Maisha, Roho, na Elimu: Sababu ya Kila Changamoto...

Leo nitatoa somo gumu; kama huwa hupendi kuichosha akili yako, usisome. 

Lakini kama unataka kuujua ukweli na kuishi maisha yenye maana, fuatilia somo hili kwa makini.

Maisha yetu ni mwendelezo. Kuna watu waliishi kabla yetu, na kila tukio lililotokea kabla yetu linaathiri maisha yetu ya sasa. 

Matatizo mengi tunayokumbana nayo ni matokeo ya kuundwa; hapo awali hayakuwepo. 

Hii inaonyesha wazi kwamba changamoto nyingi si za kiasili, bali zimeundwa au zimeanzishwa kwa namna fulani katika historia zilizoibuka kati kati ya uishi na si zinachambua mwanzo wa uishi! 

Babu zetu walielewa maisha ya kiroho kwa kina. Hawakuwa wakemeaji, hawakuwa watu wa kupepuliwa na mapepo, wala hawakuishi kwa hofu za nguvu zisizoelezeka. 

Badala yake, maisha yao yalikuwa na ufasaha, kwa sababu walikuwa na elimu ya kiutu - yaani, walijua tabia za roho, nguvu za asili, na jinsi ya kushughulikia changamoto bila kupotea kimaisha.

Elimu ya kiutu iliwapa babu zetu uwezo wa kutambua ni roho zipi za kweli, zipi ni zisizo za kiutu, na jinsi ya kuishi kwa maana bila kuingizwa na hofu au dhana zisizo na mantiki. 

Hii ndiyo sababu mara nyingi walikuwa  na hekima ya kweli, na maisha yao yalikuwa na mwendelezo wa amani na mafanikio.

Maisha yalivyoendelea, ukengeufu ukaanza kuingia. Viumbe vilivyotokea ulimwenguni vikaingiza agenda zao. 

Watu wa Ulaya walikuwa wa kwanza kupokea miongozo hiyo, na hivyo kuathirika moja kwa moja. Baadaye, wakaona si vibaya kueneza na kuleta masuala haya Afrika.

Ndani yetu, wapo watu waliopangwa na kugeuzwa kuwa mawakala wa viumbe hivyo ili kutawala akili za watu na kujinufaisha kupitia wengine. 

Hawa wanatumia nguvu, mtindo wa maneno, au nafasi zao kuendeleza malengo yao binafsi, mara nyingi kwa kuathiri wengine bila wao kujua.

Lakini pia, ndani yetu wapo wale wanaopambana kutatua matatizo hayo. Hawa ni watu wa kweli, ambao wanatumia akili, hekima, na uthubutu kushughulikia changamoto. 

Hata hivyo, wapo wengine ambao wako tayari kuishi ndani ya matatizo na kuyaendeleza bila kujitahidi kuyatatua, na hivyo maisha yao na ya watu waliowazunguka hubakia kwenye mizunguko ya changamoto. Hawa ndiyo huitwa makahokwa😂😂

Moja ya changamoto kubwa inayokabili watu wengi na kuwapotosha vichwa ni changamoto ya kiroho.

Zipo roho nyingi lakini leo nitachambua roho zinazowavuruga watu!

Roho za kiutu - hizi ni roho za watu, sehemu ya vizazi vyako, ambazo ni chimbuko la kuzaliwa kwako. Roho hizi hubeba tabia na mwenendo kama wa mtu aliyeishi.

Mara nyingi, roho hizi hukemewa pale mtu anaposhindwa kuelewa asili yake. 

Matokeo yake, mtu hukataa utu wake na hujaribu kuingiza nguvu zisizo sahihi. Hatimaye, hujikuta akiharibikiwa kwa sababu baadhi ya roho hizi zilikufa kichamungu - yaani, zikiwa na utambuzi na uelewa wa kweli wa maisha.


Roho za majini, malaika, aliens, na viumbe vingine -  ni viumbe vilivyowazunguka watu kiakili,kwa kuwatoa kwenye elimu ya kiutu. 

Roho hizi zimesababisha mkanganyiko mkubwa kwa wengi; zimewapoteza watu na kuwaunda ndani ya kitanzi kikubwa cha matatizo. 

Watu wameharibika kimaisha kwa kushika na kuifuata agenda zinazotokana na mwongozo wa viumbe hawa, na hivyo kupoteza uelewa wa asili yao, utu wao, na maana ya maisha.

Shida hujitokeza pale mtu anapotokewa na roho ya kiutu - roho za kizazi chake ambazo ndizo msingi wa uwepo wake. Bila roho hizo, yeye asingekuwepo. 

Lakini badala ya kusikiliza shauri na kuelewa ujumbe, mtu huyo huanza kukemea kile asichokijua.

Hatimaye anakataa utu wake mwenyewe, na kujaribu kupandisha roho zisizo za kiutu. 

Wazazi wanawatokea, mnawapuuza, mnashindwa kupokea mashauri yao yanayolenga kuwanufaisha matokeo yaje, na mnajikuta mko kwenye kitanzi cha changamoto. 

Maisha yenu yanageuka na kuwa kama ngoma: leo unapigwa tukio hili, kesho linakuja lile.

Mtu hujikuta akizunguka kutoka imani moja kwenda nyingine, kila moja ikiwa chini ya mwongozo wa viumbe hivyo, akitafuta msaada asiupate 

Mwishowe huambiwa: “Huo ni mzimu wa fulani, ukemee.” Lakini hata baada ya kukemea, haoni matokeo. 

Na akishindwa kuwa makini, anaweza hata kuangamia mwenyewe kwa sababu ya hasira kubwa zinazomzunguka - kwa kuwa amekataa shauri la mzimu unaomtokea.

Mtu huamua kwenda kwa mganga, akitarajia kupata suluhisho la tatizo lake. Hata hivyo, mganga hushughulikia jambo hilo kwa taratibu zisizoelezeka. Kisha hukutabiria kwamba huo ni mzimu wa fulani, lakini hakuelezi mzimu huo unataka nini.

Matokeo yake ni kwamba mtu hujikuta akichoka, akihangaika zaidi, akiishi kwa hofu, na hatimaye kuharibikiwa zaidi kimaisha.

Kwa hiyo, katika safari ya mapito yako, unajikuta unaambiwa “rudi kwenye ukoo wenu, kafanye taratibu fulani ili mambo yako yanyooke.” 

Lakini kinachoumiza ni kwamba huelekezwi taratibu zipi hizo, zinafanyikaje, na kwa nini.

Hapo ndipo ugumu mkubwa unapoanza - unaachwa na mkanganyiko, unaishi kwenye giza la kutokuwa na uhakika. 

Badala ya kupata mwanga na amani, unajikuta unazidi kuingiwa na hofu, mashaka, na hata kujiona kama mtu anayechezea hatima yake.

Kama hatujui, mizimu ni roho zilizokufa kichamungu; zilijua ukweli wa kuishi, na kwa Mungu ni roho fasaha. Hazitafutwa na uishi wa milele.

Mizuka ni roho za watenda mabaya (watu waliojikengeusha). Waganga na wachawi hutumia mizuka kufanya machawi yao na upumbavu wao na kuwaharibia wengine maisha!

Watu wengi hawaelewi kwamba pale wanapokimbilia hospitali, wanashughulikiwa tabia za mwili tu, si jambo la kiroho. 

Wanapimwa, hawaoni ugonjwa, kwa sababu tatizo si la mwili bali ni la kiroho. 

Matokeo yake, kwa kukosa maana, wanasema: “Mungu anapaswa kuingilia.” Lakini Mungu hakubahatisha maisha yetu; kila tukio lina mantiki.

Kubahatisha kunatokea pale mtu anapokosa kuchanganua roho, au anapokosa elimu ya kiroho.

Leo jiulize: Ni nini chanzo cha roho zinazokemewa? Tutaendelea kuzikemea mpaka lini?

Haya mambo yanahitaji elimu ya kweli. Alichokifanya Mungu kinaeleweka na ni kikubwa Sana! MUNGU si jambo dogo ndugu zangu!

Yote unayopitia ni matokeo ya ukosefu wa kutambua roho.

Hitimisho:

Maisha si ya bahati tu; ni mwendelezo unaohitaji utambuzi wa kina.

Changamoto nyingi ni matokeo ya historia, roho, na uelewa mdogo wa mtu.

Elimu ya kiroho ni muhimu zaidi ya hofu na tabia zisizo na mantiki.

Kila tukio lina mantiki, na Mungu hakubahatisha; tunapaswa kuelewa tabia ya roho na kuchukua hatua sahihi.

Kwa wale wanaotaka kuishi maisha yenye maana, utambuzi wa kiroho, historia ya mtu, na mantiki ya maisha ni nguzo kubwa za mafanikio.

Ndimi mbulwa king'ung'e 
Mawasiliano: 0744284329

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...