*“Nilifuata Ramani ya Jamii Nikabaki Mtupu -Kisha Nikagundua Siri ya Kweli ya Mafanikio...*”


Je, umewahi kufuata ramani ya maisha uliyopangiwa na jamii- ukasoma kwa bidii, ukafaulu mitihani, ukahitimu chuo - halafu mwisho wa siku ukajikuta umepotea, bila mwelekeo, ukiwa na cheti mkononi lakini moyo wako hauna dira?

Hiyo ndiyo ilikuwa safari yangu.

Nilizaliwa kwenye familia iliyokuwa na falsafa moja kubwa: “Soma kwa bidii, ufaulu, upate ajira serikalini, uishi kwa mshahara na ufurahie pensheni baada ya kustaafu.”

Nikaiamini ramani hiyo, nikajitupa kwa nguvu, nikasahau kabisa vipaji vyangu. 

Nilipokuwa sekondari nilikuwa nikiandika nyimbo, kutunga maigizo ya kuelimisha, hata kuandika makala. Na nilikuwa naigiza..

Nakumbuka siku ya mahafali nilirap mbele ya hadhira na mama yangu hakusadiki kwamba mwanae ndiye aliyekuwa pale akitupia mistari.

Lakini yote hayo niliyaweka pembeni, nikakimbilia kufuata ramani ya jamii.

Kidato cha nne nikafaulu. Kidato cha sita nikafaulu. Chuo kikubwa nikahitimu kwa alama nzuri kabisa. 

Lakini nilipoingia kwenye hatua ya mwisho - ajira - nikakutana na ukuta. Nilipiga hodi kila kona, lakini nafsi yangu iligoma. 

Nilihisi kama nimefungwa. Wengi walinipongeza kwa kuhitimu, lakini ndani yangu nilihisi sifahamu chochote. Nikiwa na shahada mkononi niliona bado niko mtupu moyoni.

Hapo ndipo maswali makali yakaanza kugonga katika kichwa changu kama nyundo. Nikajiuliza :

“Nisingesomea hii fani, ningekuwa nani?”

“Kwa nini wapo waliokomea darasa la saba lakini leo wanaishi ndoto zao?”

“Kwanini kijana tuliyesoma naye, ambaye hakuwa na ufaulu, sasa ana gari lake mwenyewe wakati mimi nimesalia na matumaini tupu?”

Hapo ndipo akili yangu ilianza kuhamia upande mwingine. Nikaacha kuamini ramani ya ajira pekee, nikaamua kuutafuta ukweli. 

Maumivu ya kuona wengine wakipiga hatua wakati mimi nimekwama yakanifanya nibadili mwelekeo. Nilihamisha akili yangu kutoka kwenye ndoto ya ajira na kuanza kutafuta majibu mapya.

Nikajitupa kusoma vitabu:

Vitabu vya utambuzi binafsi- vilinisaidia nijitambue, hatimaye nikaweza kujiongoza, kujitawala na kujisimamia.

Vitabu vya saikolojia- vilinifanya kuwa mshauri na mentor.

Vitabu vya uchumi na fedha - vilinifungua macho kuhusu saikolojia ya pesa, uwekezaji na biashara.

Na hapo nikagundua kitu - maarifa niliyoyapata ni hazina, na hazina hii inaweza kugeuzwa kuwa huduma. 

Nikakumbuka tena mapenzi yangu ya zamani ya kuandika, ikumbukwe huwa haupendi vitu bila sababu, nikarudi kwenye ndoto yangu ya enzi za sekondari nza kuandika na kufundisha.

Nikatambua pia kuwa uongozi ulikuwa ndani yangu tangu zamani. Wakati wa sekondari marafiki waliniambia, “Tukikaa na wewe tunajikuta tunafanya maamuzi sahihi tu.”

Nilikuwa sielewi, kumbe walikuwa wanaona kipawa ambacho mimi nilikizima.

Ndipo mwaka 2023 nikaanzisha King Mentorship Program. Na tangu siku hiyo imekuwa mwanga kwa wengi waliopoteza dira kama nilivyopotea mimi.

King ni kifupi cha jina langu la ukoo - King’ung’e. 

Mentorship ni mwongozo wa maisha. 

Program ni mafundisho ya muda mfupi -huduma hii hudumu miezi mitatu tu. Hivyo basi, King Mentorship Program ni safari ya miezi mitatu ya kukujenga upya, kukufanya ujitambue, ujisimamie na ujitawale.

Naamini kitu kimoja ambacho leo hii nikiseme kwa sauti kubwa: Utambuzi binafsi ndiyo nguzo ya mafanikio ya kweli.

Bila utambuzi binafsi, utageuka kuwa mtumwa wa mawazo ya wengine. Lakini unapojitambua, hakuna mtu wala mfumo utakaoweza kuzima mwanga wako.

Kwa hiyo, ninakualika. Ikiwa unahisi unakabiliana na mapito kama niliyopitia mimi - umekwama, unatafuta dira, unataka kubadilisha maisha yako - karibu kwenye kozi zangu. 

Nitakupa uzoefu wangu, nitakuongoza hatua kwa hatua, na utajengwa upya uwe mtu ambaye hujawahi kufikiria unaweza kuwa.

Hii ndiyo zawadi ya King Mentorship Program.
👉 Ukiwa tayari, andika neno “Nipo Tayari” ili upate maelekezo.

Mawasiliano: 074428484329

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...