USITAFUTE HELA BILA KUJUA MISINGI YAKE


Kabla hujamwambia huyo mja kwamba unataka uamuru hela iende kwake…

Na wewe mja kabla hujaenda kuombewa upate hela… tulia kwanza!
Ndiyo, tulia kwanza!

Ndugu zangu wachungaji, waumini, na wote mnaokimbilia madhabahuni kutafuta fedha bila kujua historia kamili ya fedha - naomba mnisikilize vizuri leo.

Mnadhani fedha zinashuka moja kwa moja kutoka kwa Mungu?

Mnadhani kuna maombi fulani yanaweza kuibadilisha sheria ya thamani?

Aaah! Ngoja nikusimulie kitu ambacho wengi wenu hamjawahi kuambiwa - kweli isiyopingika, iliyozikwa kwenye historia ya Watu.

Zamani za kale, kabla hata ya historia tuliyoisoma shuleni, kulikuwepo bara kubwa sana tuliloliita leo Antaktika.

Lakini wakati huo lilijulikana kwa jina lake la asili kama Sapriyango.

Katika kizazi cha Shudgil na Sebro, Watu waliingiliana na viumbe wa kutokea ulimwenguni waliotoka mbali sana- viumbe hawa wanajulikana kwa lugha ya Kibantu kama Konvodi.

Siku hizi, tungesema ni aliens, lakini jina lao la asili ni hilo.

Konvodi hawa walikuja na taaluma mpya kabisa duniani - taaluma ya kutengeneza fedha.

Lakini hawakuleta tu maarifa hayo; walileta pia uovu mwingi.

Ndiyo maana nakwambia, tangu mwanzo, fedha imebeba pande mbili: baraka na laana.

Antaktika ndiyo lilikuwa bara la kwanza duniani kufundishwa utengenezaji wa fedha.

Na mara tu baada ya utengenezaji huo kuanza, tamaa ikawa malkia, wivu ukawa mlinzi, na hila zikatawala.

Watu wakaanza kupigana, na ugomvi mkubwa ukazuka kati ya Watu na hawa Konvodi.

Vita vikubwa vikaanza - si vya panga na mishale tu, bali vita vya nguvu zisizo za kawaida.

Konvodi walitoka kwenye sayari ya makazi ya “malaika” - wale wanaoitwa wajumbe wa  wa Mungu. (Kumbe ni wajumbe wa mchongo TU.)

Kwa sababu ya watu wa bara lile kuingiliana na viumbe mbalimbali walitokea viumbe wengine wapiganaji wapya walioitwa Hezibriyo Luaganzi.

Hawa walikuja kusaidia Watu kupambana na Konvodi.

Lakini Hezibriyo Luaganzi walikuwa na silaha ya kutisha: waliweza kufua baridi kali sana.

Walileta upepo wa barafu ulioua viumbe wengi wasiohimili.

Baridi hiyo haikuchagua - iliua bila huruma.

Watu waliokimbia walikimbilia bara la Eyastugo (Ulaya) na wengine wakaenda Australia.

Na hivyo taaluma ya fedha ikasafirishwa hadi Ulaya, hasa katika eneo la Obiz - leo hii tunaiita Ujerumani.

Huko ndipo MTU aitwaye Jeremy Jidi Eyap alianza rasmi kutengeneza fedha au hella na kuanza kutumia fedha kwa kubadilishana vitu vya thamani.

Sasa sikiliza vizuri - hii si hadithi ya kubuni, ni kumbukumbu ya kweli.

Fedha imekuwepo duniani kwa takribani miaka 10,000 hadi sasa

Na kila mahali ilipoingia, iliweka maamuzi makubwa mikononi mwa MTU:
Kuchagua kuiweka kwa manufaa au kuipeleka kwenye maovu.

Lakini tatizo ni kwamba Watu wengi wameiacha misingi ya utu kwa sababu ya fedha.

Tazama historia ya Sapriyango - Watu waliuana, walikimbia makazi yao, viumbe wakafa, na bara zima likaachwa tupu isipokuwa wale Hezibriyo Luaganzi waliobaki kwenye baridi yao ya mauti.

Leo hii, tunaona taswira ile ile:

Wanafarakana kwa sababu ya fedha.
Wanauana kwa sababu ya fedha.
Wanang’ang’ania madaraka kwa sababu ya fedha.

Fedha ni chombo tu cha mabadilishano ya thamani kati ya kiumbe na kiumbe—si kitu cha kuacha utu wako!

Usiruhusu ebuko la kati kati ya maisha yako kiwe sababu ya kifo cha utu wako.

Rafiki, usipuuze funzo hili.

Tusiruhusu yaliyotokea Sapriyango yarudi tena kwenye dunia hii.

Na wewe, unayetafuta fedha bila kujua misingi yake - tulia kwanza.

Jua unachoshika mkononi kina historia ya damu, jasho, na mizozo.

Ukiishika vibaya, inaweza kuua. Ukiishika vyema, inaweza kubariki.

Na kwa kuwa ninakupenda sana.

Mwezi huu ninaadhimisha birthday yangu!
Na nimekuandalia zawadi maalum—KITABU changu kipya kinachoitwa:
"Fedha ni Haki Yako – Mwongozo wa Hatua kwa Hatua Kufikia Uhuru wa Kifedha"

Habari njema ni kwamba KITABU hiki nitakupa bure kabisa.

Ndiyo, bure kabisa- ni zawadi KWAKO kuonesha thamani ya uwepo wangu.

Ukihitaji kitabu hicho, jibu ujumbe huu kwa kuandika neno KITABU.

Ndimi Mbulwa
Sende Esupriy Dewo Ochi

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...