Thamani
Katika ulimwengu huu mpana sana uliojaa kelele nyingi na fujo za kutosha!
Lipo neno moja ambalo linachukuliwa kikawaida sana lakini lina MAANA kubwa kwa wale wanaolipa mashiko!
Neno Hilo ni thamani kwenye kamusi lipo na kwenye akili za Watu lipo lakini limepoteza maana yake ya msingi.
Katika zama hizi thamani ya kiumbe MTU inapimwa na kupitia ujuzi wake na ule uwezo wa kufanya mambo yatokee!
Ieleweke kwamba si kila ujuzi ni wa thamani kuna ujuzi ambao MTU anapewa ili azubaishwe kiakili baada ya hapo yule aliyempa ujuzi ndiye anakuwa mtawala huku aliyepokea ujuzi akibaki chini!
MTU huyu asipoamua kutafuta ukweli wa kuishi atabaki na thamani ndogo sana ilihali NDANI yake ana hazina kubwa sana isiyochimbwa.
Ukija kwenye bara letu la arikasi/ Afrika ni dhahiri kwamba wanatengenezwa kuwa na thamani sawa ijapokuwa hawana hazina sawa NDANI Yao.
Na wakihitimu mafunzo wanaonekana ni sawa na hata wakipata KAZI kuna kiwango cha mshahara kimoja!
Kwa MAANA hiyo kuna thamani ambayo mfumo unakupangia.
Ndiyo MAANA kuna baadhi ya kada huwa inadharaulika sana hususani katika nchi za Africa!
Hii si nyingine ni kada ya ualimu, kwanini, kwa sababu ni wengi na wanachukuliwa kikawaida sana kutokana mfumo uliowatengeneza!
Mnapopitishwa kwenye mfumo mmoja mnafanywa kuwa kitu kimoja na kuanza kuchukuliwa kirahisi!
Hapa ndipo wengi wanageuzwa na kuwa watumwa, kwa kushangilia kila jambo, kupongeza kila jambo kwa sababu thamani yao ni ya chini kimfumo na si kiuhalisia!
Wanatumwa kufanya mabaya na uharibifu kwa maisha ya wenzao kwa sababu ya thamani ya kupandikizwa!
Wanawadhuru wengi kwa kuwafanya mabaya kwa sababu hawatambui thamani zao na thamani za hao wanaowadhuru!
Ndugu zangu thamani ni kitu cha msingi sana katika uishi wetu.
Sasa leo kaa Chini halafu jiulize ungekuwa hujapitishwa kwenye Mfumo unaokupangia thamani ungekuwa na thamani Gani?
Na ingetokea umepewa nafasi uanze Upya ni thamani gani ungeitengeneza?
Naam nayasema haya si uzushi, ni ukweli!
Tumetolewa kwenye misingi ya kiutu kwa sababu ya kufichwa thamani Zetu!
Badala ya kufundisha kuona NDANI tumefundishwa kuona nje!
Wengi tumekuwa na uoga, hatuwezi kujaribu mambo mapya kwa kuwa thamani Zetu hazitupi kibali!
Lakini tumaini bado lipo, bado tuna nafasi ya kutengeneza kizazi hiki!
Na hii Ndiyo sababu ya King Mentorship Program!
Yap ipo ili kuongeza thamani kwa kizazi hiki ili tupate kizazi kinachojielewa!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e
Comments
Post a Comment