ACHA KUSUBIRI — TENDA MWENYEWE!
Bado kichwani mwako unawaza kuwa MUNGU atatenda kwa niaba yako?
Bado unalemaza akili kwa kutegemea kwamba Bwana akusaidie?
Kwa hiyo unafikiria MUNGU atoke kule aliko aje akutendee wewe?
Kwa upekee upi ulionao, ilhali upekee wa kweli ni wa MUNGU Mwenye vyote?
Je, wewe ni zaidi ya mende, kunguni, chawa na mamba na mijusi?
Ni jambo la kushangaza kuona mtu ameshindwa kuwajibika kisha anasema:
"Ninasubiri Mungu atende!"
Kumbuka: Mungu tayari ameumba maisha kabla hujazaliwa, bila kukuomba.
Ameandaa muujiza wake unaoendeleza maisha ya kila kiumbe hapa duniani.
Kakupa akili kichwani na uwezo wa kufanya mambo yatokee.
Leo hii unasema Mungu hakusaidii? Swali ni: Unataka msaada gani zaidi?
Kwenye maisha, ukweli ni huu:
Wewe mwenyewe una uwezo wa kufanya mambo yatokee.
Mimi nina imani hiyo - na najua wazi ni wajibu wangu kutekeleza MALENGO yangu ili maisha yangu yaende.
Nisipoweka kalamu mkononi na kuandika, Mungu hataniandikia.
Nisipopambana kutafuta fedha, Mungu hataniletea fedha - kwa sababu Yeye hatengenezi fedha.
Kwa maneno mengine, nina wajibu wa kusababisha mambo yatokee, si kusubiri yawe kama muujiza wa ghafla.
Maisha yako unapaswa kuyagawanya katika makundi mawili:
1. Mambo unayoweza kuyabadilisha
Tabia zako
Mawazo yako
Fikra zako
2. Mambo usiyoweza kuyabadilisha
Tabia za mtu mwingine
Mawazo yake
Fikra zake
Kwa upande wangu, sina kisingizio. Nimejiweka kama mhimili wa maisha yangu mwenyewe.
Sina wa kumlaumu.
Hata mtu mwingine akiniendea kinyume, sibaki na hasira - hubadilika ili kuendana na hali mpya ili malengo yangu yasikwame.
Lengo langu ni moja: Maisha yangu yaende kama ninavyotaka!
HITIMISHO:
Acha kusubiri msaada wa kutoka kwa ya MUNGU bila wewe kutenda.
Mungu hana jukumu la kutengeneza maisha yako - jukumu hilo ni lako.
Msaada ni wa viumbe hai, na wewe ni mmoja wao.
KOMAA, kwa sababu una uwezo wa kufanya mambo yatokee.
Ila katika kukomaa KWAKO usisahau kuomba kwa yake MUNGU yakunafuu Kwa machache.🙏😊
Wasifu wa Mwandishi
M’bulwa ni mwandishi, mnasihi na mwalimu wa maendeleo binafsi kupitia King Mentorship Program.
Amefundisha na kushauri makundi mbalimbali ya watu kuhusu utambuzi binafsi, ujasiriamali, na kujenga tabia za mafanikio.
Kupitia maandiko na mihadhara yake, M’bulwa amesaidia watu wengi kuacha kisingizio na kuchukua hatua ili kufanikisha ndoto zao.
Jiunge na King Mentorship Program
Je, uko tayari kuondoa vizuizi vya kifikra na kuanza kutumia uwezo wako wa ndani ili kufanikisha maisha unayotaka?
Jiunge na King Mentorship Program leo na ujifunze mbinu za:
Kujitambua
Kuvunja tabia zinazokurudisha nyuma
Kuamua na kutekeleza malengo yako
Kujenga ujasiri na nidhamu ya kifedha
📞 Wasiliana sasa: 0744 284 329
Comments
Post a Comment