“Fedha Hazisikii Maneno, Zinafuata Mikakati.”
Katika zama hizi, imekuwa kawaida kusikia kauli kama “ukitaka kuwa milionea, jitamkie kila siku mimi ni milionea, kuwa na imani chanya, siku moja utakuwa.”
Hizi ni kauli zinazopendwa sana na motivational speakers duniani kote.
Lakini kuna swali muhimu ambalo watu wengi hushindwa kuuliza: Kama kujitamkia kunatosha, mbona wengi wanaotoa mafundisho hayo wenyewe hawajawa mamilionea licha ya kujitamkia zaidi ya watu wanaowahudhuria?
Huu ni ukweli ambao watu wachache wana uthubutu wa kuukubali: Mafanikio ya kifedha hayatokani na maneno - yanatokana na nidhamu, mikakati, na vitendo vinavyoakisi maamuzi yako ya kifedha.
Unaweza kuwa na maono, unaweza kuwa na mipango, lakini kama hutachukua hatua, tayari unaandika mkataba wa kushindwa.
Kwa sababu wengi wetu hatukutokea kwenye familia za kifalme au nyumba ambazo mali ni urithi wa kuzaliwa, safari ya mafanikio ya kifedha huwa ndefu na yenye changamoto.
Mara nyingi, kinachotukwamisha si umaskini; ni mtazamo wa kifedha uliojaa giza nene - ukosefu wa elimu ya kifedha, dhana potofu kuhusu fedha, na matarajio yasiyoendana na vitendo.
Makala hii haikusudii kukupa faraja, bali kukupa mwelekeo wa kivitendo - inakupa mikakati muhimu inayoweza kukusukuma kuanza safari ya mafanikio ya kifedha kuanzia leo.
1. Jenga Utamaduni wa Kujiwekea Akiba (Financial Preservation Culture)
Hatua ya kwanza ya mtu yeyote anayetaka kujijenga kifedha ni kujenga tabia ya kuweka akiba.
Jiwekee utaratibu wa asilimia ya kipato chako unayoweka akiba - lakini hakikisha si chini ya asilimia 10.
Mataifa yaliyoendelea kwa uchumi, kama Japan, Korea Kusini na Singapore, mafanikio yao yamejengwa juu ya utamaduni mmoja: “Savings-first culture.”
Wao huweka akiba kabla ya kutumia. Sisi wengi hapa tunatumia kabla ya kuweka akiba - na mwisho wa mwezi hakuna kinachobaki.
Usiweke akiba kwenye akaunti isiyotoa faida. Kila mwaka, thamani ya fedha hupungua kutokana na mfumuko wa bei, kwa hiyo ukiweka akiba bila faida, unajipunguzia nguvu ya ununuzi kimya kimya.
Kumbuka: Akiba ni mbegu; uwekezaji ni shamba.
Usiwe mtu anayeweka akiba bila malengo. Kama hujarithi utajiri, basi unapaswa kuujenga.
Anza kidogo, ongeza polepole, na ufikie kiwango unacholenga. Ukishafika, peleka fedha hizi zifanye kazi:mradi mdogo, hisa, kilimo cha muda mfupi, biashara ya mtandaoni, mali isiyohamishika ndogo ndogo.
Warren Buffett alianza kwa kuweka akiba ya senti chache alipokuwa na miaka 10. Shangazi yake ndiye alimfundisha utamaduni huo. Leo, dunia nzima inamnukuu.
Siri haijabadilika. Akiba = mwanzo wa uhuru wa kifedha.
2. Kuwa na Bajeti (The Blueprint of Wealth)
Bajeti ni dira ya matumizi yako. Ni mpango unaotabiri na kuongoza jinsi pesa itatumika kabla haijatoka mfukoni.
Bajeti inakupa nafasi ya kuamua matumizi yako kabla hayajakuamulia.
Kama hadi sasa hauna bajeti ya kila mwezi, ninakuonea huruma - kwa sababu safari yako ya mafanikio itakuwa ya kubahatisha.
Huhitaji kujitamkia “siku moja nitakuwa milionea.”
Unahitaji kuanza kupanga bajeti leo.
Mfano halisi: Watu wawili wanaweza kupata mshahara mmoja. Mmoja akiwa na bajeti, ataweza kuweka akiba, kupunguza matumizi ya ovyo, na kuwekeza. Yule asiye na bajeti ataishia kujiuliza kila mwezi, “Fedha zimekwenda wapi?”
Bajeti ndiyo inakutofautisha kati ya mtu anayepiga hatua na mtu anayeendesha maisha kwa matumaini pekee.
3. Kuwa na Nidhamu (The Global Wealth Principle)
Nidhamu ndiyo nguzo kubwa ya mafanikio ya kifedha. Kuwa na akiba kunahitaji nidhamu ya kutoyatumia hovyo.
Kufuata bajeti kama ilivyo pia kunahitaji nidhamu. Kukataa matumizi yasiyo ya lazima - mambo madogo madogo yanayoiba fedha zako kimya kimya - kunahitaji nidhamu ya hali ya juu.
Nidhamu ndiyo inakusaidia:
kuweka akiba hata kama una uchache,
kufuata bajeti hata kama kuna vishawishi,
kukataa matumizi yasiyo na tija,
kujizuia kuishi maisha ya kuonyesha uwezo ambao huna.
Haya mambo hayahitaji kuombewa.
Hayahitaji kufunga na kutubu.
Hayahitaji kulaani shetani.
Yanahitaji uwazi wa nafsi na nidhamu binafsi.
Wewe hujarogwa.
Hakuna mtu aliyekuharibia bahati.
Hakuna mkono wa mtu.
Unajikwamisha mwenyewe kwa maamuzi ya kifedha yasiyo sahihi.
Hicho ndicho kiini cha ukweli ambao watu wachache wanauzungumza kwa ujasiri.
Nahitaji mtu mmoja tu - aliyekomaa, aliyechoka kuishia palepale, na aliye tayari kushauriwa kuhusu nguzo tatu za mafanikio ya kifedha: Akiba, Bajeti, na Nidhamu.
Sitoi huduma ya bure.
Ukikuwa tayari, jibu ujumbe huu nami nitakupa utaratibu kamili.
Ndimi Mbulwa King'ung'e
📞 Mawasiliano: 0744 284 329
Comments
Post a Comment