Usichanganye Imani, Kuwa na msimamo....

Ilikuwa asubuhi tulivu sana. Nikiwa bado nimelala, ghafla simu ikaita, namba ngeni! Kabla sijapokea, nilijiandaa kisaikolojia, nikaunda sauti yangu vizuri.

Nikapokea, “Hello,” 
Upande wa pili ukajibu:
“Mr King’ung’e?”
“Ndio mimi,” nikajibu.
Akasema: “Mr Shemson anaongea kutoka Dodoma!”

Mara moja nikatambua, “Huyu ni MC!” Kisha akaniambia:
 “Nina ombi, Unaweza kuandaa kipindi na kuhubiri kidogo kanisani kwangu?”

Nikamjibu: “Nashukuru sana kwa kuniona ninastahili na kwa kunipa nafasi hii ambayo sikuitarajia. Lakini hebu nikuulize, hadhira yako ni ya aina gani, na mafundisho haya yanalenga dhehebu gani?”

Akanijibu: “Ni kipindi cha dini, kitarushwa redioni. Hakina dhehebu maalumu, ni kwa wakristo wote.”

Nikasema: “Nipe muda nitafakari, kisha nitakurudia.”

Lakini moyoni, akili yangu, nafsi yangu, na roho yangu hazikuwa tayari. Nilimpigia my woman kumshirikisha. Akanijibu kwa hakika: “Don’t do it, najua ulichosimamia.”

Kwa adabu kubwa na unyenyekevu, nikampigia tena Mr Shemson, nikamwomba radhi kuwa sitaweza kutimiza hitaji lake.

Tukio hili liliniacha nikitafakari sana. Nikagundua kitu kimoja: maisha yangu yanaangaza; nipo katika nuru, na ninang’aa muda wote. 

Watu wengine wanaweza kuona mwanga huo na kutamani kushirikiana nao, lakini lazima ujue wapi unaposimama kiroho.

Kwa nini nilikataa?

Sijakataa MWITO kwa sababu sijui Biblia, hapana! Najua Biblia vizuri na ninaweza kuifundisha kwa kina. Bali ninajua pia *lugumu wa kiroho unaoweza kutokea.

Kila imani uliyo nayo, ina wigo wa roho zinazoiangalia na kuisimamia. 

Unapojiweka chini ya wigo wa imani fulani, roho hizo zinaanza kukutambua na kukupa msaada kwa kukunafuu kwa machache.

Lakini pale unapokosa msimamo, leo uko hapa, kesho uko pale; leo unasimama na hiki, kesho kingine, roho zinakuona kama *msaliti*.

Matokeo yake ni mabaya: mtu utaishia kupauka kukauka na kuharibikiwa kimaisha!

Wakemeaji wengi wana nguvu ya imani, lakini mara nyingi wanakosa elimu ya kina. Ni lazima tujiulize:

* Roho hizi zinatoka wapi?
* Mapepo tunayoyakemea yanatokea wapi?

Bila kuelewa majibu ya maswali haya, tutakemea kizazi hadi kizazi bila kupata suluhisho.

Hivyo basi, si kwamba nilikataa mwaliko kwa sababu ya woga au ujinga. La hasha! Nilijua uzito wa kile kilichokuwa kikiombwa. Nikachagua msimamo.

Leo napenda kukuuliza swali: *Je, wewe una msimamo wa kiroho?*

Ama unaishi maisha ya kuhamahama, kutafuta mwanga kidogo huku na kidogo pale?

Ninakiri kwa hakika: hakuna roho ya mtenda mabaya itakayoweza kunidhuru. Kwa sababu namjua Mungu Mwenye vyote na kile alichokifanya kwa viumbe vyake.

Kumbuka hili:

Ya Mungu huwaangazia walio thabiti.
Roho hutambua wenye msimNuru hubaki kwa walioamua kusimama imara.

Chagua msimamo wako leo, kwa sababu msimamo wako ndio ulinzi wako wa kiroho.

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...