MUNGU SI UPENDELEO: Fahamu Uhalisia wa Maisha na Sababu Zake.
Kuna misemo ambayo mtu, ukimuelewa Mungu kwa usahihi, utaacha kabisa kuitumia, kwa sababu misemo hiyo humweka Mungu katika taswira ya viumbe vinavyoishi.
Mungu hana upendeleo. Aliviumba viumbe vyake vyote kwa hekima na akavipa akili timamu iwe mwongozo katika maisha yao.
Kwa hiyo, mtu kupata jambo fulani au kuneemeka kwa namna fulani haimaanishi kuwa Mungu amempendelea zaidi kuliko mwingine.
Bali ni kwa sababu zipo sababu za kuishi zinazomzunguka kila mtu ambazo ndizo husababisha kufanikisha au kukutana na fursa fulani.
Sababu hizo si Mungu, wala haziko kwa Mungu; zipo kwenye mfumo wa maisha na ndani ya mtu mwenyewe. Kila mtu huzungukwa na sababu takribani 77 zinazochochea matokeo yake ya maisha.
Hivyo basi, unapokutana na fursa, bahati, au matokeo mazuri, si kwamba Mungu amekupendelea, bali ni kwamba sababu hizo zimekutana kwa wakati sahihi katika maisha yako.
Lakini wengi hawajui hilo. Mtu akinunua gari husema, “Ni Mungu amenipendelea.” Akiwa amepata kazi husema, “Ni Mungu amefungua milango.”
Akinusurika ajali husema, “Mungu alinilinda.” Hata akiwa amechelewa kufa, atasema, “Mungu ameniongezea muda.”
Misemo hii inaonekana yenye heshima, lakini kwa undani inamweka Mungu katika taswira ya kiumbe anayeamua kwa upendeleo nani apate nini na nani anyimwe.
Mtu kusema “Mungu kampendelea fulani” ni kumweka Mungu katika mfumo wa hisia za vinavyoishi, kwa sababu upendeleo ni sifa ya viumbe, si kanuni ya uumbaji.
Matokeo yake, watu wengi huanza kujenga chuki kwa Mungu, wakihisi kama wameachwa au kusahauliwa.
Ndiyo maana wengine husema, “Mungu mbona umenisahau?” kumbe Mungu hajamsahau mtu yeyote; tatizo ni kutokujua mfumo wa uumbaji na jinsi mambo yanavyofanya kazi katika uhalisia.
Hivyo ndugu yangu, haipendezi kumhusisha Mungu na mashindano ya upendeleo.
Mungu haingii kwenye mlinganyo wa nani apendelewe na nani asipendelewe. Muujiza wake ni mfumo kamili, unaofanya kazi kwa usawa bila ubaguzi.
Kuna kitu kinachoitwa Neema. Neema haijatengezwa kwa kundi maalum la watu.
Imetolewa kwa kila kinachoishi - kiwe kimepotea, kiwe kipumbavu, kiwe cha kidini au la.
Vyote hivi huneemeka kwa uwezo wa Mungu bila kupendelewa.
Lakini pia, wako wale wanaomsingizia Mungu kila jambo. Kikitokea kitu kibaya, husema, “Ni mapenzi ya Mungu.”
Mtu akifukuzwa kazi, atasema, “Ni Mungu kapanga.” Akiachwa kwenye mahusiano, atasema, “Labda Mungu hakutaka tuwe pamoja.”
Hata akifeli mtihani, atasema, “Pengine Mungu ana mpango mwingine.”
Kwa mtazamo wa ndani, hizi zote ni njia za kuficha ukweli kwamba hatutaki kukubali wajibu wa matendo yetu.
Kwa mtazamo wa uumbaji, Mungu alishaweka mfumo kamili wa maisha - mfumo wa kanuni, matokeo, na usawa.
Mungu aliumba maisha kwa wema na amani. Kiumbe kinapoacha mema na kukumbatia mabaya, hiyo siyo kazi ya Mungu, bali ni matokeo ya uamuzi wa kiumbe mwenyewe.
Kiumbe kinapofanya maovu, kinapoharibu uhai wa vingine au kuleta mateso, hicho hakihusiani na makusudi ya Mungu.
Hapo ndipo mimi hukataa kabisa msemo “Yote ni mapenzi ya Mungu.” Kwa sababu Mungu ni mwenye vyote na si mwenye yote, tena huyo MUNGU hajawahi kusababisha shari kwa kiumbe chochote.
Mtu akifa kwa ajali, badala ya kuchunguza chanzo cha ajali - kama uzembe wa dereva, ubovu wa gari, au kukiuka sheria za barabarani - husema, “Mungu kamchukua.”
Mtu akiumwa kwa muda mrefu kwa sababu ya kutokujali afya, atasema, “Ni Mungu ananijaribu.”
Kwa namna hii, tunamgeuza Mungu kuwa chanzo cha kila uchafu, kila huzuni, kila hasara, na kila kilichoharibika, ilihali yeye si chanzo cha hayo.
Mara nyingi nikitafakari kwa kina, huona maelezo mengi yanayomhusu Mungu hayajajitosheleza. Pengine ndiyo maana Mungu hufananishwa na vinavyoishi, kwa sababu tumempa sifa ambazo ni za viumbe.
Kama Mungu ni Roho, basi tujiulize: ni roho ya aina gani?
Roho ziliandaliwa na MUNGU Mwenyewe kupitia muujiza wake uitwao alotro jabaz kwa ajili ya viumbe hai ili zibebe kumbukumbu za matukio.
Mara tu kiumbe anapofikia ukomo wa maisha yake, hufa, na roho yake huondoka na kumbukumbu zote za alichowahi kuwa, alichofanya, na alichopitia.
Roho hizo hubeba sifa za kiutu au za kiumbe husika, hivyo ni rahisi zikimtokea mtu zikaendelea kudhihirisha tabia au mitazamo ya yule aliyewahi kuishi kabla.
Kwa hiyo, roho ikimtokea mtu, huweza kuonekana kama ina upendeleo au mwelekeo fulani - si kwa sababu ni Mungu, bali kwa sababu ni roho iliyowahi kuishi na kubeba historia yake.
Hapa Duniani hususani katika anga iitwayo zugril galayo na maalumu nunu, zipo roho nyingi: za majini, za malaika, za dragons, za aliens, na viumbe vingine ambavyo vilishawahi kuishi.
Kwa kuwa roho hizi zilibeba sifa za vilivyokuwa, zikimtokea mtu, huja na vuli ya kiroho inayoendana na asili yao.
Roho hizi zinaonekana kuwa na upendeleo, kwa sababu zinatambua maisha ya viumbe na zinawajuwa baadhi ya watu.
Hivyo basi, kupendelea huyu na kumwacha huyu inawezekana kabisa - si kwa sababu Mungu amemchagua, bali kwa sababu roho hizo zinataka kutimiza misheni fulani kupitia MTU huyo.
Wengi hushindwa kuelewa hali hii kwa sababu hawaitambui maana halisi ya “roho.”
Wanapomuona mtu akipata fursa fulani au kuepuka hatari, mara nyingi husema, “Ni Mungu amemchagua.”
Na hapo ndipo hata Mungu alipoitwa “Roho,” ilihali yeye, kwa muujiza wake mkuu, ndiye aliyewaandalia viumbe roho zao - akivipa kila kiumbe nguvu ya kuishi kulingana na mfumo wa uumbaji.
Kwa hiyo, swali langu la tafakari kwako ni hili:
KWAKO MUNGU NI NANI?
Ndimi,
Mbulwa King’ung’e
Mawasiliano: 0744284329
Comments
Post a Comment