BADILISHA VYANZO VYAKO VYA MAARIFA – BADILISHA MAISHA YAKO!
Ukweli mchungu ni huu:
Kila siku unayoishi, kila hatua unayochukua, kila jambo unalofanikisha - limejengwa juu ya kitu kimoja muhimu sana: kile unachoruhusu kiingie ndani ya akili yako.
Kila mtu ana ndoto. Wengi wanaota kuwa na maisha bora, magari makubwa, familia yenye furaha, biashara zenye mafanikio.
Lakini wachache sana hujua siri hii ndogo iliyo na nguvu ya kubadilisha maisha:
Ubongo wako ni kama shamba.
Kile unachokipanda ndicho utakachovuna.
Kama utapanda magugu kwa kuruhusu taarifa zisizo na maana, marafiki wasio na dira, muziki unaokupoteza au mazungumzo yenye kukushusha - usiwe na ndoto ya kuvuna mazao bora.
Lakini kama kila siku utaamua kuwekeza ndani yako, kusoma vitabu vinavyokujenga, kuzungumza na watu wanaokuinua, kusikiliza vipindi vya maarifa na kushirikiana na walimu wanaokutia moyo - basi maisha yako hayatahitaji muujiza mwingine; maisha yako yataanza kubadilika taratibu kwa njia za ajabu.
Wengi wamekosea hapa. Wanataka matokeo ya 100% bila kuweka mbegu yoyote.
Wanataka asubuhi waamke tajiri ilihali hawajachukua hata dakika moja kusoma, kujifunza, au kuwekeza kwenye akili zao.
Rafiki yangu, maisha hayana mahesabu kama hayo! Hata mtoto wa darasa la saba atakuambia: “Kama hujapanda mbegu, usitarajie mavuno.”
Sasa hebu jiulize kwa ujasiri:
Ni nini unachokilisha akili yako kila siku?
Ni taarifa zipi zinaingia ndani yako kupitia simu, runinga, marafiki, au hata mitandao?
Je, unajenga au unabomoa?
Ukweli ni huu:
Kile unachoruhusu kiingie kichwani mwako leo, ndicho kitakachojenga au kubomoa maisha yako ya kesho. Badilisha vyanzo vyako vya maarifa.
Tafuta maarifa kila siku. Jaza akili yako kwa taarifa zinazojenga na unyanyuke juu ya kila hali iliyokuamulia mipaka.
Usisubiri kesho. Usitafute miujiza.
Miujiza ipo ndani yako - katika vyanzo vya maarifa unavyovipokea kila siku.
Kuhusu Mwandishi
Emmanuel Samuel King’ung’e ni mwandishi na mhamasishaji anayefahamika kwa maneno yake yenye nguvu ya kuinua na kugusa maisha.
Amejitoa kusaidia watu kugundua kile walichobeba ndani mwao King Mentorship Program, programu inayotoa elimu ya utambuzi binafsi, maamuzi bora na mikakati ya maisha yenye mafanikio.
Jiunge na King Mentorship Program
Unataka kujifunza zaidi kuhusu jinsi ya kubadilisha vyanzo vya maarifa yako, kuvunja mipaka iliyoko kichwani mwako na kufanikisha maisha yako?
Jiunge sasa na King Mentorship Program!
📞 Mawasiliano: 0744284329
Kumbuka: Kile unachoruhusu kiingie ndani yako leo, ndicho kitakachobadilisha maisha yako ya kesho. Anza leo. Chukua hatua!*
Comments
Post a Comment