Tofauti Kati ya Msomi, Mnukuzi, na Mtu Aliyeelimika...

Kuna watu baadhi ya watu wanaodhani ya kwamba, kuwa msomi ni sawa na kuwa na elimu, lakini ukweli ni kwamba si kila mwenye elimu ni msomi, na si kila msomi ameelimika kweli. 

Wapo waliojaa vyeti lakini vichwa vyao havina tafakuri; na wapo wasiokuwa na vyeti lakini fikra zao zimefunguka zaidi ya wale waliofika vyuoni.

Watu wengi  hudhani kuelimika ni sawa na kujua kusoma na kuandika. Lakini ukweli wa mambo ni kwamba maarifa ya kweli hayapimwi kwa vyeti, bali kwa namna mtu anavyotumia akili yake kufikiri, kutafakari, na kutenda.

Msomi ni nani?

Msomi ni mtu anayefikiri kwa kina, anayechambua mambo, anayetafuta maana iliyo ndani ya maana. 

Msomi si yule mwenye stashahada, bali ni yule anayeweza kuhoji, kuchambua, na kufikia hitimisho lenye maana.

Msomi hachukui kila kitu kama kilivyo - anahoji, anachunguza, anapima, kisha anatengeneza mtazamo wake wa aina yake.

Msomi si lazima awe na shahada; bali lazima awe na mtazamo wa tafakuri.

Msomi ni yule ambaye anaweza kuona mbali zaidi ya macho, kusikia zaidi ya masikio, na kufikiri zaidi ya mazoea.

Msomi ni kama mtafiti wa nafsi yake mwenyewe - haishi kuuliza “Kwa nini?”

Anapoona jambo, hachukui kama lilivyo; analipima, analitazama kutoka pande zote, kisha analeta tafsiri mpya yenye kuleta mwanga.

Msomi ni mtengenezaji wa fikra, si mtumiaji wa fikra za wengine.

Anaweza kuwa na shahada au asiwe nayo, lakini alichonacho ni hekima, si taarifa tu.

Mnukuzi ni nani?

Mnukuzi ni yule anayehifadhi maneno ya wengine bila kuyatafakari. 

Anaweza kukariri vitabu, kuzungumza kwa maneno makubwa, lakini hana nguvu ya kufikiri nje ya mipaka ya alichofundishwa.

Mnukuzi ni kama photocopy ya maarifa ya wengine. Anaweza kuonekana anajua, lakini mara nyingi hajui kwa undani - anabeba taarifa, si hekima.

Ni mtu anayejua kusoma, lakini hajui kutafakari.

Tofauti kati ya msomi na mnukuzi ni kama tofauti kati ya mchoro na msanii: mmoja ananakili, mwingine anatengeneza.
Kuwa na elimu na kuwa mjinga

Kuelimika ni zaidi ya kwenda shule. Ni uwezo wa kuelewa uhalisia, kujitambua, kufikiri kwa uwazi, na kutumia maarifa kwa manufaa ya dunia.

Ujinga, kwa upande mwingine, siyo kukosa kusoma - ni kukataa kufikiri, ni kujifungia katika mawazo finyu, ni kuishi bila kutaka kuelewa.

Ujinga ni kama kivuli - kila mtu anakibeba, lakini wenye hekima wanakigeuza kuwa funzo.

Kuelimika ni hali ya kufunguka kiakili na kiroho.

Ni kuona zaidi ya macho, kusikia zaidi ya masikio, na kufikiri zaidi ya kawaida.

Ni uwezo wa kutambua uhusiano kati ya mambo, kuishi kwa busara, na kutumia maarifa kutatua changamoto halisi.

Je, mtu aliyeelimika hawezi kuwa mjinga?

Anaweza kabisa.
Kwa sababu elimu ya darasani*l haiwezi kubadilisha akili iliyofungwa.

Mtu anaweza kuwa na PhD lakini akashindwa kuelewa namna ya kuishi na watu, au kufikiri kwa uhalisia.

Mjinga anaweza kuvaa suti ya elimu, lakini ndani akawa maskini wa fikra.

Kama alivyoandika Albert Einstein:  “Elimu si kujaza akili kwa taarifa, bali ni kufundishwa namna ya kufikiri.”

*LJe, kuna mtu asiye mjinga duniani?

Hakuna.
Kila mtu ana kipofu chake cha maarifa.
Kila mtu ana eneo analolitafuta bado.
Kila MTU ni mwanafunzi wa maisha; tofauti ni kwamba wengine wanajua kuwa wanajifunza, na wengine wanadhani wanajua kila kitu.

Hitimisho

Msomi huchunguza, mnukuzi hukariri.
Aliyeelimika hutenda kwa busara, mjinga *huishi kwa mazoea.

Ujinga si kosa, ila kubaki mjinga ni uamuzi.

Usiishi kama kioo cha fikra za wengine - kuwa taa inayoleta mwanga wa uelewa mpya.
Tambua, tafakari, elewa, kisha tenda.
Hapo ndipo utaanza safari ya kweli ya kuelimika.

Kama unataka kufungua upeo wako wa kufikiri, kuondokana na ujinga wa kifikra na kuishi maisha yenye mwanga wa ndani, jiunge na King Mentorship Program.

Hapa tunawafundisha watu *kuishi kwa kuelewa*, si kwa kurudia.

📞 Wasiliana nasi sasa: +255 744 284 329
🌐 King Mentorship Program -Building Conscious Thinkers for a New World.

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...