

Nilihisi kuchoka kabisa, lakini uchovu ule ulikuwa mwanga ulionisukuma kutafuta mabadiliko.

Badala ya kukimbia maumivu, niliamua kuyakabili - na sasa ninayatumia kuanzisha safari ya kujitambua.

Nilitafuta ukweli wa kuishi - na nikaupata! Ukweli huo ulibadilisha huzuni yangu kuwa furaha, na udhaifu wangu kuwa nguvu.

Nikajua si haki kubaki nao peke yangu. Hii ni kwa sababu maisha ni kubadilishana uzoefu. 

Kile ninachojua kinaweza kukusaidia wewe, na ulichonacho kinaweza kunisaidia mimi. 

Lakini si kila mtu hupata nafasi ya kushirikishwa yale yanayoweza kumsaidia.

Hapo ndipo nilipojiuliza: “Naweza kuanzisha jukwaa gani la kusaidia watu wengi wajitambue na kuondoa minyororo ya fikra zinazowafunga?”

Ndipo wazo la King Mentorship Program likazaliwa - taasisi inayojikita katika Utambuzi Binafsi.

Sababu kubwa ni moja: watu wengi wanateseka kwa sababu hawajui misingi ya kuishi.

Tunaona wasomi wakifanya mambo yasiyo ya kiutu, yasiyo na maadili - kwa sababu hawajapata elimu ya utambuzi binafsi. Wanaishi kwa mshahara, lakini hawana utu. 

Wengine wana fedha, lakini ndani wamejaa maumivu.

Nimeona watu wengi wakiwa watumwa wa maamuzi ya wengine. 

Hawana sauti ya kusema "hapana" hata wanapojua jambo si sahihi. Maisha hayakumaanishwa yawe hivyo. 

Ukipoteza ukweli wa kuishi, utaishishwa na mfumo usiokupa furaha, amani, wala mafanikio ya kweli.

Ndiyo maana King Mentorship Program ipo. 

Ni mpango wa kukupa misingi ya kujitambua, kujiongoza, na kujitawala. 

Huu si mpango wa kushawishi akili, bali ni safari ya kujenga utu na kuishi maisha yenye kusudi.

Furaha yangu ni kuona Tanzania mpya yenye watu wanaojitambua, wanaoishi kusudi lao, na wanaoleta mabadiliko ya kweli.

Nipo tayari kuleta mabadiliko. Nipo tayari kuchochea mabadiliko. 

Kama na wewe ni mmoja wa wachache wanaoona dunia kwa jicho la tofauti, nakukaribisha kwenye Kozi za King Mentorship Program.

Kozi hizi huchukua miezi mitatu pekee - na ni safari ya kukuwezesha kujitambua, kujielewa, na kujisimamia.

Karibu tufanywe nuru kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Je, upo tayari kuanza safari hii ya mabadiliko?

Andika neno “Nipo Tayari" sasa ili kujiunga.

📞 Mawasiliano: 0744 284 329

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...