MAISHA NI KUCHAGUA, LAKINI SIYO KILA CHAGUO NI SAHIHI...!
Unachokipitia leo ni matokeo ya yale uliyowahi kuchagua jana.
Kuna nguvu katika kila uamuzi unaoufanya.
Maisha ni mlolongo wa machaguo. Kila MTU ana nafasi ya kuchagua, lakini si kila chaguo huzaa matokeo chanya.
Kuna machaguo tunayoyafanya kwa hiari, machaguo yanayotokana na mifumo tuliyokuta, na mengine tunayoyafanya kwa kushinikizwa, na habari mbaya ni kwamba, yote huzaa matokeo.
Kila siku unapokaa kimya, unachagua.
Unapoamua kubaki kwenye hali fulani, unachagua.
Unapoamua kufumba macho kwa sababu unaogopa ukweli, bado unachagua.
Na ukweli ni huu: Machaguo yako ndiyo yanayoandika hadithi ya maisha yako.
Hakuna kinachoitwa bahati mbaya. Kuna kupanga au kupangiwa.
Kuna kufikiri au kuachia wengine wakufikirie.
Na kila kimoja kina matokeo yake.
Huenda umewahi kuchagua kuingia kwenye mahusiano kwa haraka bila kuchunguza kwa kina, na sasa umebeba majeraha ambayo usingeyataka.
Huenda umewahi kuchagua kuridhika na kipato kidogo kwa sababu uliamini hakuna njia nyingine, na leo unaishi kwenye mzunguko ule ule wa changamoto.
Huenda umewahi kuchagua kunyamaza wakati moyo wako ulitaka kupaza sauti - na sasa unajilaumu kimya kimya.
Ukichagua kuishi maisha ya kulalamika bila kuchukua hatua, utabaki katika hali hiyo hadi siku utakayofanya chaguo jipya.
Ukichagua kujidharau, kujiona hufai, utabaki kwenye kivuli hicho maisha yako yote.
Machaguo ndiyo mizizi ya matokeo.
Ukipanda woga, utakua ukosefu wa furaha.
Ukipanda ujasiri, utavuna uhuru.
Ukipanda utambuzi, utavuna mafanikio.
Ninayasema haya kwa sababu nguvu ya machaguo ndiyo chanzo cha matokeo yetu.
Ni rahisi kulaumu mfumo, watu au mazingira - lakini kumbuka, una Akili Timamu.
Naam,a akili timamu IPO kukusaidia wewe kiumbe MTU katika kufanya uchanganuzi kwenye machaguo Yako.
Itumie. Iamrishe. Iweke kazini. Usiifubaishe!
Usiishi kama kondoo, bali kama MTU mwenye utambuzi.
Usiruhusu hisia zikuongoze; zithamini, lakini zitawale.
Fanya maamuzi yako kwa kuona mbali - fikiria matokeo ya muda mfupi na muda mrefu.
Badala ya kulalamika, jifunze mbinu mpya za kujikwamua.
Badala ya kushinikizwa, tafuta uhuru wa kiroho, kiakili na kifedha.
Badala ya kusema “maisha yamenibana,” sema “ninaanza kubadilisha machaguo yangu.”
Badala ya kusema “sina bahati,” sema “sina mipango sahihi, lakini naianza leo.”
Badala ya kusema “wananizuia,” sema “nimeamua kujikomboa.”
Mimi nimechagua kuishi kwa utambuzi, kufikiri kwa kina na kupanga kwa uangalifu.
Machaguo yangu yamenifanya niwe hivi nilivyo leo.
Najivunia mimi. Najivunia safari yangu. Najivunia machaguo yangu.
Na wewe je, machaguo yako yamekuletea nini maishani mwako?
Ikiwa ungependa kujifunza zaidi kuhusu sanaa ya kufanya maamuzi yenye tija na jinsi ya kuyageuza machaguo yako kuwa matokeo bora -
jiunge na King Mentorship Program leo.
Hapa utapata mwongozo kamili wa kufikiri, kupanga, na kufanya maamuzi yatakayobadilisha maisha yako milele.
📞 Mawasiliano: 0744 284 329
Ndimi Mbulwa King’ung’e
Founder & Mentor - King Mentorship Program
Comments
Post a Comment